Viongozi na ukafiri wao ktk siasa za tanzania

bakuza

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
490
225
Ni nini maana ya neno Kafiri hapa?
Kafir (Arabic: -- kāfir; plural -kuffār) The term refers to a person who rejects God or who hides, denies, or "covers" the truth.

Nimelitumia neno kafiri kuelezea mwenendo mzima wa siasa,wanasiasa na wafuasi wa siasa jinsi walivyoinajisi nchi kwa kutofuata misingi sahihi ya vyama na itikadi zake katika nchi.Chama cha mapinduzi(ccm) abacho waasisi wake walikijenga juu ya misingi na itikadi ya ujamaa na kujitegemea lakini baada ya kulivunja Azimio la Arusha na kuibua Azimio la Zanzibar ndipo chama kiliendeleza nyimbo na ngoma za kijamaa na kujitegemea huku wana CCM wakicheza kipepari badala ya itikadi yao na hii imeleta shida nyingi katika Taifa kwa kukosa utulivu wa kisiasa na kiuchumi.

CCM kama chama Tawala kimekosa mwelekeo kwa waamini wake wa ni kipi cha kukiamini kwa sababu msaafu wake unaamini katika ujamaa na kujitegemea na ndiyo mafundisho ya chama lakini viongozi wake hawaamini katika hilo.Hapa ndipo msemo usemao fuata maneno yake na usifuate matendo yake unapodhihiri ndani ya chama na wanachama wake na kukikosesha chama weledi katika tasinia nzima ya uongozi.
CCM kimekuwa na makundi(wanamtandao) tangia uwepo wa Hayati Baba wa Taifa JK Nyerere mpaka ilipelekea kuwafukuza chamani baadhi ya wanachama wake kama Maalim Seif Sharif Hamad na wenzake lakini hilo halikuondoa uimara wa chama maana kiliendelea kuwa na nguvu za kimaamuzi kupitia secretariat yake.Kufikia Mwaka 2005 chama kilinyanganywa nguvu na uwezo wake wa kuamua mambo yake na makundi yaliyoibuliwa na mbio za kuwania madaraka hasa Urais yakiratibiwa vyema na Jk,Edward Lowassa Rostam Azizi na wenzao katika kila mkoa na wilaya zote nchini.Makundi haya yaliyotumia ushawishi wa nguvu ya pesa kwa viongozi wa kada zote ndani ya chama na hata vyombo vya habari yaliweza kujijenga vyema na kuwa na nguvu ktk vikao vya juu vya chama na hili lilidhihilishwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete pale alipokuwa akihojiwa na Tido Mhando mara baada ya kushinda Urais.
Kundi hili lilipingwa na Mangula wakati huo akiwa Katibu mkuu wa Chama na wengine wengi ambao waliitakia nchi mema na walijua wanamtandao wakiachwa waishike nchi kutakuwa ni kuweka rehani nchi na chama kwa ujumla,lakini nasikitika hawakuweza kushinda pale ambapo Mwenyekiti wake pia Rais wa wakati huo Benjamin Mkapa alipoweka mbele maslahi ya chama na kuyaacha maslahi ya nchi kwa kumkubali chaguo la wanamtandao badala ya chaguo la Chama na yeye mwenyewe hapo kabla.Mkapa alifanya hivyo kuogopa chama kisimfie mikononi hasa baada ya kutishwa kama angeendelea na msimamo wa chaguo lingine basi hawa wangekihama CCM na kwenda chama cha upinzani yaani CHADEMA ndipo Mr. Clean akajikuta anacheza ngoma ya wanamtandao ambayo kwa ndani hakuitaka.
Baada ya kuingia ikulu Rais Kikwete hakuchelewa kulipa visasi kwa kumpiga chini Mangula aliyepinga uteuzi wake na badala yake akalipa fadhira kwa kuwapa vyeo bila kujari uwezo wao wale wote walioshiriki kwa njia moja ama nyingine kumuingiza ikulu,akiwamo Mwandishi Salvatory Rweyemamu,mawaziri,makatibu wakuu na wakuu wa idara mbalimbali na machungu ya sakata hilo tunayajutia leo na hata miaka mingi ijayo.
Wanachama wa kada ya chini waliobaki CCM ni wale ambao ni mashabiki wa chama na si waumini wa chama.Tofauti ya mshabiki na muumini wa chama ni kuwa mshabiki hushabikia na kupigia vigeregere kwa chochote kile kinachosemwa ama kufanywa na upande anaoushabikia bila kujari kama ni kizuri au kibaya na lakini unapokuwa muumuni ina maana unachambua sera na itikadi za chama na unazikubali kuzifuata lakini inapotokea zikaachwa basi muumini hukemea na ikishindikana husitisha uumini wake ktk kundi hilo mara moja bila hata kugeuka nyuma.Waumini wa CCM waliobaki ni wanaCCM wasio hai(wanachama wafu) kwa maana kwamba hata kadi zao hawazilipii ada na hawashiriki ktk shughuli za chama ipasavyo kwa sababu ya kukata tama na mwenendo mzima wa Chama.CCM IKO WAPI KWA SASA MWISHO WAKE NINI?
CCM kama chama cha siasa kipo kwa jina na usajiri wake wa kudumu japo hakina itikadi ya kufuata hasa kwa mkanganyiko wake katika kuisimamia itikadi ambayo ni msingi wake yaani ujamaa na kujitegemea.Viongozi na watawala ndani yachama hiki wamekuwa ni makafiri wasiofata miongozo ya chama na itikadi zake.Wamebaki na itikati za waasisi ndani ya midomo yao na vitabu ila vitendo vyao vyote ni vya kibepari kwa maana nyingine ni mabepari ndani ya suti ya ujamaa na kujitegemea.
Tulikuwa na misingi miwili ya kufuata katika siasa:-
i.Ujamaa
ii. Kujitegemea
Wameukataa ujamaa kwa madai kuwa umeshindwa sawa tunakubali na Kujitegemea je nako kumeshindwa ama hatutaki kujitegemea?

