Viongozi gani wapo miongoni mwenu?

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
NI VIONGOZI GANI WAPO MIONGONI MWENU

Nachukua nafasi hii muhimu kuwakumbusha na kuwatahadharisha wananchi juu ya viongozi wanaotaka kugombea nafasi tofauti za uwakilishi kupitia uchaguzi mkuu uchaguzi wa mwaka 2015 iwe kiti cha Urais, Ubunge ama Udiwani kwa sifa na ahadi zilizopambwa kila tunu za uzalendo na uwajibikaji.

Ikumbukwe tu kwamba tunaingia ktk wakati mgumu sana wa kisiasa, wakati ambao Watanzania wengi wameburuzwa ktk kuipokea katiba ilopendekezwa na wapishi wa keki hiyo na sasa wanataka kuila wenyewe maana mwongozo ni ule ule ulotufikisha hapa tulipo isipokuwa wametenganisha vizuri sahani zao katika ugawanaji wa keki ya Taifa chini ya sheria zile zile zilizotuletea Makabaila na mabwanyeye. Tusidanganyike na sauti za majukwaani maana hata wakoloni walikupoja na biblia/Quran wakatuambia tufumbe macho tusali, tulipofumbua tukakuta wameisha chukua ardhi, sisi tumebakia na dini ambayo leo hii ndio kilema chetu kikubwa. Hata pale Mwenyezi Mungu anapotaka sisi tufanye maamuzi magumu basi bado humsubiri Mungu achukue yeye jukumu hilo. Tusikubali kununuliwa kwa T-shirt na khanga kama mababu zetu waloingizwa utumwani kwa kupewa shanga na njuga wakatukuzwa kwa ngoma!.

Ni muhimu sana kwa wananchi kufahamu hili sio swala la upande gani ama nani anaweza kusimamisha Uzalendo na uwajibikaji kwa raia wake bali kwa ujumla wetu ni mwongozo gani utakao tafsiri na kusimamisha UTU kuwa sheria mama na utawala bora. Pasipo mwongozo bora unaotambua UTU wetu na kuamrisha kila mtu awe mzalendo, muadilifu, mwajibikaji, muwazi na kutambua usawa basi sio rahisi watu wananchi wake wazawa na wageni wakauthamini UTU kwa kutumia hisia zao za kibinadamu kwani kila binadamu ameumbwa na Unyama ndani yake na sheria pekee ndio huutengua unyama huo kwa kusisitiza UTU.

Mwaka huu 2015, watakuja wagombea uongozi ambao sio baina yenu na kudai wanaelewa mahitaji yenu, wanaelewa adha zenu na watajitambulisha kuwa baina yetu kama tunavyoomba misaada nchi za nje. Hizo benki Kuu za dunia na vyombo vya misaada kama IMF ni walaghai sawa sawa na wagombea uongozi ambao wataonyesha uchungu juu ya shida na umaskini wetu lakini ukweli ni kwamba hawa sii baadhi yetu hawajui machungu hayo, hawa ni wafanya biashara ambao hutukuza mfumo wa kiuchumi unaopambanisha mahitaji (demand) na upatikanaji (supply) hivyo wanaweza kuyaunda mahitaji pale wanapokwama na bidhaa zisokuwa na soko. Tukumbuke tu hawa wanawajibika kwa benki kuu na IMF ifanye biashara ya faida na sio kwetu sisi ni mateja wao.

Vivyo hivyo wagombea uongozi ambao sii baadhi yetu watatumia kila hila kuudanganya umma kwamba wao watayaleta maendeleo na kubadilisha maisha yetu ilihali wao ni watumishi wa kundi la Walalahai walowaweka pale ili kusimamia, kutetea na kulinda mali na nafasi zao kwa sababu sii miongoni mwenu WAKULIMA na WAFANYAKAZI. Chama cha Mapinduzi kimeshindwa kutuongoza na sii swala la Kikwete, Pinda, Makamba ama Lowassa bali tukumbushane mambo haya muhimu sana.

1.Chama hiki kina sera gani, uongozi wake wana matumaini gani dhidi ya makundi gani ya kiuchumi na wamefanikisha yapi, tukumbuke tu kwamba itikadi ni ufunuo fasihi wa mapambano dhidi ya falsafa pinzani, aidha kutofautiana ktk walengwa au misingi yake ya utekelezaji kiuchumi na kijamii.

2. Chama hiki kinajinasibisha na kundi gani, ni kina nani walengwa wa mipango yao ya maendeleo.
Nakumbuka zamani enzi za mwalimu CCM kilikuwa chama cha Kijamaa kikipambana dhidi ya Ubepari na walijenga sera zake dhidi ya Ubepari, na maadui wakubwa wakatajwa kuwa ni Ujinga, umaskini na maradhi tofauti kabisa na wachumi unaotazama fedha kama msingi wa maendeleo. Je, leo hii CCM wana sera zipi? Ni falsafa gani hasa wasokubaliana nayo na wanapambana nayo vipi kisiasa ili kuhakikisha wanajenga Taifa la watu gani!

