Viongozi mbali mbali wa nchi na mabalozi wa nchi wakitembelea sehemu zilizowekwa maiti za ajali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi mbali mbali wa nchi na mabalozi wa nchi wakitembelea sehemu zilizowekwa maiti za ajali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 19, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=2]Thursday, July 19, 2012[/h][h=3]Shughuli za Kutambua pamoja na kuzika maiti zilizokosa kutambuliwa[/h]

  [​IMG]

  Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli ya Skagit iliozama hapo jana zikitambuliwa na Ndugu zao na kuruhusiwa Kuzichukuwa kwa ajili ya Kufanya taratibu za mazishi hapo katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
  [​IMG]

  Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Learnhat Alfonso wakatikati akionekana na huzuni Baada ya kuziona Maiti zilizookolewa katika Meli iliozama hapo jana katika Bahari ya Chumbe Zanzibar.Balozi alifika katika Viwanja vya Maisara ili kuona namna shughuli za kushughulikia maiti zinavyoendelea.
  [​IMG]

  Mama alietambulika kwa Jina la Bitatu Uyelo ambae amenusurika na Kupoteza Mtoto wake wa miezi tisa katika Ajali ya Meli ya Skagit iliozama hapo jana katika Bahari ya Chumbe ikitokea Dare es salaam.
  [​IMG]

  Waziri wa Mamboya ndani wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Emanuel Nchimbi alifikakatika Eneo lililohifadhiwa Maiti wa Ajali ya Meli ya Skagit ili kutambuliwa na Ndugu zao na Kupata maelezo kwa Daktari Kiongozi hayupo pichani Hapo katika Viwanja Vya Maisara Zanzibar.
  [​IMG]

  [​IMG]

  Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio.
  [​IMG]

  ~Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio.
  [​IMG]

  Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio.

  Picha na Yussuf Simai, Maelezo

  Imewekwa na MAPARA at 8:48 PM 0 Maoni [​IMG] Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook


  Links to this post

  [h=3]DK Bilal afariji Wafiwa na Wahanga wa ajali ya meli[/h]

  [​IMG]

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Khamis Haji Khamis, jinsi ulivyandaliwa utaratibu wa kuwahifadhi marehemu watakaokosa kutambuliwa na ndugu zao, wakati Makamu alipofika kwenye Viwanja vya Maisara mjini Zanzibar, leo Julai 19, 2012, kuangalia shughuli za uokoaji na utambuzi wa marehemu. Kushoto ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
  [​IMG]

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skiget, Kitwana Makame Ali (24) mkazi wa Unguja, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Kulia ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
  [​IMG]

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mgonjwa aliyenusulika katika ajali ya Meli ya Skagit, Hamisa Akida (45)mkazi wa Ununio mjini Bagamoyo, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


  Imewekwa na MAPARA at 8:37 PM 0 Maoni [​IMG] Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook


  Links to this post

  [h=3]Rais Kikwete Atua Zanzibar Kufariji Waliopatwa na Maafa[/h]

  [​IMG]

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja leo July 19, 2012.
  [​IMG]

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali leo July 19, 2012.


  [​IMG]
  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, wakipata maelezo kutoka kwa daktari wa jeshi la Polisi anaeshughulikia vinasaba (DNA), Dk. Ahmed Makata, alipofika katika eneo la kuhifadhia maiti wa ajali ya kuzama meli ya MV.Skagit, kwenye viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar jana.
  [​IMG]

  Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana Bw Kitwana Makama Haji ambaye kalazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja leo July 19, 2012
  [​IMG]

  Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bi Salome Abeli, mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo ya meli. Yeye ni mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission akitokea Arusha kwenda Pemba Kikazi leo July 19, 2012.
  [​IMG]

  [​IMG]
  PICHA NA IKULU
  [​IMG]  Imewekwa na MAPARA at 7:57 P
   
 2. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu kwa picha. Poleni sana wafiwa. R.I.P. marehemu wote.
   
 3. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Mtoa taarifa na picha ana mkanganyiko wa Kiswahili. Maiti hazikuokolewa bali zimeopolewa. Waliookolewa ni wale waliotolewa majini wakiwa wazima. Poleni Wafiwa na manusura.
   
Loading...