Viongozi acheni tabia hii - mazishi ya wakili Stanslaus Boniface Makulilo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi acheni tabia hii - mazishi ya wakili Stanslaus Boniface Makulilo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAKULILO, Jun 3, 2012.

 1. MAKULILO

  MAKULILO Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Viongozi acheni tabia hii


  Na Happiness Katabazi
  BABA wa taifa aliwahi kusema ‘ukweli una tabia moja nzuri sana kwani auchagui rafiki wala adui’.
  Na kwa mara nyingine leo nalazimika kutumia nukuu hilo kwasababu mada yangu nitakayoijadili leo kwa asilimia kubwa itagemea sana kuhusu suala zima la ukweli.

  Itakumbukwa kuwa Mei 29 mwaka huu, mwili wa gwiji la uendeshaji wa mashitaka nchini ambaye alikuwa na wadhifa wa Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha uendesha mashitaka na pia ndiye aliyekuwa Msimamizi mkuu wa uendeshaji kesi zenye maslahi kwa umma, Stanslaus Boniface Makulilo (44),uliagwa na kuzikwa katika nyumba yake ya milele pale katika Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam.

  Jamii ya wasomi wa fani ya sheria wakiwemo majaji,mahakimu, mawakili wa serikali na kujitegemea na wananchi wengine wa kada tofauti walishiriki katika mazishi mazishi hayo na wengi wao walikuwa na huzuni na wengine kushindwa kujizuia na kujikuta kila mara wakibubujikwa na machozi kutoka na majonzi ya kumpoteza gwiji hilo la mashitaka ambalo lililikuwa ni mwiba mkali,ambaye alikuwa akiisaidia kwa hali na mali kitaaluma mahakama kufikia maamuzi ya haki na aliyekuwa ametanguliza maslahi ya taifa kwanza.

  Binafsi niliudhulia msiba huu mwanzo hadi mwisho yaani kuanzia siku aliyokufa yaani Mei 27 alfajiri katika Hospitali ya Regency pale nyumbani kwa mdogo wa marehemu Dk.Alexander Makulilo tangu hadi siku Mei 29 siku tuliyoenda kumzika Boniface makaburi ya Kinondoni.

  Ni kweli mimi nimwandishi wa habari za kimahakama na nilikwenda msibani kwanza kama mfiwa kwasababu Boniface na mawakili wengine wa serikali na kujitegema kila siku tumekuwa tukifanya nao kazi pamoja,pia nilikwenda msibani pia kama mwandishi wa habari kwaajii ya kutazama na kurekodi matukio yote yaliyokuwa yakiendelea katika msiba huo ili niuabarishe umma.

  Ama kwa hakika kwa siku zote hizo miongoni mwa viongozi wa chache ambao nilikuwa nikiwashuhudia wakifika msibani hapo na wanakaa hadi usiku ni Mwanasheria Mkuu wa serikali Fredrick Werema na Naibu wake George Masaju ,Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), Eliezer Feleshi,Mkuu wa Chuo cha Sheria(Law School) Gerad Ndika, aliyekuwa Mkuu wa Shule ya Sheria(UDSM),Profesa Paramaganda Kabudi ,Mbunge wa Kigoma Mjini,Peter Serukamba,maofisa wa jeshi la polisi ,waandishi wa habari za mahakamani mawakili wakujitegemea na wale wa serikali na kada nyingine na siku ya mazishi kule makaburini ndiyo Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe alikuja.

  Kwanza naomba ieleweke wazi kuwa wale wote ambao hawakuhudhulia msiba wa Boniface hawajatenda kosa la jinai na wala siyo deni.Na pia kuzikwa na watu wengi siyo kwenda mbinguni.

