VIONGOZI AFRIKA NA AHADI: Kabila=0; Kikwete =0 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VIONGOZI AFRIKA NA AHADI: Kabila=0; Kikwete =0

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbunge, Oct 9, 2008.

 1. M

  Mbunge Senior Member

  #1
  Oct 9, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UPEMBUZI unaonesha kwamba marais Kabila na Kikwete ndio wanaoongoza Afrika kwa kutoa ahadi zisizotimizwa.

  Kabila aliahidi kuunganisha nchi; kupiga vita wizi wa madini; kuwaondoa askari mamluki wa Rwanda na Burundi toka Kongo; na kummaliza Jenerali wajina wa baba yake, Laurent Nkunda.

  Yote hayo karamba garasha. Na sasa Nkunda anatishia kuikomboa Kongo. Kila la kheri ili mradi tu msiwazidishie mno mateso wananchi wa Kongo.

  Mwenzake naye hapa Tanzania kaahidi mengi: kuleta muafaka=0; kupiga vita rushwa na ufisadi=0; kuleta neema kwa watu wote=0; ari mpya=0; kasi mpya=0; nguvu mpya=0; Tanzania bila ukimwi=0; kuuondoa umasikini=0; kujenga udugu na nchi za China, Japani, Scandinavia na zote ambazo hazina historia ya kusababisha vita hivi au vile na nchi zingine duniani=0; uchumi mbadala=0; ajira=0; usafi=0; umeme wa bei nafuu=kafungwa 10; maji kwa wote=kafungwa 2; madini kuwa na manufaa kwa Watanzania=0; mawaziri wachapa kazi-kafungwa 1; mishahara ya walimu na madaktari kafungwa 4; demokrasia Tanzania; kafungwa 3; uwazi na ukweli=anarudia kule kule kwa Mkapa na wizara yake bomu ya habari nchini.

  Lakini angalau kafunga magoli kwenye kuhatarisha amani ya Tanzania na Afrika kwa kujenga ukuruba na Marekani [na imeandikwa Takribun Marekani!!!].

  Baraza kubwa mno la mawaziri [not manageable span of control] na mawaziri wasio na performance yartdstick. Kisha kushindwa kuelewa kabisa umuhimu wa delegation na decentralization katika good governance.

  Kama vile Nyerere alivyoshindwa katika kuleta Ujamaa kwa kuwa na mawaziri na watendaji 'bogus' ambao moyoni walikuwa mabepari lakini usoni wakijifanya wajamaa ndivyo leo ndugu yetu anajikuta ana mawaziri ambao usoni wanaonesha uwezo, nia na sababu lakini moyoni na rohoni hawana uwezo, nia wala sababu kwani wapo hapo walipo kwa ajili ya wake zao, watoto wao, jamaa zao, ndugu zao na makabila yao. Pole sana mzee!
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Oct 9, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  I for one didn't believe a thing Kikwete was promising. How can you believe someone who has never (at least I haven't seen anything) delivered on a promise before? Does that even make sense?
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Easier Said Than Done!
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Oct 9, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  He performs in Modeling.our superstar actor!
   
Loading...