viongozi 6 wa dini wakiri kuhusika na madawa ya kulevya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

viongozi 6 wa dini wakiri kuhusika na madawa ya kulevya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 18, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  VIONGOZI sita wa madhehebu ya dini wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini, wamejitokeza mbele ya Kamati ya Maadili ya Viongozi wa Dini na Haki za Jamii na kukiri kujihusisha na biashara hiyo kwa muda mrefu sasa.

  Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, baada ya kuhojiwa, viongozi hao waliiomba Kamati hiyo kutowataja hadharani majina ama madhehebu yao kwa kuhofia kubezwa kwa madhehebu wanayoyaongoza.

  Akizungumza mwishoni mwa ziara yao Zanzibar, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentekoste Tanzania, alisema mbali ya orodha hiyo, ipo pia ya watu 18 wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wanasiasa wanaojihusisha na biashara hiyo.

  Alisema orodha zote zitafikishwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchini.

  Mchungaji Mwamalanga alisema tatizo la ongezeko la dawa za kulevya, pia inazihusu nchi mbalimbali duniani na kwamba kamati hiyo itakutana na kamati nyingine kama hizo za nchi za Maziwa Makuu kuzungumzia ufumbuzi wa suala hilo.

  Alisema mkutano huo pia utapendekeza kwa mabunge ya nchi hizo na Bunge la Afrika Mashariki kutunga sheria za kuwafilisi wote waliojilimbikizia mali kutokana na biashara za dawa za kulevya kwa nchi wanachama.

  Hata hivyo, Kamati hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Dini na Haki za Jamii ikiwa Visiwani, imesifu na kupongeza juhudi za Jeshi la Polisi kwa hatua zao za kukabiliana na ongezeko la dawa za kulevya.

  Akizungumzia kero ya dawa za kulevya visiwani hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma Mohammed, alisema Jeshi hilo limekuwa likiwakamata wengi wa wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za kulevya na kuwafikisha mahakamani.

  Hata hivyo, Kamanda Aziz alitoa mwito kwa wananchi na wadau mbalimbali wa usalama kuendelea kusaidiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za wale wote wanaojihusisha na mtandao wa dawa hizo.

  Kamanda Aziz alisema kama kila mwananchi atatoa taarifa za siri Polisi za kuwepo kwa mtu ama kundi la watu wanaojihusisha na biashara hiyo ama uhalifu mwingine wowote, ni wazi kuwa Polisi itawatia mbaroni.

  Wiki iliyopita, watu wawili wakazi wa Dar es Salaam, wamekamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume, Zanzibar kwa nyakati tofauti wakitokea Brazil, ambapo kila mmoja alipatikana na kiasi kikubwa cha dawa za kulevya aina ya kokeini.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,631
  Trophy Points: 280
  hawa nahisi watakuwa pelege tu makambale yako dar yanaongeza magari makubwa kwenye list
  anyway list haswaaaaaaaaaaa anayo JK Mwenye uwezo wa kumuhoji alipoificha aje atueleze yyuko nani
  hao kina panzi wala atuwaitaji mje kujichukulia vyeo juu yao njooni Dar
   
 3. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #3
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizi taarifa zinaacha maswali mengi, ilikuwaje wajisalimishe kwa pamoja kwani walikuwa wakishirikiana kufanya biashara hiyo ambayo ni ya siri? Viongozi hao ni wa dhehebu moja? Isije ikawa taarifa hizi ni za ku cover story fulani ya mkuu...
   
 4. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  mbona hili la viongozi wa dini flan kuwa wanajihusisha na madawa ya kulevya lipo open sana-si jipya na hawajaanza kukiri leo-kifupi ni kwamba prezidaa analifahamu na majina yote anayo-kama hana basi akiyahitaji atapewa mara moja-sema kaamua kulipotezea
   
 5. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tumechoka na orodha isiyo namajina kama wanaamini kwenye kusmamia ukweli wayaweke wazi!
   
 6. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  viongozi hawa ni wa dhehebu moja-hawakuanza kujisalimisha leo-walishafanyaga mkutano kama huu arusha-hawa mabwana wakajitokeza hadharani kipindi hicho-,na wakaomba wasilhusishwe kwenye mchakato wa kupanga jinsi ya kuzuia uingizwaji wa haya madawa-maana wao ndo biashara inayowaweka mjini-as long wanajua hawawez chukuliwa hatua-ndo maana wameamua kujitokeza tena
   
 7. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kwa nini wasitajwe. Hii ni vita na maadui wote wanapaswa kufahamika hadharani.
   
 8. s

  sir echa Member

  #8
  Jul 18, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kweli kuna UWAZI na UKWELI wawataje hadharani,hao tayari ni watuhumiwa na kama imethibitishwa basi wapandishwe kizimbani sheria ichukue mkondo wake.
   
 9. k

  kbhoke Member

  #9
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Mwandishi wa habari hii, alitaka kuuza gazeti, hamna chochote hapa!
   
