Viongozi hawa wawajibishwe ili kuleta taswira nzuri katika taifa letu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi hawa wawajibishwe ili kuleta taswira nzuri katika taifa letu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kilongayena, May 17, 2011.

 1. K

  Kilongayena Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Habari wana JF,[/FONT]
  Naandika habari hii kwa masikitiko makubwa, Nina mashaka na ubunifu na uelewa wa baadhi ya viongozi katika nchi yetu hasa kwenye masuala ambayo yanaonyesha taswira ya Taifa letu . Naandika hivi kwa sababu nimeshuhudia kitu cha ajabu mno jumamosi ya Tarehe 14/05/2011 pale uwanja wa taifa wakati Timu yetu ya Taifa(Taifa Stars) ikicheza na Timu ya Taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) na ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia uwanja ule.
  [FONT=&quot]Kiingilio kilikuwa Tshs 5,000 na Tshs 10,000 kwa VIP, Binafsi nilikata tiketi ya Tshs 5,000 lakini ni kashangaa napewa tiketi mbili moja inaonyesha mechi ya Taifa Stars na New Zealand ikionyeshwa inachezwa tarehe 3/06/2009 saa 7:00 P.M na nyingine Taifa Stars na Bafana Bafana inachezwa tarehe 14/05/2011 saa 18h00 (6:00 P:M) ilinichanganya sana hii kitu,kumuuliza mmoja wa wakatisha anadai eti tiketi za mechi ya siku hiyo hazina seat no ndo wametoa hii ya pili kwa ajili ya kupata seat nikajaribu kuhoji zaidi akawa mkali eti shida yako nini niende kuuliza mlangoni kwa kuingilia nitapata maelezo zaidi.[/FONT]
  [FONT=&quot]Baada ya kuingia ndani nilikuta mechi imeshaanza,hivyo nilikuwa busy kuangalia mpira . mpaka kipindi cha kwanza Timu zote zikuwa suluhu 0 -0, wakati timu zimekwenda kupumzika nikawa natafakari na kumtafuta kiongozi yeyote wa TFF au Wizara husika niweze kupata majibu juu ya niliyoyakuta kabla ya kuingia uwanjani. Kulikuwa na matangazo ya Cocacola na NMB tu yalikuwa yanaonyeshwa kwenye Screen iliyopo uwanjani pale, Uwekaji wa matangazo yale ulionyesha wazi walikuwa wanatumia CD, ilikuwa ikioneka dhahiri hata mtoto mdogo angetambua lile kwani background ya DVD player ilikuwa inaonekana moja kwa moja. Kabla sijafanikiwa kuonana viongozi hao mara CD iliyokuwa na Tangazo la NMB (alikuwa Lady Jay Dee Yule na tangazo NMB Mobile Pesa fasta) ikasimama (ikastack) ikatolewa CD ile na kuwekwa ya tangazo la Coca cola yote haya yalikuwa yanaonekana kwani background ya DVD player ilikuwa inaonekana dhahiri yaani uswahili mtupu, na baadae screen ikawa kimya kabisa mpaka wachezaji wanaingia uwanjani lakini yakawekwa matangazo yale yale tena kabla ya kuanza kuonyeshwa mpira kipindi cha pili.[/FONT]
  [FONT=&quot]Tanzania tuna vitu vingi vya kutangaza ili wenzetu waliopo nje wajue nini tunacho, Screen ile imekaa takribani dakika 10 bila kuonyeshwa kitu chochote wakati wa mapumziko, Tuna mbuga za wanyama na vivutio vingi ambavyo ilipaswa vionyeshwe mle ndani tuweze kupata watalii wengi zaidi. Hata hili jamani mpaka twende semina elekezi jamani,hebu oneni aibu viongozi wetu.[/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa kweli wana JF nilijikuta naona aibu sana siku ile kwani pembeni yangu kulikuwa na raia wa Denmark nao walikuja kutuunga mkono pamoja na familia zao, nikabaki nawaza hivi uongozi wa uwanja unafanya nini, TFF ipo wapi na Wizara wanasimamia nini jamani? ,Tunashindwa kuweka mfumo wa computer kuendesha uwanja ule kitu ambacho gharama yake haifiki hata 12 milioni, ni kununua computer moja au mbili na programu za kuchezea video tu,kinachofuata ni kucopy matangazo husika kuweka kwenye computer na kutangazwa kupitia mle. Viongozi mliopewa dhamana kwenye michezo hebu liangalieni hili.[/FONT]
  [FONT=&quot]Nawasilisha wana JF.[/FONT]
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nadhani wameshindwa kuvua gamba kilichobaki ni kuwachuna ngozi kabisa.
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu kilongayena upo sahihi kabisa, hii nchi kwasasa haina uongozi subiri utoe hayo mawazo tukipata Tume huru ya uchaguzi. hivi unategemea nani atamuajibisha mwenzake kwasasa? kama Rais wa nchi mwenyewe hajui uwezo wa watu aliowateu mpaka anauliza kama kuna mtu hawezi kazi aondoke
   
 4. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,053
  Likes Received: 3,083
  Trophy Points: 280
  Huwa wanashindwa hata kuonesha ukanda wa timu,magoli na dakika za mchezo wakati mechi ikiwa live kwenye Tv,mtu unaangalia Tv hujuhi ni dakika ya ngapi,hawajuhi matangazo yakae wapi,utashangaa mara tangazo liko juu,mara limeshushwa chini,yaaani hovyo hovyo,unajiuliza hivi tatzo ni nn hasa,mbona watanzania wengi wamesoma programing,ya nini kuweka wajomba,mashemeji wasiokuwa na shule
   
Loading...