Viongozi na wanasiasa waache kujipa majina yao katika mitaa, Shule au Hospital

kupe

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
1,035
326
Nianze Kwa haraka haraka kuna daraja la Mfugale. Soko la Ndugai.. Shule ya Jokate huko kisarawe.. Shule ya Juma Homera huko Tunduru ... Hospital ya.... Mtaa wa.... Na wengineo wengi... inakuwaje wanajipa haya majina au huyo anayewapa anawapa kwa kigezo gani. Maana mfano Ole Sabaya angejipa mtaa kule wilaya ya Hai au shule au barabara ... Na leo ije igundulike kuwa ni mharifu au jambazi na akafungwa itakuwaje hiyo shule au hospital itumie jina la mfungwa au mharifu.. Jambazi.. Mwizi...

Ushauri wangu majina yatolewe baada ya viongozi kustaafu au kufariki na kuthibitika pasipo shaka kuwa wapo safi.

Asante.
 
Ndo esense na lengo liko hivyo, na ndo wafanyavyo nchi za wenzetu, ni ngumu kuamini mhuni kama jokate kuitwa shule ambayo wanetu wanasoma, je vipi kesho ya hawa wanaojiit viongozi tunaijua?
 
Tena hayo majina yakapitie bungeni ndio mtu apewe hiyo heshima
 
Ndo esense na lengo liko hivyo, na ndo wafanyavyo nchi za wenzetu, ni ngumu kuamini mhuni kama jokate kuitwa shule ambayo wanetu wanasoma, je vipi kesho ya hawa wanaojiit viongozi tunaijua?
Kama kila mkuu wa mkoa au wilaya atajipa jina nchi itakuwaje!?? Mbona miaka nyuma wamwpita wakuu wengi wa mikoa hali haikuwa hivi!?? Tatizo la hawa wa sasa hasa waliotokana na Magufuli wengi ni washamba na malimbuken wanajiona miungu watu
 
Kiuungwana, ili sehemu iitwe kwa jina lako basi kuwepo na sababu mojawapo katika hili.
1. Uwe marehemu. (Kumbukumbu ya heshima)
2. Uwe umestaafu (Asiwe na mamlaka yoyote ya kushawishi hilo kutendeka).

Bahati mbaya sana, hapa Tz viongozi wanajipa majina maeneo wakati bado wako hai, hawajui wanajichulia kufa au kustaafu. Mifano hai ni hii
-Stand ya Magufuli (hakuchukua round akafa kwa Corona!?)
-Kijazi interchange (naye akafa)
-Daraja la Mfugale (naye kafa).
-Soko la Ndugai (Huyu bado bado)
 
Ni upuuzi kujitukuza!!
 
Back
Top Bottom