Viongozi Karatu ‘waitunishia misuli’ Kamati Kuu Chadema

KIBE

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
943
184
Mgogoro ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha umechukua sura mpya baada ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji Wilaya hiyo kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kwa maelezo kwamba, haina mamlaka hayo.

Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Karatu, Thomas Moshi Darabe, alisema kupitia taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana kuwa wamesikitishwa na uamuzi wa Kamati Kuu wa kuisimamisha kamati hiyo yenye wajumbe 17 bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza.

Alisema uamuzi huo wa Kamati Kuu unakiuka katiba ya CHADEMA ibara ya 6.5.6 na ibara 7.4.7 (g) inayoeleza kuwa kikatiba chombo chenye mamlaka ya kusimamisha/kuondoa Kamati ya Utendaji ya Wilaya ni Mkutano Mkuu wa chama wilaya.

Darabe alisema kwa burasa ya kawaida hata kama kulikuwa na sababu za kufanya hivyo, wangepewa hati ya kuitwa na kwamba, kwa maelezo hayo kamati ya utendaji ya chama wilayani humo iko kazini itaendelea na shughuli zake za kila siku.

Alisema awali, Kamati ya Utendaji Wilaya ya Karatu, ndiyo ilikuwa inawatuhumu baadhi ya viongozi kwa kudhoofisha chama na kushauri wachukuliwe hatua, lakini wakashangaa wanasimamishwa wao uongozi.

Darabe alisema kutokana na uamuzi uliofikiwa na Kamati Kuu, Kamati ya Utendaji ya Wilaya, madiwani wa CHADEMA na wadau wa chama hicho watafanya mkutano kuanzia kesho na keshokutwa.

Alisema mkutano huo utafuatiwa na mkutano wa hadhara wa wananchi utakaofanyika Jumamosi wiki hii, Karatu, ambao utahudhuriwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.

Mapema katika mkutano wake wa siku mbili mfululizo, uliohitimishwa Desemba 16, mwaka huu, Kamati Kuu ya CHADEMA ilifikia uamuzi wa kusimamisha uongozi wa chama hicho wilaya hiyo, baada ya kubaini kasoro za utendaji wa viongozi wake.( SOURCE NIPASHE DEC 27.
 
haka kautaratibu walikokaanzisha chadema ka kutunishiana misuli katawatafuna kama mchwa anavyokula mbao.wanatakiwa wawe wanatumia busara zaidi kuliko kupelekana kibabe.
 
haka kautaratibu walikokaanzisha chadema ka kutunishiana misuli katawatafuna kama mchwa anavyokula mbao.wanatakiwa wawe wanatumia busara zaidi kuliko kupelekana kibabe.

Mkuu nakuunga mkono kwa asilimia 100 na mimi nimefikia hatua ya kutokuwa na imani sasa na hivi vyama vya upinzani ambavyo nilidhani vinaweza kuleta mapinduzi ya uongozi katika nchi hii,na vyenyewe vimeiga ujinga ulioko ndani ya CCM vimekua ni vyama vya malumbanio kila siku badala y kuketi na kujipanga namn ya kukiimrisha chama,ni ukweli usipingika kwamba kuna baadhi pia ya wafuasi,wanachama ama viongozi wa CHADEMA ambao mimi binafsi naona wanahusika moja kwa moja tena kwa kudhamiri katika kukihujumu chama ili kionekane hakifi mbele ya jamii,kwa mfano hata humu kuna wafuasi mbao wanashbikia hata mambo ya kipuuzi yanayofanywa na baadhi ya viongozi wa chama badala ya kukemea.

Hata CCM nao walianza hivi hivi na ndiyo mana leo kinaonekana kinnuka mbele ya jamii.
 
Lumumba propaganda fm at work.

Inaonekana wewe ni kipofu na huoni,kwa sababu badla y kuangalia ukweli ulipo na utoe ushauri namna ya kutatua tatizo unasingizia mpinzani wako,shauri yako kalia hayo tu mwisho wake utauona.
 
Naona lumumba imeamka

Endelea tu kusema hivyo wakati nyumba inaendele kuungua,bdla ya kuangalia namna ya kuzima moto we unabaki kulumbana na aliyewasha moto,itkula kwako endelea na hayo mawazo mgando.
 
Freeman Mbowe nadhani anaingia kwenye orodha ya wanamkakati mahiri kabisa, hapa anaangusha mti kuanzia kwenye mzizi. Zitto una mengi ya kujifunza kutoka kwa huyu jamaa.
 
Last edited by a moderator:
endelea tu kusema hivyo wakati nyumba inaendele kuungua,bdla ya kuangalia namna ya kuzima moto we unabaki kulumbana na aliyewasha moto,itkula kwako endelea na hayo mawazo mgando.

ukweli hapo mimi huwa nachoka na wapenzi na viongozi wa chadema...jambo ambalo linakuwa si zuri kwao wao wanasema ni uongo tu uzushi wa lumumba.... Haya ila ndo ukweli huo kuwa nyumba inaungu vyema ukapokea ushauri
 
wakijing'ang'ania madaraka watafukuzwa kwenye chama kwa kunyang'anywa kadi kama madiwani wa arusha na mwanza
 
[h=1]Mbowe ziarani wilayani Karatu( MWANANCHI DEC 27)... MBOWE KAONA KUNA TATIZO LAKINI WENGINE WANAONA NI UZUSHI WA LUMUMBA[/h]
 
Alisema awali, Kamati ya Utendaji Wilaya ya Karatu, ndiyo ilikuwa inawatuhumu baadhi ya viongozi kwa kudhoofisha chama na kushauri wachukuliwe hatua, lakini wakashangaa wanasimamishwa wao uongozi.

toka mwanzo nilimwamini TUNTEMEKE
 
Last edited by a moderator:
Bado tatizo liko kwa viongozi wa cdm..na hasa dr.slaa ndio chanzo ya yote mana ufisadi w amradi karatu unamlenga yeye sasa wanaomtuhuma anataka wafukuza mapema ..ngoma nzito jamaa wamegoma teh teh
 
Back
Top Bottom