Viongozi kuweni waangalifu na kauli na matendo yenu

ndoto2020

JF-Expert Member
Feb 25, 2017
226
352
Wanabodi , Bila kujali itikadi zetu za siasa kwa mwendelezo wa matamko na matendo ya baadhi ya viongozi napenda kuwapa ushauri na kuwakumbusha kidogo baadhi ya wenzao ambao walikuwa na kauli nzito nzito na majivuno balaa lakini kibao kimegeuka wamekuwa wapole na wanyonge balaaa bila kutegemea yanaweza kutokea

1. Waziri mkuu mmoja aliwahi kutamka hadharani ukitaka kufanikiwa biashara au mambo yako yakunyookee kuwa CCM - Leo mpinzani tena mwenye hasira na uchungu kweli kweli kwa matamshi yake anavyoyatoa - siku hizi mnamkubali ana logical criticism.
2. Waziri mmoja wa fedha awamu ya tatu - alikuwa mbabe kweli kweli AKA tutanunua ndege ya raisi hata mkila nyasi- baada ya muda nikasikia yupo gerezani - mara sinza kufanya usafi sasa huru
sikuwahi kutegemea wala kufikiri.
3. Waziri mmoja wa sheria - alimtunishia mfanyabiashara mmoja misuli balaa sasa hivi mpole na kimya sana .
4. Mkuu wa mkoa mmoja morogoro awamu ya tatu alikuwa maarufu kweli kweli kama maarufu wa sasa , baada ya awamu ya nne tu kuingia - du alitia huruma sana hasa hasa miaka ya 2012-13 kabla sijaondoka Tanzania sasahivi sijui anaendeleaje.
5. IGP mmoja mr Ngunguri - Huyu naye alikuwa mtemi kweli kweli lakini awamu ya nne kuingia naye alitulia sana , nadhani pia kiuchumi aliyumba kidogo na alitaka ubunge morogoro mjini lakini Abood kajikita vizuri kwa wananchi sio wa kutolewa leo labda 2025

USHAURI KWA WALIO MADARAKANI tendeni kwa hekima na busara bila visasi kwa wenzenu kwa sababu kuna siku unaweza kujikuta na wewe ni kundi lile lile mtakaolia na kulalamika mnanyanyaswa kipindi hicho 2025 sio mbali , usije kukumbukwa kwa mabaya tu

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom