Viongozi ombeni ushauri kwa mama Rehema Nchimbi kuhusu suala la wamachinga

COMOTANG

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
1,728
2,000
Nina shauri kwa suala la Wamachinga, Viongozi mtafuteni Mheshimiwa MAMA REHEMA NCHIMBI awasaidie ushauri na jinsi ya kuweka utaratibu mzuuri katika kuwapanga machinga.

Kwani Mama huyu aliweza kutenga maeneo, kupanga na kuweka utaratibu mzuri Sana kwa machinga wa Dodoma, kipindi akiwa Mkuu wa mkoa. Tulifanya biashara kwa Uhuru, na amani ilitawala kwa machinga, raia watu wa kawaida na wafanyabiashara nyingine.
 

AbouZakariya

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
1,364
2,000
Kwa wenye kumbukumbu, wakumbuke miaka ya nyuma mtaa wa lumumba kuanzia makutano ya uhuru ulikuwa unafungwa baadhi ya siku katika wiki kwa ajili ya wafanyabiashara wadogowadogo.
Inawezekana.

Pia mtaa wa Kongo Kariakoo, ni mtaa ambao wafanyabiashara wadogowadogo wamekuwa hapo kwa miongo kadhaa sasa, cha msingi ni kuwatengea maeneo yao maalum yenye huduma zote za muhimu.

Inawezekana.
 

Abdalah Abdulrahman

Senior Member
Aug 29, 2019
187
250
suala la wamachinga linachukuliwa kisiasa,mfumo wa vitambulisho na kuwaweka mahali tengefu ndio utakua mwarobaini.Wamachinga hawawezi kupangika bila ushiriiano kati ya wananchi na serikali
 

Juma chief

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
2,681
2,000
Suala la machinga na serikali ni kama kujaribu kuzipanga karatasi kwenye upepo uvumao....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom