Viongozi serikalini wabinafsi, wezi - Naibu Waziri wa Fedha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi serikalini wabinafsi, wezi - Naibu Waziri wa Fedha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 9, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Maulid Ahmed
  Tarehe: 9th November 2009

  NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi, Omar Yussuf Mzee amesema,viongozi serikalini ni wabinafsi, wanajali maslahi yao kuliko ya taifa.

  Mzee pia amesema, watendaji hao si waadilifu, wanashirikiana na wazabuni kuongeza bei za kununulia vifaa.

  Amewaeleza wabunge kuwa, hali hiyo imebainika tangu Sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004 ilipoanza kutumika.

  “Changamoto nyingine tangu kuanza kwa sheria hii ni uwepo wa viongozi wa umma wanaojali zaidi umimi kuliko utaifa”, amesema Mzee leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua semina ya siku mbili kwa wabunge kuhusu taratibu za ununuzi katika sekta ya umma.

  Mzee amewaeleza wajumbe wa semina hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), kuwa, kwa ujumla wamebaini kwamba, kuna uwezo mdogo wa usimamizi katika manunuzi serikalini.

  Wakati anawasilisha mada kuhusu umuhimu sekta ya manunuzi katika kukuza uchumi wa taifa, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk. Ramadhan Mlinga amesema, katika ukaguzi uliofanywa na mamlaka hiyo kwa taasisi za umma 100 imebainika kuwa, taasisi za umma zinatoa upendeleo wa zabuni kwa kampuni za watendaji wa taasisi za umma, ndugu zao au marafiki zao.

  “Kuna kupokea bidhaa duni au kazi zenye kiwango duni tofauti na ilivyoonyeshwa kwenye nyaraka za zabuni na mikataba na kunatozwa bei kubwa kwa ununuzi wa nyaraka za zabuni hata pale isipostahili”, amesema Mlinga.

  Kwa mujibu wa Mlinga pia walibaini kuwa,taasisi za umma zinaweka masharti magumu ya ushiriki wa zabuni, kutotangazwa zabuni kwa walengwa,na kuchukua muda mrefu kufanya tathmini hadi kumtangaza mshindi wa zabuni.

  Amesema, PPRA imejiwekea lengo kuwa hadi mwaka 2010 asilimia 80 ya taasisi zote za umma ziwe na uwezo wa kutekeleza ipasavyo sheria ya Ununuzi na kanuni zake.

  Wakati anawasilisha mada kuhusu sheria hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya chuo cha Manunuzi na Ugavi(IPS), Didas Masaburi, amewaeleza wabunge kuwa, sheria hiyo ya mwaka 2004 inahitaji kurekebishwa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali.

  “Sheria inasema zabuni zisigawiwe vipande vipande lakini wanafanya hivyo ili kukwepa kutangaza na pia bodi ya zabuni inateuliwa na Mkuu wa shirika au Katibu Mkuu lakini bodi hiyo hiyo imepewa uwezo wa kumchukulia hatua mkuu huyo hivyo si rahisi kumchukulia hatua mtu aliyewateua” amesema Masaburi.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Mmh kumekucha...waziri wa utawala bora kasema hakuna asie fisadi ccm...huyu nae serikali imejaa ubinafsi loh....haya bado waziri mkuu na makamu wa raisi waje na yao...hapa tushapata semi za waziri na naibu waziri klutudhihiiirishia uchafu wa ccm...nnape upo,...njo na wewe ya uvccm...usiogope bwana afukuzwi mtu si umeona mama zako na baba zako kule dododma
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ahsante kwa kupasua hili

  Lakini, hatutaki kutafuta cheap popularity. Tueleze ni viongozi gani, walifanya nini, wapi, ushahidi uko wapi ili wawajibishwe kikamilifu na liwe funzo kwa wengine.

  Maana bila kufanya hivyo utaleta matatizo mawili.

  1. Utaacha mafisadi waendelee kufanya ufisadi bila kudhibitiwa.

  2.Utawapaka matope viongozi wengine serikalini ambao hawahusiki na ufisadi huu, kwani kauli hii bila majina na details itaonekana ku apply kwa viongozi wote serikalini.naamini kuna wengine, hata kama ni wachache, ambao hawahusiki na haya.