  Lakini mimi binafsi na baadhi ya watu walioudhulia msiba huo tumebaki tukijiuliza ni kwanini viongozi wa juu kabisa wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal,Waziri Mkuu Mizengo Pinda.Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye, Katibu Uenezi wa Chama Cha Demokrasi Chadema, john Mnyika na vyama vingine na vile vyama vya kiraia, wale wapambanaji wa ufisadi walishindwa kabisa kuudhulia msiba huo au hata kutuma salamu za pole kutokana msiba wa Boniface?

  Ieleweke wazi kuwa tangu Kikwete apishwe kuwa rais wa taifa hili Mei 21 mwaka 2005, serikali yake ndiyo imeandika historia ya kuwafikisha vigogo mahakamani kwa kesi mbalimbali na hatua hiyo ilitokana na kelele nyingi zilizokuwa zikipigwa na wananchi zilizotaka watuhumiwa wa ufisadi wa wizi wa fedha za EPA,Richmond,UDA,Shirika la Ndege(ATCL) wafikwe mahakamani haraka.Na walifikishwa mahakamani na DPP-Dk.Feleshi na Boniface na wenzake ndiyo waliokuwa wakiziendesha kesi hizo kwa nguvu zao zote hadi kufikia hatua ya kutishiwa usalama wao na watu wasiojulikana mara kwa mara.

  Ni huyu Rais Kikwete Pinda na huyo Nnauye na wabunge wengine wa ccm kwa mara kadhaa tumekuwa tukiwashuhudia katika majukwaani wakijinasibu kuwa serikali ya awamu ya nne imefanya mengi ikiwemo kuwafikisha mahakamani vigogo. Ni kweli serikali hiyo hilo imelifanya lakini cha kushangaza viongozi hao kupitia wasaidizi wao wameshindwa hata kuandika taarifa kwa umma kwamba wameupokeaje msiba huo.Ni ajabu sana.

  Uenda Boniface aina ya mchango wake kwa taifa hili ulikuwa hauthamini na hautiliwi maanani sana na makundi hayo kuliko mchango uliokuwa ukitolewa na watanzania wenzetu kama wasanii na wanasiasa waliotangulia mbele za haki ambao vifo vyao vilisababisha CCM na serikali yake vilijifanya kuonyesha kutaharuki hadi rais Kikwete,Dk.Bilal kwenda kwa zaidi ya mara mbili kwenye msiba mmoja.Katika msiba mmoja ambao sitalitaja jina la marehemu hao, Rais Kikwete na viongozi wenzake licha marehemu hao hata hawakuwa watumishi wa serikali waliofariki mwaka huu waliudhulia tena hadi usiku lakini viongozi hao wakashindwa kutenga hata siku moja kuja kuudhuria msiba wa Boniface.

  Niwe mkweli kabisa tabia hii imeanza kuwafanya baadhi ya watu kuamini kuwa viongozi wetu wa kisiasa wanachagua misiba ya kwenda.Wakifikiri msiba fulani kama wa Boniface ambao ulisheheni wasomi wa sheria hawatapa upenyo wa kujigenga kisiasa hawaudhurii wala kutoa salamu za pole na msiba fulani wakishapiga hesabu wakabaini wakiudhulia msiba huo watapata upenyo wa kujitangaza kisiasa basi haraka sana wanaudhuria msiba huo na kutoa salamu za pole.

  Hii ni tabia isiyopendeza na kukatisha tamaa watendaji hususani wale wa serikali ambao ni waadilifu na wachapakazi kwa viongozi hao kwani miongoni mwao waliniuma sikio msibani wakisema msiba wa Boniface ndiyo ungekuwa ni msiba wa msanii basi Ikulu ingeamia katika msiba huo na kutoa misaada mingi.Kauli kama hizi hazipendezi kwani zinaonyesha kutolewa na wafanyakazi wa serikali walioanza kukatishwa tamaa na viongozi wao.Badilikeni.

  Hivi katika hali ya kawaida leo nyie viongozi hao nyie vyama vya upinzani,CCM na wanaharakati na nyie baadhi ya wabunge mliokuwa mmejipambanua kupambana na ufisadi mnaweza kuwa na jeuri ya kusimama majukwaani na kutuleeza nini kuhusu kesi za ufisadi, wakati hata kutoa salamu za pole kwa marehemu Boniface aliyekuwa akiongoza dawati la kuendesha kesi zilizokuwa na maslahi ya umma mmeshindwa?Kutwa kutoa matamko kuhusu ufisadi, maandamano na kupikiana majungu na kufukuzana kazi na kusuka makundi ya kugombea urais mwaka 2015.

  Ndiyo maana kuna baadhi ya majaji ,maofisa wa serikali waliniuma sikio wakiambia kuwa miongoni mwao muda mrefu walichaacha kuudhulia sherehe za kitaifa kwani wao wakifa vingozi hao wa juu wa serikali hawaudhulii madhishi yao.
  Boniface alipenda sana kazi ya Uwakili wa Serikali na hasa kuendesha mashtaka.Alikuwa tayari kuendesha kesi yoyote bila woga.Alikuwa msaada kwa mahakama katika kufikia maamuzi ya haki.

  Hii inadhiirika kwa kusoma hukumu na maamuzi ya mahakama ya mashauri ambayo aliiwakilisha serikali.
  Mfano mzuri ni hukumu ya Mahakama ya Rufaa Na. 250/2006 katika kesi ya Silivester Hillu Dawi na wenzake dhidi ya Mkurugenzi wa Mashitaka ambapo jaji Edward Rutakangwa alimwelezea Boniface aliyekuwa akiiwakilisha serikali katika shauri hilo kuwa ni mkweli na mpenda haki.

  Jaji Rutakangwa aliweka kanuni ya washitakiwa wanaokabiliwa na shitaka kuchangia nusu ya thamani ya mali inayohusika shtaka husika ili kupata dhamana badala ya kila mshitakiwa kutoa nusu ya thamani hiyo.

  Kesi nyingine ni ya Mwenyekiti wa Timu ya Simba, Ismail Aden Rage dhidi ya Jamhuri katika Mahakama ya Rufaa Na. 286/2005, ambapo Jaji Mroso alieleza wazi kuwa Jamhuri iliyokuwa ikiwakilishwa na Boniface,ilikuwa imewakilishwa na mtu mwenye uwezo na msaada pale alipotamka.

  Kwa hukumu hizo mbili,ni wazi zimeuthibitishia umma kuwa hata Mahakama ya Rufaa Tanzania ilikuwa ikiheshimu na kumtambua Boniface kuwa ni wakili mahiri wa serikali.Na sisi watu tunaofikiri sawa sawa na wale wasomi wa sheria tutaendelea kuuenzi mchango wa marehemu na kumkumbuka daima katika tasnia ya sheria nchini. Mungu ailaze roho ya Boniface mahali pema peponi.Amina.

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
  0716 774494
  www.katabazihappy.blogspot.com
  Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Juni 3 mwaka 2012.
  Viongozi acheni tabia hii


   
 2. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha! Siasa ni kitu mbaya sana.
   
 3. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah,ni ukweli kabisa!
   
 4. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Pole (Bw.Makulilo wa JF) ndio usanii wa viongozi wetu unapojidhihirisha.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,571
  Likes Received: 18,542
  Trophy Points: 280
  Msiba ulikuwa ni wa Kanumba!. Hii mingine yote ni kama misiba tuu!.
   
