Viongozi CWT wasimamishwa kwa makosa ya uhujumu uchumi

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,005
1,583
Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT), limewasimamisha uongozi Katibu Mkuu wa chama hicho, Deus Seif na mweka hazina, Abubakar Allawi baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kutiwa hatiani kwa kosa la uhujumu uchumi na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kaimu Rais wa CWT, Dinah Mathamani ameyasema hayo leo Jumamosi Septemba 17, 2022 wakati akizungumzia uamuzi wa baraza hilo lililokutana kwa dharura kuanzia Septemba 15,2022 hadi Septemba 17,2022.

"Baada ya Baraza la Taifa kupokea taarifa na kujadili wajumbe waliazimia kuwasimamisha Mwalimu Deus Seif na Abubakar Allawi katika nafasi zao za uongozi na utendaji ndani ya chama cha Walimu Tanzania wakisubiri maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Taifa," amesema.

Amesema viongozi hao wamesimamishwa na baraza hilo katika kikao chake cha jana, kwa kipindi chote ambacho wamesimamishwa hawatahusika na shughuli zozote zinazohusiana na CWT.

Juni 28, 2022 Seif na Allawi walihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi, Dar es Salaam kifungo cha miezi sita jela pamoja na kurejesha fedha za CWT Sh13.9 milioni baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na uchepushaji wa fedha hizo.

Chanzo: Mwananchi
 
Hawakuona aibu kuibia waalim ambao kila siku wanapambana kujikwamua kimaisha.

Hizi ajira za kuwa waangalifu sana, hali siyo
 
Hela za walimu huwa ni za kupiga tu,
Hao wamepiga kdg ,waoga, halafu hawakuwa makini,
 
Mkutano mkuu uwafukuze kabisa na uwachunguze kwa miaka yote waliokua viongozi
 
Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT), limewasimamisha uongozi Katibu Mkuu wa chama hicho, Deus Seif na mweka hazina, Abubakar Allawi baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kutiwa hatiani kwa kosa la uhujumu uchumi na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kaimu Rais wa CWT, Dinah Mathamani ameyasema hayo leo Jumamosi Septemba 17, 2022 wakati akizungumzia uamuzi wa baraza hilo lililokutana kwa dharura kuanzia Septemba 15,2022 hadi Septemba 17,2022.

"Baada ya Baraza la Taifa kupokea taarifa na kujadili wajumbe waliazimia kuwasimamisha Mwalimu Deus Seif na Abubakar Allawi katika nafasi zao za uongozi na utendaji ndani ya chama cha Walimu Tanzania wakisubiri maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Taifa," amesema.

Amesema viongozi hao wamesimamishwa na baraza hilo katika kikao chake cha jana, kwa kipindi chote ambacho wamesimamishwa hawatahusika na shughuli zozote zinazohusiana na CWT.

Juni 28, 2022 Seif na Allawi walihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi, Dar es Salaam kifungo cha miezi sita jela pamoja na kurejesha fedha za CWT Sh13.9 milioni baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na uchepushaji wa fedha hizo.

Chanzo: Mwananchi
Pesa hizi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom