Viongozi kujifanya wanalipia gharama za matibabu kwa mgonjwa mmoja badala yakujikita kuweka misingi imara ya huduma ya afya ni HADAA

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
787
755
Hii naweza kuiita HADAA za kisiasa.
Hii ni HADAA haswa kwa wananchi tuliowachagua.

Viongozi wamekuwa na tabia hii ya kujifanya ni watu wema sana kuchagua baadhi ya wagonjwa na kulipia gharama za matibabu au kuhakikisha wanasaidiwa katika hospitali zetu za rufaa. Inasikitisha kwa sababu unakuta huyo mgonjwa mmoja anachaguliwa baada ya kupata kiki za kwenye media huko.
Ila UKWELI unabaki kuwa kusaidia mmoja sio kazi za wanasiasa badala yake wao wangejikita kuunda mifumo na sera thabiti ili kila mtu afaidike na hizi huduma kuliko kujifanya wema kwa kusaidia mgonjwa mmoja na kuacha wengine laki moja wakifa huku wakitaka tuendelee kupiga VIGELEGELE kwa "utu wema wao".

WanaForums tukemee kwa nguvu hizi tabia za viongozi kuhadaa wananchi ili waonekane wema huku wakiacha sera zao na mipango yao mibovu ikiua watu wengine. Huwezi kusikia wakikemea haya mambo. Huwezi kusikia wataboresha vipi sera ya bima lakini watakuwa wa kwanza kujifanya wema sana kusaidia wagonjwa huku wakiita vyombo vya habari vyote vianike "wema wao"
 
Back
Top Bottom