 6. J

  Juma123 Senior Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 193
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hi RIP Kamanda ulizikwa NA Mawakili wenzio NA wote Wenye mapenzi mema kwa kesi zenye maslahi ya umma, Asante Happiness Katabazi KWA kujali!!!!
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco ndio taifa letu limefika huku. Kwenye msiba wa wasanii viongozi wanasukumana kwenda msibani akitoka huyu anaingia huyu tena na vyombo vya habari vikiwa nyuma. Serikali inahudumia mazishi na kisha inatoa ubani wa milioni 10. Kwenye msiba wa mtumishi wa serikali anyefanya kazi katika mazingira hatarishi ya kusimamia mashtaka dhidi ya mafisadi hali inakuwa hiyo!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Msishangae ya Mussa kwani bado hamjaona ya firauni;hii serikali imeshindwa hata kupeleka uwakilishi kwenye mazishi ya Dr. Kyaruzi mmoja wa waasisi wa kugombea UHURU wa nchi hii itakuwa kwenye mazishi ya huyu wakili!! Hii serikali haina mbele wala nyuma bali ipo ipo tu!!
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Hahaha! Na wakiumwa ze comedy presidaa anaenda kusalimia wasanii wenzie! Ama kweli kupanga ni kuchagua!
  Makulillo, pole na msiba mwayego. Ila kaka Malecela nahisi atakuwa aliwakilisha aisee, hamkumuona tu
   
 10. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Alikuwa "naibu mkurugenzi wa mashitaka" na majukumu yake makubwa yalikuwa kusimamia kesi za ufisadi! Na kwa jukumu hili alishawahi kutishiwa maisha na watu asiowafahamu.
  Sina la kuongeza mwenye macho haambiwi tazama.

  Tunashukuru Happiness kwa kutujuza, tuiombee sana nchi yetu.
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Pasco, viongozi wetu walianza vibaya na watu wengi walihoji kama wataweza kuendeleza huo mtindo wa kutaka kuonekana kwenye misiba. Siku chache zilizopita tulikuwa na habari kama hii kuhusu msiba ya Dr Kyaruzi, na leo tunaongelea mtumishi wa serikali. Na bado bunge halijaanza tuone itakuwaje. Nchi haina tena kanuni, mambo ni mtindo wa kushtukiza.

  Sitoshangaa kusoma mtu analalama kuwa rais, makamu wa rais, waziri mkuu na hata kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni hawakuonekana kwenye kitchen party ya binti yake. We are heading that direction.
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Ila dada Happy with all due respect jifunze kozi ya kiswahili kwa kweli! Wewe kama mwandishi hupaswi kutumia maneno haya! Najua its mother tongue effect ila ukijifunza utaweza:
  Auchagui
  Inadhiirika
  Niwaabarishe
  Hawaudhulii mazishi
   
 13. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Fikiria kwenye gazeti kuna mhariri na wasaidizi tena wanalipwa mishahara na hawayaoni hayo. Inasikitisha
   
 14. mzalendokweli

  mzalendokweli JF-Expert Member

  #14
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mweh.!
   
 15. mzalendokweli

  mzalendokweli JF-Expert Member

  #15
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  thanx Happy. RIP learned brother.
   
 16. m

  mahoza JF-Expert Member

  #16
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Nimeipenda hii. Editor aseme kitu hapo. Kwa kweli ujumbe umefika lakini hayo maneno na kwa mwandishi!
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Jun 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,469
  Likes Received: 19,854
  Trophy Points: 280
  jamani hadi kwenye mazishi tunaanza kushikana mashati? mwacheni ndugu yetu alale kwa amani
   
 18. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #18
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Watanzania walalmishi sana,

  hivi kweli kila msiba unataka rais, makamu wa rais , waziri mkuu wahudhurie? Jamani huu si mzaha huu! Mbona watu wanapenda kulalama sana!
   
 19. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #19
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Nina hakika hivi vituko sasa vimewachosha wasomi wa hapa nchini.
  Wamefariki magwiji wa fani mbalimbali pale UDSM,ajabu watawala wetu huwa hawaonekani.
  Inashangaza sana.Kwa nini hawakutaka kwenda kumzika mtu mkubwa wa hadhi ya MAKULILO?
  Poleni wafiwa.
   
 20. t

  tabu kuishi JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Iatakuwa hakuwa mjenzi huru
   
Loading...