Viongozi serikalini nao kujivua gamba

Umslpogaaz

Member
Apr 14, 2008
94
56
Viongozi serikalini nao kujivua gamba

By Jukwaa Huru on July 29, 2011

nape1.jpg
Nape Nnauye

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema baada ya kumalizika kwa mchakato wa kuvua gamba ndani ya chama, mpango huo utahamia kwa viongozi wa Serikali ambao si waadilifu na wameonekana ni mzigo kwa Taifa. Nnauye alisema hayo juzi wakati akijibu maswali ya baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS) na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Askofu Stephano Moshi (SMMUCO).

Wanafunzi hao walitaka kufahamu msimamo wa CCM kwa baadhi ya mawaziri akiwemo Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja waliyedai ameshindwa kutekeleza majukumu yake na wizara yake kusababisha mgawo wa umeme ambao pia unaathiri uchumi wa Taifa.

Pia walihoji sababu za Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi kutojiuzulu licha ya mabomu kulipuka katika kambi ya Mbagala na baadaye Gongo la Mboto na kuua wananchi wasio na hatia.
"Chama kimewabana baadhi ya viongozi wake waliokuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu, wamejivua gamba…leo hii wapo baadhi ya mawaziri akiwemo Ngeleja ambao pamoja na kutofanya vizuri hawataki kuwajibika," alisema.
Akizungumzia kauli hiyo, Nnauye alisema chama kimepanga kujisafisha na pamoja na mchakato kuendelea ndani ya chama lakini suala la kujivua gamba ndani ya Serikali haliepukiki.

"CCM ni chama makini sana na ninyi mnajua, hilo lisiwape shaka tunafanya mambo kwa hatua moja baada ya nyingine…hao watendaji mnaodhani wanaachwa watavuliwa gamba kama ilivyotokea kwa wengine," alisema.
Hata hivyo, hoja ya Ngeleja kujiuzulu ilishawahi kujibiwa ambapo suala la mgawo wa umeme lilifafanuliwa kuwa lilitokana na ukame uliopunguza maji katika mabwawa ya kufua umeme na hivyo kupunguza uzalishaji wa nishati hiyo.

Pia ilifafanuliwa kuwa mgawo huo umechangia na uwekezaji mdogo katika sekta hiyo kwa muda mrefu wakati mahitaji yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa.

Kuhusu kujiuzulu kwa Dk. Mwinyi, wakati wa bajeti ya wizara hiyo, alifafanua kuwa kiongozi anapaswa kuwajibika kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake na sio baada ya ajali kutokea katika wizara yake.
 
Nadhani watakuwa wamemnukuu vibaya...

huwezi kutumia maneno haya tena..."KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema baada ya kumalizika kwa mchakato wa kuvua gamba ndani ya chama, mpango huo utahamia kwa viongozi wa Serikali ambao si waadilifu na wameonekana ni mzigo kwa Taifa..."
 
Viongozi serikalini nao kujivua gamba

By Jukwaa Huru on July 29, 2011

nape1.jpg
Nape Nnauye

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema baada ya kumalizika kwa mchakato wa kuvua gamba ndani ya chama, mpango huo utahamia kwa viongozi wa Serikali ambao si waadilifu na wameonekana ni mzigo kwa Taifa. Nnauye alisema hayo juzi wakati akijibu maswali ya baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS) na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Askofu Stephano Moshi (SMMUCO).

Wanafunzi hao walitaka kufahamu msimamo wa CCM kwa baadhi ya mawaziri akiwemo Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja waliyedai ameshindwa kutekeleza majukumu yake na wizara yake kusababisha mgawo wa umeme ambao pia unaathiri uchumi wa Taifa.

Pia walihoji sababu za Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi kutojiuzulu licha ya mabomu kulipuka katika kambi ya Mbagala na baadaye Gongo la Mboto na kuua wananchi wasio na hatia.
“Chama kimewabana baadhi ya viongozi wake waliokuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu, wamejivua gamba…leo hii wapo baadhi ya mawaziri akiwemo Ngeleja ambao pamoja na kutofanya vizuri hawataki kuwajibika,” alisema.
Akizungumzia kauli hiyo, Nnauye alisema chama kimepanga kujisafisha na pamoja na mchakato kuendelea ndani ya chama lakini suala la kujivua gamba ndani ya Serikali haliepukiki.

“CCM ni chama makini sana na ninyi mnajua, hilo lisiwape shaka tunafanya mambo kwa hatua moja baada ya nyingine…hao watendaji mnaodhani wanaachwa watavuliwa gamba kama ilivyotokea kwa wengine,” alisema.
Hata hivyo, hoja ya Ngeleja kujiuzulu ilishawahi kujibiwa ambapo suala la mgawo wa umeme lilifafanuliwa kuwa lilitokana na ukame uliopunguza maji katika mabwawa ya kufua umeme na hivyo kupunguza uzalishaji wa nishati hiyo.

Pia ilifafanuliwa kuwa mgawo huo umechangia na uwekezaji mdogo katika sekta hiyo kwa muda mrefu wakati mahitaji yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa.

Kuhusu kujiuzulu kwa Dk. Mwinyi, wakati wa bajeti ya wizara hiyo, alifafanua kuwa kiongozi anapaswa kuwajibika kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake na sio baada ya ajali kutokea katika wizara yake.

mmeshamaliza kuvua gamba? duh ehee
 
Ye kama nani awe na mamlaka ya kuwawajibisha watumishi wa uma?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom