Viongozi ombeni ushauri kwa Rehema Nchimbi kuhusu suala la wamachinga

COMOTANG

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
1,756
2,000
Nina shauri kwa suala la Wamachinga, Viongozi mtafuteni Rehema Nchimbi awasaidie ushauri na jinsi ya kuweka utaratibu mzuri katika kuwapanga machinga.

Kwani Mama huyu aliweza kutenga maeneo, kupanga na kuweka utaratibu mzuri Sana kwa machinga wa Dodoma, kipindi akiwa Mkuu wa mkoa. Tulifanya biashara kwa Uhuru, na amani ilitawala kwa machinga, raia watu wa kawaida na wafanyabiashara nyingine.
 

AbouZakariya

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
1,378
2,000
Kwa wenye kumbukumbu, wakumbuke miaka ya nyuma mtaa wa lumumba kuanzia makutano ya uhuru ulikuwa unafungwa baadhi ya siku katika wiki kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo.
Inawezekana.

Pia mtaa wa Kongo Kariakoo, ni mtaa ambao wafanyabiashara wadogowadogo wamekuwa hapo kwa miongo kadhaa sasa, cha msingi ni kuwatengea maeneo yao maalum yenye huduma zote za muhimu.

Inawezekana.
 

Abdalah Abdulrahman

Senior Member
Aug 29, 2019
188
250
suala la wamachinga linachukuliwa kisiasa,mfumo wa vitambulisho na kuwaweka mahali tengefu ndio utakua mwarobaini.Wamachinga hawawezi kupangika bila ushiriiano kati ya wananchi na serikali
 

Juma chief

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
2,683
2,000
Suala la machinga na serikali ni kama kujaribu kuzipanga karatasi kwenye upepo uvumao....
 

Mtafiti77

JF-Expert Member
Oct 31, 2011
1,534
2,000
Kwa wenye kumbukumbu, wakumbuke miaka ya nyuma mtaa wa lumumba kuanzia makutano ya uhuru ulikuwa unafungwa baadhi ya siku katika wiki kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo.
Inawezekana.

Pia mtaa wa Kongo Kariakoo, ni mtaa ambao wafanyabiashara wadogowadogo wamekuwa hapo kwa miongo kadhaa sasa, cha msingi ni kuwatengea maeneo yao maalum yenye huduma zote za muhimu.

Inawezekana.
Hii ni kupunguza tatizo tu mkuu. Si suluhu ya tatizo hata kidogo kwa sasa. Hawa watu ni wengi mno. Pia, asili yao ni kumfuata mteja alipo. Hivyo, kuwapa hizo barabara kwa muda hakutoshi,lazima kuna watakaoendelea kuuza maeneo mengine yasiyoruhusiwa.

Ninachokiona, ni lazima ubabe unaojali maslahi ya watu ufanyike. Tenga maeneo kama hizo barabara au maeneo tu ya wazi, wapeleke huko, kisha asinuse mtu mabarabarani. Hii ibaki kuwa kanuni miaka yote hadi mtanzania atakapokubali kununua vitu eneo rasmi.Yani afuate bidhaa.

Ubaya wanasiasa ni wanafiki, hapo vuta kasi,mpaka uchaguzi ukikaribia, tutaona mengine. Pia akija kiongozi mwingine tunaweza ona mengine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom