Viongozi na wanasiasa, ninyi ni wafungwa na mahabusu watarajiwa. Wekeni mazingira safi huko selo

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Kwa mfumo wa siasa za Tanzania zilipofikia kila mtu ni mahabusu au mfungwa mtarajiwa isipokuwa kwa wale wenye kinga.

Naomba kwa nafasi zeni wekezeni kutengeneza mfumo wa kisheria unalazimisha vyombo vya dola visirundike watu mahabusu na gerezani bila ushahidi.

Wekezeni kutengeneza mfumo unaoruhusu dhamana kwa watuhumiwa waliowengi kuliko Sasa mlipotengeneza sheria nyingi zinazozuia dhamana.

Mpunguzieni DPP mamlaka ya kupoka Uhuru wa watu, dhamana ibaki kuwa jukumu la mahakama si jukumu la DPP

Wekezeni kujenga selo Bora na Magereza Bora

Wekezeni kuboresha mfumo wa sheria,.

Kuna siku mtanikumbuka mtakapoitwa watuhumiwa hata mkiwa hakuna kosa mlilotenda.waulizeni wafanyabiashara na wanasiasa ambao wameonja joto ya Magereza watawasimulia.

Nanyi matajiri, tumieni influence zenu kutafuta Uhuru kupitia misingi imara ya kisheria inayokuakikishia Uhuru wakati wote. Mkiendelea kujikomba biashara zenu zitatumika Kama fimbo kwa tuhuma zisizo na mashiko zinazoambstana na kamata kamata for bargaining
 
Africa hakuna viongozi ambao ni responsible. Uwajibikani ni negative yani ni under zero percent.

Unalozungumzia ni feasible katika nchi za wanaojielewa tu wala sio huku kwetu.

Huku utasikia "mkurugenzi atumbuliwa kwa ufisadi" lakini hutawahi sikia amefikishwa mbele ya Pilato kwa makosa yake didhi ya umma wa "wanyonge" (kama kweli wapo hao wanyonge).

Bull crap TZ.
 
Back
Top Bottom