Viongozi Maziwa Makuu ya Afrika wakutana Kampala

mdau wetu

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
548
58
Viongozi 10 wa nchi za eneo la Maziwa Makuu ya Afrika wanakutana leo mjini Kampala Uganda kwa shabaha ya kuujadili kwa kina mgogoro unaoendelea kutokota huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Henry Oryem Okello Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya kimataifa wa Uganda amesema kuwa, kikao hicho kitajikita zaidi kutafuta njia za kuutatua mgogoro huo unaoendelea kuumiza vichwa vya viongozi hao wa Kiafrika na jumuiya za kimataifa. Waziri Henry Oryem Okello ameongeza kuwa, kikao cha wakuu hao wa nchi za eneo watajadili mpango wa kutumwa kikosi cha wanajeshi elfu nne huko mashariki mwa Kongo kwa lengo la kupambana na waasi wa M23. Uganda ikiwa ni mwenyekiti wa mzunguko wa nchi 11 wanachama wa eneo la Maziwa Makuu ya bara la Afrika, hivi karibuni ilikuwa mwenyeji wa Marais wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma, makao makuu ya jimbo la Kivu Kaskazini.
 
Back
Top Bottom