Viongozi na wana ccm mnapaswa kuitafakari kauli hii ya baba wa taifa kuwa" ccm si mama yangu" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi na wana ccm mnapaswa kuitafakari kauli hii ya baba wa taifa kuwa" ccm si mama yangu"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Oct 5, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,032
  Likes Received: 37,800
  Trophy Points: 280
  Katika kumbukumbu zangu kama sikosei baba wa taifa,marehemu mwalimu Nyerere,aliwahi kusema kwamba"... ccm si mama yangu..".Bila shaka kauli hii ya baba wa taifa ilimanisha kuwa, hatasita kujitoa ccm siku chama hiki kitakapokwenda kinyume na misingi ya kuanzishwa kwake.

  Watanzania wenzangu hebu tujiulize hii ccm ya leo imeshafanya mambo mangapi na mazito ambayo kama tungekuwa na watu makini ndani ya ccm wangeshajiondoa tangu siku nyingi.Kufanya makosa ni jambo la kawaida, ila kama hakuna hatua za kuridhisha kurekebisha makosa hayo ni nini wanasiasa ndani ya ccm walipaswa kufanya kama sio kujiondoa kama kweli ni wazalendo?

  Kuna wana ccm kila siku wanalia na ufisadi,rushwa na wizi ndani ya chama na serikali na hakuna hatua za kuridhisha zinazochukuliwa ila bado wamo tu.Kuna wana ccm wamelalamika kutendewa uovu kama kulishwa sumu kama ambavyo baadhi yao walivyolalamika hadharani,wengine kuambiwa kuwa si raia n.k ila bada wamo tu.Hii ni mifano michache tu ila bado wamengangana tu ndani ya ccm.Hivi huku si kuwa mtumwa wa chama cha siasa.

  Ukitafakari kwa makini utagundua wengi wao hawafanani kimawazo na kimtizamo na muasisi wa chama chenyewe ambae misingi ya chama kwake ilikuwa kitu muhimu zaidi ila hawa wa leo kwa muhimu zaidi ni madaraka tu.Ukweli ni kwamba wengi wao wanavumilia minyukano na siasa za makundi ndani ya chama sio kwa sababu wanakipenda chama bali ni kwasababu wanapenda madaraka na hasa ya uraisi,uwaziri n.k ambayo kwa mtizamo wao wanaamini ukitoka ccm huwezi kutimiza malengo hayo.Kwahiyo wako radhi kuendelea kunyanyasika kama kulishwa sumu,kutoswa katika chaguzi n.k kwa kulinda madaraka waliyonayo au yale wanayotarajia kuyapata kwa kubaki ndani ya ccm.

  Hakika huu ni uthaifu mkubwa kwani wengi wao walipaswa kujiondoa wenyewe tangu siku nyingi tu.Na kwa kutumia udhaifu huu ndio maana kigogo mmoja hivi karibuni aliwataka wale ambao hawakuridhika na mchakato wa kuwapata wajumbe wa NEC kujiondoa ccm na si kulalamika.Alisema hivyo kwa kujua udhaifu huu na aliamini hakuna atakaethubutu kujiondoa na mpaka leo wanaishia kulalama tu kama ilivyo ada. Achani kuwa watumwa wa vyama vya siasa na mtambue hizi ni zama za siasa za vyama vingi na ukiona hakuna haki jiondoe kama kweli wewe ni mwanasiasa uliekomaa na unajiamini.

  Tanzania itajengwa na wana ccm na wasio wana ccm.
   
Loading...