Hapo ndipo wanachama wa kada halisia yaani sisi wakulima na wafanya kazi tulipokonywa chama mikononi mwetu na kukiweka mikononi mwa mabepari ili tuwe watumwa ndani ya nchi yetu na tayari tumekuwa watumwa hilo halina ubishi labda kwa asiyejitambua ndiye halioni hili.
Ila ndugu zangu wanaCCM ili tuweze kufikia mahala tukasimama upya na nchi kwenda katika maadili na kufuata misingi stahiki ya maendeleo na kujivua hii minyororo ya utumwa tuliyovishwa na hawa viongozi lazima tukubari maumivu na kuchukuwa maamuzi magumu ya kuwaadhibu wote waliotufikisha hapa tulipo na hakuna njia nyingine ya kuwaadhibu bali nikukiweka chama pembeni kwa miaka mitano hadi kumi ili kikajipange upya nje ya majukumu mazito ya kuendesha dola kwa kuiangalia misingi ya chama (Ili mbegu ije mpya lazima ife na kuzikwa).
Hii ya kukiweka pembeni chama katika uchaguzi itatusaidia nini?
Ngoja nikupe mambo kadhaa ambayo ndiyo sababu ya mimi kutamka hivyo:-
1. Wanamtandao wapo ndani ya chama kuchuma mali za watanzani kwa maslahi yao binafsi.

2. Wanamtandao wapo humo kulinda maslahi yao ya kibiashara ili yasiguswe na serikali
3. wapo ili kurahisisha kupata upendeleo ktk mambo yasiyohitaji upendeleo kama kukwepa kodi.
4. Kutimiza matakwa ya mabwana zao wa magharibi ambao wamewasaidia kwa njia moja ama nyingine kuwa madarakani.

5……..n.k
Kwa mantiki hii tukikiweka chama pembeni hakika hawa waliokivamia chama watatoka na kukiacha chama kwa wazalendo wa kweli kwa sababu wataona chama hakina tena uwezo wa kuwatimizia matakwa yao ya kifisadi na hapo ndipo chama chaweza kujiimarisha kwa muda huo na kurudi madarakani,kikiwa na miongozo ya kueleweka na imara zaidi.Nasema kurudi madarakani kwa sababu bado CCM ina sera bora ambazo kupitia kwa hawa wahujumu wa nchi,hizi sera haziwezi kutekelezeka ila wakirudi kwa mwonekano wa kuzisimamia basi wananchi watakirejesha madarakani kwa muda huo bila shaka yoyote.


MAONI YANGU KWA WATANZANIA
Ningekuwa na uwezo basi kitu cha kufanya ni kuwapa elimu watanzania ili kila mmoja ajitambue na si kushawishi ahame chama A alichomo na kwenda chama B maana naamini kama watanzania tutajitambua basi tutapiga kura pale penye maslahi na nchi yetu hata tusipohama vyama.Mtindo kama huo ulifanyika Kenya wakaweza kuiondoa KANU madarakani wakiwa ndani ya chama hicho. Huwezi kufanya mabadiliko yenye manufaa kwa wananchi kwa kuwaondoa mawaziri hata wangekuwa wote bila kubadili mfumo mzima ambao ndiyo unazalisha watendaji wa aina hiyo.Kama tuna kumbukumbu nzuri basi zoezi la kuwaondoa mawaziri limefanyika mara nyingi lakini halikuwa na tija kwa taifa maana kila aliyeingia alikuwa na tabia hizo hizo za kurithi toka mfumo uliopo Hivyo hata kama tungeletewa mtu muaminifu kiasi gani kutoka ndani ya CCM na hata wakipewa wapinzani nafasi za uwaziri ndani ya Serikali inayoongozwa na CCM bado mambo yataenda hovyohovyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom