Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,703
- 4,697
Navitaja vyuo hivi kutokana na maeneo vilipo na kutokana na hali wanayoionyesha ktk maendeleo na hali za wanafunzi.
Tatizo kubwa ni jinsi viongozi wa vyuo hivi wanavyoshindwa kuwapatia malazi bora wanafunzi wao ktk maeneo ya vyuo, badala yake wanaitumia nafasi hiyo kujinufaisha kiuchumi kwa kuwafanya wanafunzi kuwa wapangaji ktk majengo yao ya biashara.
Viongozi hawa wanashindwa kabisa kujenga hostels za wanafunzi na hawaonyeshi dalili za kuhangaika kuweka hostel ndani ya maeneo ya chuo kwa sababu tu wanapenda kuwafanya wanafunzi kuwa wateja ktk nyumba zao binafsi wanazoziita ni hostels. Ni sahihi kuweka vitega uchumi vya aina hiyo lakini siyo sahihi kufanya haya kwa makusudi, kwa kutumia nafasi walizonazo na kuzolotesha maendeleo ya vyuo.
Tabia hii imejengeka vyuo vikuu vya Mzumbe, SUA na Mkwawa. Tafadhalini jengeni hostel za wanafunzi. Wanafunzi wanastahili kuishi maeneo ya kitaaluma na siyo mitaa ya vibaka.