  Kwa hiyo ndugu naibu Waziri ili kumaliza vita hii uliyoanzisha mwaga details hizo uonekana kweli unamaanisha unachosema. Ama sivyo utaonekana msanii unayetaka kuitumia vita dhidi ya ufisadi kujipatia umaarufu tu, hususan wakati huu ambao uchaguzi unajongea.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Yeye ni kiongozi? Ndiyo.Yeye yuko serikalini? Ndiyo. Hivyo basi yeye ni:
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  mbinafsi

  yeye ni mwizi

  yeye ni fisadi
   
 6. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  'Viongozi serikalini wabinafsi, wezi'

  Imeandikwa na Maulid Ahmed

  NAIBU Waziri wa Fedha na Uchumi, Omar Yussuf Mzee amesema,viongozi serikalini ni wabinafsi, wanajali maslahi yao kuliko ya taifa.

  Mzee pia amesema, watendaji hao si waadilifu, wanashirikiana na wazabuni kuongeza bei za kununulia vifaa.

  Amewaeleza wabunge kuwa, hali hiyo imebainika tangu Sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004 ilipoanza kutumika.

  “Changamoto nyingine tangu kuanza kwa sheria hii ni uwepo wa viongozi wa umma wanaojali zaidi umimi kuliko utaifa”, amesema Mzee leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua semina ya siku mbili kwa wabunge kuhusu taratibu za ununuzi katika sekta ya umma.

  Mzee amewaeleza wajumbe wa semina hiyo iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), kuwa, kwa ujumla wamebaini kwamba, kuna uwezo mdogo wa usimamizi katika manunuzi serikalini.

  Wakati anawasilisha mada kuhusu umuhimu sekta ya manunuzi katika kukuza uchumi wa taifa, Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk. Ramadhan Mlinga amesema, katika ukaguzi uliofanywa na mamlaka hiyo kwa taasisi za umma 100 imebainika kuwa, taasisi za umma zinatoa upendeleo wa zabuni kwa kampuni za watendaji wa taasisi za umma, ndugu zao au marafiki zao.

  “Kuna kupokea bidhaa duni au kazi zenye kiwango duni tofauti na ilivyoonyeshwa kwenye nyaraka za zabuni na mikataba na kunatozwa bei kubwa kwa ununuzi wa nyaraka za zabuni hata pale isipostahili”, amesema Mlinga.

  Kwa mujibu wa Mlinga pia walibaini kuwa,taasisi za umma zinaweka masharti magumu ya ushiriki wa zabuni, kutotangazwa zabuni kwa walengwa,na kuchukua muda mrefu kufanya tathmini hadi kumtangaza mshindi wa zabuni.

  Amesema, PPRA imejiwekea lengo kuwa hadi mwaka 2010 asilimia 80 ya taasisi zote za umma ziwe na uwezo wa kutekeleza ipasavyo sheria ya Ununuzi na kanuni zake.

  Wakati anawasilisha mada kuhusu sheria hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya chuo cha Manunuzi na Ugavi(IPS), Didas Masaburi, amewaeleza wabunge kuwa, sheria hiyo ya mwaka 2004 inahitaji kurekebishwa ili kukabiliana na changamoto mbalimbali.

  “Sheria inasema zabuni zisigawiwe vipande vipande lakini wanafanya hivyo ili kukwepa kutangaza na pia bodi ya zabuni inateuliwa na Mkuu wa shirika au Katibu Mkuu lakini bodi hiyo hiyo imepewa uwezo wa kumchukulia hatua mkuu huyo hivyo si rahisi kumchukulia hatua mtu aliyewateua” amesema Masaburi.

  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=4312
   
 7. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Kila Mtu anasema Lwake sasa...Kuna Mmomonyoko mkubwa wa maadili kwenye serikali ya Muungwana...Serikali imekuwa kama danguro,hakuna heshima hata kidogo!Inasikitisha...Historia itawaumbua hawa watawala.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Mimi namtolea uvivu Jumatano hii;
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Kumbe hata serikalini nako kuna makundi kama bungeni? Kweli tunayoyaona ni kivuli cha kuendesha mambo yetu kwa misingi ya uongo uongo
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama WaTz wanajua maana ya sheria! It appears to be a grossly misunderstood concept!
   
 11. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nashukuru kwa kupasua jibu kwani tusiposhiriki vita hii ya kujitolea basi nchi hii itageuka nchi ya kifisadi. Hivi mp haoni haya?? Au na yeye ana ndugu??? Ni mzabuni?
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180

  Hakuna serikali hapa, it is agroup of selfish comedians masquerading as a government!!
   
 13. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nayeye pia yumo asiwasingizie wenzie apate umaarufu kirahisi... km analijua hilo kachukua hatua gani tangu agundue hayo mauchafu???
   
Loading...