 10. P

  Popompo JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  hii habari niliisikia jana star tv kwa kweli ipo kama kumwosha mkuu!mimi ni Mtanzania na nina uchungu na taifa langu naona huu unaoendelea ni uhuni uliopitiliza.vijana kote mijini na vijijini wanateketea kwa ajili ya matumizi ya haya madawa halafu mtu anakuja na story eti wameombwa wasiwataje na wao wakakubali!jamani natamani kutoa lugha ya kuudhi kuanzia na rais mwenye mamlaka halafu hafanyi chochote kazi kutalii wakati vijana wanaangamia!hawa viongozi wa kiroho nao watachomwa moto wa jehanam kwani wanawaficha hao wanaoliangamiza taifa!
   
 11. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  ni upuuzi kusema kitu kisichokamilika, ni vipi hawawezi kuwataja? Kwa maslahi ya nani? Ina maana hao viongozi wa dini hata wakiwa majambazi hawatatajwa? Kiufupi viongozi wa juu wa serikari ndio wanalea huu upupu na inawezekanaa wao ndio wanawawezesha kifedha.
   
 12. M

  Mr.Right JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 408
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona JK keshawataja kwamba wametoka ktk dini ya Kikristo. Aliwahi khutubia na kuwaambia waache hizo tabia, mbele ya Kanisa. Watu wakaanza kupiga kelele JK anawaonea. Sasa hivi ukweli ndiyo huo, hawa jamaa wameamua kujitokeza wenyewe. Sasa majina ya nini? hawa ni viongozi wa dini na si vizuri majina ya kutajwa, kwa sababu nchi yetu ni sensitive sana ktk mambo ya dini.
   
 13. M

  Mr.Right JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 408
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mbona JK keshawataja kwamba wametoka ktk dini ya Kikristo. Aliwahi khutubia na kuwaambia waache hizo tabia, mbele ya Kanisa. Watu wakaanza kupiga kelele JK anawaonea. Sasa hivi ukweli ndiyo huo, hawa jamaa wameamua kujitokeza wenyewe. Sasa majina ya nini? hawa ni viongozi wa dini na si vizuri majina ya kutajwa, kwa sababu nchi yetu ni sensitive sana ktk mambo ya dini.
   
 14. M

  Mr.Right JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 408
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mbona JK keshawataja kwamba wametoka ktk dini ya Kikristo. Aliwahi khutubia na kuwaambia waache hizo tabia, mbele ya Kanisa. Watu wakaanza kupiga kelele JK anawaonea. Sasa hivi ukweli ndiyo huo, hawa jamaa wameamua kujitokeza wenyewe. Sasa majina ya nini? hawa ni viongozi wa dini na si vizuri majina ya kutajwa, kwa sababu nchi yetu ni sensitive sana ktk mambo ya dini.
   
 15. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  lengo hapa si kulinda heshima bali hawaitajiki ktk uongozi ndio maana nataka watajwe, mbona wanaobaka wanatajwa? Unaweza kuniambia madawa ya kulevya yana kipi cha ziada? sidhani kama wewe unaweza ukampeleka binti yako ktk shule ambayo inasifika kwa uhuni ili akafundishwe.
   
 16. Ungana

  Ungana JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 358
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Islamist JK up in arms against pro-Chadema Clergy!
   
 17. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Watajwe.....nashangaa sijui ni kwanin huwa kuna kificho sana kuhusiana na watuhumiwa WAKUBWA WA COCAIN DEAL
   
 18. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Lazima viongozi hao watajwe hadharani ili waumini wao wawajue.Watumishi hawa wa shetani wame endelea kulisha pumba their unsuspecting congregations for too long. Hali hiyo haiwezi kuachwa iendelee.Lazima waumini wao wajue,waamue wenyewe kubaki au kuondoka.
   
 19. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Habari iliyoletwa ni ya UONGO kwa uthibitisho wa kufuatilia watoa taarifa (chanzo), upande wa ilikotoka (wa Dar alitoa jina 1 ilikumnusuru mkuu na aibu ya kuitwa MWONGO kufuatiwa na deadline aliyopewa na maaskofu, japo alithibitika kuwa hivyo, leo anakuja mwingine na majina 6 toka Znz) eti ni kama ku-balance Bara wapo na Zenj-bar wapo,duh! Hebu wakuu naomba mfuajilie kama kweli hayo majina yapo huko Znz yaani la huyo afisa wa Polisi na Mch wa KLPT.

  Lakini nikirudi kwa Edward Teller ni kuwa BWANA Mungu, anachumkia shahidi wa uongo asemaye uongo.
   
 20. M

  MSEHWA Member

  #20
  Jul 18, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe ikubali habari hiyo. Mbona mnataka kuwasafisha? Mie najua maaskof wakiombwa wasisemwe wanakubaliwa b'se wao wanajiona wako juu ya sheria. Iko siku mambo yatakua hadharani. Ukiona shule za st zinajengwa ujue kuna siri kali. Haya teteeni wenye mbeleko ya kuwabeba waovu sisi yetu macho.
   
Loading...