Pili, CCM ilikuwa chama cha Wakulima na Wafanyakazi na kweli kilihakikisha wakulima na wafanyakazi wanapewa nafasi ya kwanza kuondokana na umaskini japo serikali ilikuwa na uwezo mdogo sana. Leo hii viongozi wa CCM badala ya kuwahudumia wakulima na wafugaji basi wao ndio wamekuwa vinara wa kuchukua ardhi kubwa ili wawe wakulima na wafugaji na ukiwauliza wanasema maslahi binafsi kwanza sio dhambi.Tunashuhudia yale yale ya mkoloni aloiba ardhi yetu kwa watawala wanaojinasibisha nasi kwa rangi na uafrika!

Pasipo kuelewa undani wa mwelekeo wa chama ni kazi bure kumchagua kiongozi atoke baina yetu kutokana na ahadi zake ama sura yake maana naamini kwa dhati ya kwamba viongozi wengi watarajiwa sii baina yetu. Ni wagopmbea wachache sana wanaoweza kujinasibisha na WAKULIMA ama WAFANYAKAZI zaidi ya kuwa watumishi wa Umma walobebwa kushika madaraka nafasi za juu za utumishi wa umma kupitia migongo ya wazazi wao ama marafiki zao. Wagombea wengi wametoka ktk kundi hilo hilo la watawala walokuzwa na utumishi wa kitawala kututawala na hivyo wanaendeleza utawala!

Nawaomba sana wananchi wachunguzeni kwa makini watu hawa mtajua kina nani walikuwa nanyi na kina nani walikuwa upande wa pili japo waliweza na wanaweza kulitumia jukwaa vizuri kujinasibisha nanyi maana siku hizi katika siasa zetu imekuwa sawa na msafara wa Mamba, hata kenge wamo. Kila mmtu anataka kuwa mwanasiasa kwa sababu huko mto Mara kuna Ulaji..Tuwachunguze wagombea.

Nitauliza swali naji jiulizeni wenyewe kuhusu viongozi wagombea wa Urais walokwisha jitokeza ama webnye nia ya kugombea. Nani kati yao anajinasibisha kama yeye ni kutoka kundi la Wakulima na Wafanyakazi? Kiongozi Zitto Kabwe ambaye hatogombea uchaguzi huu ndiye pekee nayeweza kumuweka ktk kundi la viongozi wazalendo walojifunza kutokana na kundi la Walalahoi (wakulima na Wafanyakazi). Nasema ndiye pekee kutokana na safari zake kutembelea wakulima wa korosho huko Mtwara, wakulima wa katani huko Tanga, pamba mikoani Mwanza, shinyanga na kahawa huko Kigoma na Bukoba! Ukiacha mbali ofisi za wafanyakazi ktk migodi ya dhahabu, gas, mashirika ya umma na binafsi na kadhalika. Nyie wengine mmekwenda wapi kushirikiana na wananchi zaidi ya majukwaani kukitangaza chama na ushindi wenu! Uko wapi ushindi wa wananchi dhidi ya wadhalimu mabwanyeye mnaowatumikia!

Nawaomba sana viongozi wa UKAWA pamoja na kwamba mimi binafsi sikukubaliana nao katika hatua zao za kudai katiba mpya - wajipange vizuri safariu hii maana hawakunisikiliza wakati ule na wamevuna yale yale nilowatahadharisha wakanipuuza!. Waache tamaa za madaraka na wafanye ushirikiano wa nguvu bila kubaguana kutokana na kutoaminiana kwa sababu kamwe Watanzania hawawezi kuaminiana kutokana na sisi wenyewe kupoteza tamaduni zetu, kutokuwa na mwongozo zaidi ya ubinafsi kutokana na umaskini. na wakumbuke kuwa hata ndani ya vyama vuyao wapo watu wachumia tumbo walojipachika kaa kenge ndani ya kundi la Mamba iwe Chadema, CUF au NSSR.

UKAWA kuweni wawazi na sio kuhodhi nyadhifa za UKAWA ilihali UKAWA sio chama bali coalition ya vyama na watu. Wakaribisheni watu wote wa makundi ya kijamii wtakaotaka kujiunga nanyi ama wagombea binafsi ambao wana nia ya kuleta mageuzi ya kweli. Na hakika katika msafara wa Mamba kenge watakuwemo lakini itakapo fika wakati wa ushindi tukasimamisha MIIKO na MAADILI ya Uongozi, tukaandika katiba yenye kuuthamini UTU kama msingi wa Utanzania wetu kwa kuthamini mila, desturi na tamaduni zetu basi bila shaka hao Kenge watajitenga kama mafuta na maji.

UKAWA iwaalike na kuwakaribisha wapambanaji wa kweli kama Zitto Kabwe, Mzee Warioba na kundi zima la Nyerere Foundation, vyama vya Upinzani vyote, viongozi wa kambi za #ChangeTanzania (Maria Sarungi) na kadhalika kwa sababu nafasi hii haitatokea tena kama tutaipoteza leo. Na wala msifikiri kwamba pekee mtaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015, hapana CCM wana mbinu nyingi sana na baina yenu watapata penyo za kuwasambaratisha na wakishindwa kabisa watanunua ushindi. Katiba bado ipo upande wao na hakika nguvu kubwa ya ziada inatakiwa katika majukwaa bara na visiwani.

Ni Usia wangu wa mwaka 2015. na nawatakieni Kheri ya mwaka mpya wana JF wote popote mlipo. Mapambano yanaendelea
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,123
2,000
Confucius said "The strength of a nation derives from the integrity of the home."

Hatuwezi kuwa na uongozi bora wa nchi kama umma wa Watanzania haujaweza kujikita katika uthabiti wa maadili.

Viongozi wanatoka miongoni mwa umma. Umma ukijikita katika uhakiki wa uongozi kama alivyosema Mkandara , hata wahuni wanaotaka kudandia uongozi hawataweza.

Hili linataka elimu na kuwa macho mara zote.

Maana siku hizi kuna viongozi (wanaoongoza) na vitongozi (wanaotongoza kupata kula).

Ninafarijika kuona watu wanalizungumzia sana hili. Juzi nimeona Youtiube video ya mtu anaitwa Humphrey Polepole alikuwa anazungumzia hili katika moja ya vipindi vya mahojiano kwenye televisheni.
 
Last edited by a moderator:

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Confucius said "The strength of a nation derives from the integrity of the home."

Hatuwezi kuwa na uongozi bora wa nchi kama umma wa Watanzania haujaweza kujikita katika uthabiti wa maadili.

Viongozi wanatoka miongoni mwa umma. Umma ukijikita katika uhakiki wa uongozi kama alivyosema Mkandara , hata wahuni wanaotaka kudandia uongozi hawataweza.

Hili linataka elimu na kuwa macho mara zote.

Maana siku hizi kuna viongozi (wanaoongoza) na vitongozi (wanaotongoza kupata kula).

Ninafarijika kuona watu wanalizungumzia sana hili. Juzi nimeona Youtiube video ya mtu anaitwa Humphrey Polepole alikuwa anazungumzia hili katika moja ya vipindi vya mahojiano kwenye televisheni.
Mkuu kama ulikuwepo akilini mwangu kwa sababu nmetoka home hivi majuzi tu na kusema kweli tumeacha UTU wetu kiasi kwamba hata kusalimiana barabarani imekuwa kama - Nakujua?

Inasikitisha sana kuona kwamba kazi ama ajira sio dhamana bali ni matunda ya elimu ama nguvu kubwa ilotumiwa na mwenye cheo, hivyo hawajibiki kwa mtu. Na kibaya zaidi ni kwamba tumetoka katika Ubepari na kuunda mfumo wetu wenyewe uitwao "Mwenye njaa wewe!".. maana ukienda dukani unaomba kununua kitu mwenye duka ana haki ya kutokuuzia, ana haki ya kutaa hela yako na kadhalika. Nenda katika ofisi za huduma za serikali unaomba kupewa hata TIN number japo ni kitambulisho cha kulipia kodi inayomlipa yeye mshahara. Kujiandikisha kupiga kura, kuomba liseni na kadhalika yote unanyenyekea kupewa kama sii kutoa hongo (rushwa)

Hata tukipata kiongozi wa aina gani pasipo kubadilisha mfumo na haswa mwongozo unaolazimisha uwajibikaji, uadilifu na uwazi sidhani kama jamii hii iko tayari kubadilika wenyewe, na tunakoenda ni kubaya zaidi kwa sababu vitu vya nje ndivyo vinashamiri kibiashara wakati vitu vinavyotengenezwa nyumbani havina soko. Nikuchekeshe kitu, Unajua hivi sasa huduma bora utaipata wapi? kwa machinga na wauza mboga masokoni. Hawa wachuuzi hawana elimu wala tabia za kipebari lakini ni washawishi wazuri sana na usipokuwa makini utauziwa mbuzi ktk gunia. Na wasomi wetu ndio mateja wa mali za machinga!

Nilipoenda sokoni Kariakoo niliambiwa kuna Spinarch nikasema waniletee nikaletewa mboga nyingine kabisa! Nikawaambia hiyo sio Spinarch sikuaminiwa na imeendelea kuitwa spinarch hadi kesho na watu wanaipenda spinarch hiyo feki feki sijui sukuma wiki - collard green.
Hii ndio tanzania yangu!

Viongozi vitongozi ni sawa na wauza mboga kariakoo wapo radhi kuuzia kitu sicho ili mradi wao wamepata kuuza bidhaa zao!
Ni ajabu sana leo hii watu wanajitangaza kugombea Urais lakini hata siku nmoja hawajawahi kutembelea miradi ya wananchi ktk kilimo, ufugaji wala ofisi za ajira kusikiliza madai ya wananchi japo wao wanapkea mabillioni toka kodi za hao hao wanaowatawala. Sasa ikiwa mwananchi hana ajira wala mshahara mzuri hiyo kodi inayotokana na asilimia ya pato la mtu itaongezeka vipi kupandisha mishahara yao wenyewe?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom