Viongozi mnajisikiaje kuwahadaa Wananchi kwenye bei za bidhaa na huduma mbalimbali?

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,530
3,433
Viongozi mara kadhaa sasa wamekuwa wakiuhadaa Umma juu ya bei za bidhaa na huduma mbalimbali. Leo kila kitu kimepanda bei karibu mara mbili jambo ambalo ni mzigo kwa Mwananchi wa kawaida.

Sukari ilipigiwa kelele lakini bado bei iliyobaki kuwa juu mpaka leo, mafuta ya kupikia ya alizeti tulikuwa tunanunua lita tano kwa shilingi 18,000/= leo ni shilingi 28,000/=

Taarifa ni nguvu leo tunauziana njia za kuweza kupata taarifa kwa bei za kukomoana. Vifurushi "bundle" bei hazieleweki kwa mfano leo mb 900 zinauzwa shilingi 2000/= Khaaa!
 
PM aliyepo hafai kuwepo kwenye hiyo nafas...sjui hata anasimamia nini

Ni matamko ya hovyo hovyo tu...anayoyatoa then anashindwa kuyasimamia
 
Ile meli tuliambiwa ipo bandarini inapakakua mafuta tokea january haijamaliza ?

Isije kuwa ni meli hewa, au wazee wa system wametumia nafasi kujitajirisha zaidi kwa kuuza bei ile ile.

Maana ni juzi tuu nimetoka kununua mafuta ya kupika ikabidi nishangae maana hata wafanyabiashara hawajui ni nn kinaendelea.

Bandari niliiogopa sana tokea kipindi kile serikali ilipookota vichwa vya treni vyenye jina la shirika la reli la Serikali ya Tanzania(TRC).

Yaani ni sawa na mtu kuokota nyumba pamoja na hati yenye majina yake tayari.
 
As the saying goes " show me who control the world and i will tell you who control the value of money"
 
Hali ya uchumi haipo sawa kabisa wanatughilibu akili tu viongozi wetu. Suala sukari leo tukiulizana tunaona wafanyabiashara ndiyo wamehack mfumo huku matamko yakiendelea.

Kwenye mawasiliano kinatakiwa kingine kilichopo kingine kabisa. Hivi wanaposema tutaendelea na vifurushi vile vile ni kweli tulikuwa tunanunua Mb 900 kwa shilingi 2000/=?..
 
Nilinunua mafuta ya kupikia mwezi januari lita kumi kwa shilingi 52,000/=. Jana naenda kununua mengine naambiwa ni 65,000/=. Halafu tunaambiwa JPM alikuwa mtetezi wa wanyonge. Hivi kuna mnyonge anayemudu kununua mafuta ya kupikia kwa bei ya 6500 kwa lita?
 
Labda kuna sababu zilizopelekea mfumuko wa bei na nimeona sio TZ peke yetu,corona inaweza kuwa sababu but siko sure.
 
Labda kuna sababu zilizopelekea mfumuko wa bei na nimeona sio TZ peke yetu,corona inaweza kuwa sababu but siko sure.
Ndiyo maana wanasema Tanzania ni Nchi Tajiri.
bei zinafumuliwa na watu wanagangamala, maisha yanaendelea...tatizo ni wasemaji wetu kusema uongo.
 
Labda kuna sababu zilizopelekea mfumuko wa bei na nimeona sio TZ peke yetu,corona inaweza kuwa sababu but siko sure.
Mkuu mafuta ya alizeti yanakamuliwa hapo Igunga, alizeti inalimwa hapo hapo....tunanunua lita tano sasa hivi kwa shilingi 28000/= Kahama
Dar sijui utakuwa shilingi ngapi?..
Bado Mb tunaambiwa tunaendelea na vifurushi vile kumbe ni kipigo cha hatari kinaendelea.
 
Daah poleni sana,mama ni mchumi mzuri hope ataweka mambo sawa.
Vipi labda kuhusu gharama za uendeshaji?
Am sure wana strong reason na watatupa maelezo.
 
Mkuu mafuta ya alizeti yanakamuliwa hapo Igunga, alizeti inalimwa hapo hapo....tunanunua lita tano sasa hivi kwa shilingi 28000/= Kahama
Dar sijui utakuwa shilingi ngapi?..
Bado Mb tunaambiwa tunaendelea na vifurushi vile kumbe ni kipigo cha hatari kinaendelea.

Vipi huko bei ni nafuu kiasi nini?
Mafuta bei juu,bundle ndio usiseme.
Ukiwa mjanja bora uweke internet home ulipie monthly.
Ni pocket friendly,tafuta kampuni uunganishiwe,siku hizi ziko hadi unatembea nayo we unaconnect wifi tu.
 
Mafuta bei juu,bundle ndio usiseme.
Ukiwa mjanja bora uweke internet home ulipie monthly.
Ni pocket friendly,tafuta kampuni uunganishiwe,siku hizi ziko hadi unatembea nayo we unaconnect wifi tu.
Afadhali tunapeana ushauri wenyewe kuliko kusikiliza matamko yanayotoa matumaini huku uhalisia ukiwa tofauti kabisa na kilichotamkwa.
Shukrani sana Mkuu.
 
Nilinunua mafuta ya kupikia mwezi januari lita kumi kwa shilingi 52,000/=. Jana naenda kununua mengine naambiwa ni 65,000/=. Halafu tunaambiwa JPM alikuwa mtetezi wa wanyonge. Hivi kuna mnyonge anayemudu kununua mafuta ya kupikia kwa bei ya 6500 kwa lita?
Hakuna, watayaacha huko dukani mpaka expire yatupwe.
 
Back
Top Bottom