Viongozi CHADEMA ni vema kumshukuru Wassira kwa msaada mkubwa aliowapa!!


L

Laiser James

Member
Joined
Dec 5, 2013
Messages
77
Likes
1
Points
0
L

Laiser James

Member
Joined Dec 5, 2013
77 1 0
Hakika waliosema kwamba mipango ya Mungu sio ya Mwanadamu hawakukosea.
Wakati mwanadamu anawaza mambo ya kesho na keshokutwa Mungu yeye anajua Mambo ya miaka hata 100 ijayo.

Mwaka jana kabla ya Chadema kugundua hila na mipango ya CCM wakishirikiana na jeshi la polisi,usalama wa taifa na baadhi ya viongozi waandamizi wa Chadema kuhakikisha kuwa Chadema kinasambaratika au kufa kabla ya mwaka 2014, Waziri ktk ofisi ya Rais mahusiano mema mh Steven Wassira alijisahau na kujikuta akitoa siri hiyo kwa kusema kuwa Chadema kitakufa kabla ya 2014.

Kuanzia hapo baada ya kauli hiyo kutolewa na mh Wassira,ndipo tukaanza kushuhudia baadhi ya viongozi wa Chadema wakikamatwa na kushtakiwa na kuhusishwa na UGAIDI.

Ni baada ya kauli hiyo ya Wassira pia tukashuhudia baadhi ya viongozi wa CDM wakihusishwa na njama za kukipasua au kukigawa chama kwa kuandaa mipango ya uwasi kwa uongozi wa juu(Mwenyekiti,na katibu mkuu) kabla hata muda wao wa kuongoza haukwisha.

Haya na mengine mengi tunayoshuhudia sasa ni ktk mipango ile iliyokuwa imeandaliwa na Serikali ya CCM ikishirikiana na Wachumia tumbo wachache ndani ya Cdm kuhakikisha kuwa walichokipanga ambacho Wassira alituambia juu ya hujuma dhidi ya Cdm,inafanikiwa.

Mungu ni mkubwa kwa kuwa baada ya Wassira kuropoka,uongozi wa Chadema chini ya MIAMBA MIWILI iliyoshindikana kununuliwa au kurubuniwa na CCM, mh Mbowe na Dr Slaa haikukaa kimya ila iliendelea kutumia intelejensia ya chama kuchunguza kauli ya Wassira na kulinganisha na matukio yaliyokuwa yakitokea na kugundua kwamba kauli hiyo ina maana kubwa.

Leo tumeshuhudia aliekuwa naibu katibu mkuu wa Cdm mh Zitto na wenzake wakivuliwa uongozi.hii inatokana na kauli ya Wassira kuwa Cdm kitakufa kabla ya 2013.
Chadema baada ya kupata ushahidi usiokuwa na mashaka dhidi ya viongozi hao kuhusika na mtandao wa kuuwa au kukigawa chama ndipo wakabaini kuwa kauli ya Wassira ilimaanisha nini.

Pamoja na kuwa Chadema km ilivyowahi kusemwa na katibu mkuu wao Dr Slaa kwamba wana watu ndani ya Ikulu,Usalama wa taifa na hata serikalini ambao wanawaambia kila linalopangwa dhidi ya Chadema, Lakini pia CHADEMA itakuwa haifanyi vema km haitamshukuru Wassira ambae amekuwa msaada mkubwa sana kwa Chadema kwa uropokaji wake.

Ndio maana ninasema viongizi wa Chadema ni vema wakamshukuru Wassira.
 
I

ilboru1995

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
2,331
Likes
19
Points
0
I

ilboru1995

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2007
2,331 19 0
bond ya Mbowe na Dr Slaa ni Zaidi ya Sigma BOND!...Shukran ziende kwa makamanda wa ukweli Ben Saanane, Mnyika, Lisu et al ...siku zote mmekuwa mbele ya mazoba CCM...
 
K

kikule

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Messages
217
Likes
30
Points
45
K

kikule

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2010
217 30 45
magamba mwaka 2014 tutayashaga sana na 2015 tunayafukia rasm
 
manning

manning

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2013
Messages
3,524
Likes
115
Points
160
manning

manning

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2013
3,524 115 160
nakupongeza mkuu , ila napenda ujue kuwa Wasira ndie mmoja wa waanzilishi wa CHADEMA. na katika orodha ya waanzilishi wa CHADEMA WASIRA YUMO ambayo iko kwa msajiri wa vyama . kwa hiyo CHADEMA ni motto wa Wasira. Huwezi ukamzaa mtoto halafu ukamtelekeza. Wasira bado ni mlezi wa chadema na anataka kuweka rekodi ya chama alichokianzisha kushika dola. Ninavyojua Wasira yuko CCM kimwili lakini kiroho yuko CHADEMA , ILA PIA NAMPONGEZA KWA JINSI ANAVYOWAZUGA CCM kwa kujidai anaiponda sana CHADEMA n akuwa yuko tayari kuiangamiza, lakini chadema inaendelea kuimalika. Siri za mpango mzima anawapa,. Ukiona kwenye msiba mtu analia sana ujue ndiye kamuua marehemu.
 
Lekakui

Lekakui

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
1,446
Likes
53
Points
145
Lekakui

Lekakui

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
1,446 53 145
I think you have a point,though am not sure with WASSIRA,but all in all message delivered!!!!
 
chuki

chuki

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Messages
2,694
Likes
17
Points
135
chuki

chuki

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2011
2,694 17 135
Wassira kiboko yenu, tangu awali mnahofu na mnajua kama yeye akipewa kijiti na CCM nadhani Yule Babu Slaa atapata tumbo la kuhara.

Chadema yenyewe imeishajifia sahizi mnagawana mirathi.

Viva Tyson Viva.
 

Forum statistics

Threads 1,236,327
Members 475,099
Posts 29,254,324