Viongozi mnaudhi sana! Mbolea ya ruzuku inakaeje Dar na hamnaga mashamba huko!?

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,379
Niko pwani, eti nikitaka mbolea ya Ruzuku niifate Dar? Na unatonywa kisiri siri?

Mbolea inakaaje kwenye magodauni ya Dares alam ili hali inapaswa ikatumike Kwa wakulima waliolo Pwani?

Mh msatasfu Rais Kikwete ni mkulima mwenzangu, Je yeye kweli anachukulia mbolea Dar badala ya huku kwetu Pwani?

Mpaka naandika hivi, wakulima waliitwa wakajiandikisha tuu, wakaambiwa mtaitwa, toka kipindi hicho walipoandikishwa mpaka sasa yapita miezi mitatu kasoro, hakuna cha kuitwa wala nini, mbolea huku kwetu haijawahi kushuka, ni 150000+

Siku kapita jamaa na pikipiki lake shambani kwangu nalima, nilivyomtazama nikahisi ni wale wale viongozi upande wa mbolea, Mara naulizwa, vipi mbolea umepata? Nikamwambia, kwani zikekuwa za Siri Siri kupatikana kwake? Tuliambiwa tutaitwa,

Cha ajabu yule jamaa, akaniambia, mbolea unafwata mwenyewe Dar?

Tehe!
Tehe!
Haya mambo ujue ni dharau eeh!

Lambeni asali lakini kuna siku nitamgaragaza mmoja! Maana haiwezekani tuwe tunapotezeana muda, halafu jambo lenyewe halifanyiki!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom