Viongozi na mfumo wa kufikiri: Je pinda, makinda na baadhi wa wabunge wapo sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi na mfumo wa kufikiri: Je pinda, makinda na baadhi wa wabunge wapo sahihi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BUBE, Feb 1, 2012.

 1. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwanza nikiri kwamba, huu uzi sijui kama hapa ninapouweka ni pahali sahihi. Lakini kwa kuwa una elements za kiuchumi, nilidhani ni vema kuweka hapa.

  Kwa wiki kadhaa kumekuwepo mjadala kuhusu ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) za wabunge. Kwa sehemu kubwa suala hili limewaleta pamoja wanajamvi hapa (mbali na utani miongoni mwetu....kuwa hata CDM wanashadidia pia wakati walijifanya kupinga).

  Kilichonifanya nianzishe uzi huu, ni 'mfumo wa fikra miongoni mwa viongozi' na hasa sababu zilizotolewa kuhararisha posho na ongozeko kubwa namna hiyo. Kwa kuhitimisha, wale ambao tumesoma gazeti la Habari leo jana, Mh Spika alisema kuwa 'posho ni kidogo. Wabunge wanamatatizo mengi. Wanawananchi ambao wanashida lukuki' Kwa maana nyingine, sehemu ya posho inanufaisha wananchi.
  Hapa ndipo hoja yangu inapokuja!

  Hebu tujiulize. Kabla ya hela kutengwa kwa ajili ya posho ilikuwa ni ya nani? JIBU> Ilikuwa ni fedha ya wananchi
  Je hela anapopewa Mbunge kama posho inakuwa ya nani? JIBU> Inakuwa kuwa ni ya mbunge

  Je ni halali, busara SISI tena kurudi kwa mbunge na kuomba hela hiyo? Mimi nadhani hapo ndipo tunahitaji kuhoji uwezo wa viongozi wetu kufikiri. Ni nani katika dunia hii anaweza kumpatia mtu hela, kisha mtu huyo huyo aliyetoa hela ageuke omba omba na kumwendea yule aliyempatia hela na kumwambia 'tafadhali ninaomba sehemu ya hela niliyokulipa...(sic) unirudishie zinisaidie matatizo binafsi'

  Kwa hiyo, ninadhani, badala ya viongozi kutumia umasikini wetu kama gia ya kutaka kuongeza posho, ni bora wangesema wanahitaji wao hela kwa matatizo binafsi, na wa-justify kwa kusema uchumi wa nchi umekuwa, kwa hiyo keki imekuwa kubwa tunaweza kuongesha 'share' kwa kila mdau! Kwa namna hii, tutafikiria ongezeko la posho kulingana na 'economic and social returns' zinazotokana na michango ya wabunge!
  Naomba kutoa hoja
   
 2. chipanga

  chipanga JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 661
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 60
  Spika alisema gharama za maisha Dodoma zimepanda sana, hivyo ni muhimu waongezewe posho ili waweze kukabiliana na kupanda huko kwa gharama za maisha ya Dodoma. Nauliza kuna sehemu gharama za maisha zimeshuka?
   
Loading...