Wadau imejiri kwamba serikali inawabana watu wasiwazomee mafisadi na wakulu wa matawi ya juu wameshatangaza kula sahani moja na wanaozomea mafisadi.
Hizi ni dalili za kidikteta na zisipokemewa na kulaaniwa mapema zinaweza kuwa na mwisho mbaya kwa mafisadi kudhani wanaweza kufanya chochote na hakuna atayewabughudhi.
Viongozi waache undumi la kuwili kwa kufurahia na kukenua meno pale wanaposhangliwa kwa kupigiwa makofi lakini hawapo tayari kuzomewa wanapoboronga haswa kwa mambo yaliyo wazi hata kwa mtoto mchanga (Mgodi wa Kiwira ni mfano hai).
Kwa kuwa hakuna mtu aliyetukana au kushambulia mwili, kuzomea hakuvunji sheria na wananchi waachiwe huru kuelezea hisia zao ili mradi sheria za nchi hazivunjwi.
Viongozi wanaozomewa inapaswa wajiulize; mbona mzee Mwinyi, Kawawa na hayati Mwl. Nyerere, na viongozi wengine waadilifu waliopita hawakupata kuzomewa, na jibu liko wazi wazee wale hawakuwa mafisadi, walikuwa na makosa yao ya kibinadamu na kiutendaji lkni si ufisadii. Na kwa hivyo basi ili uepuke kuzomewa simamieni uadilifu na epukeni ufisadi.
Miungu ibariki Tanzania na utuepushe na mafisadi na vitimbi vyao