Viongozi 32 wa ngazi ya juu wa CDM warudisha kadi zao za uanachama!

Viongozi tajwa hapo juu wa CDM Mkoani Mwanza wilaya ya Nyanza wameripotiwa kurudisha kadi zao ya uanachama.

Wamerudisha kadi zao baada ya chichiem kufanya mkutano wa hadhara ktk wilaya ya Nyanza na ndipo mafisadi wakawarubuni wanaCDM hao na kurudisha kadi ya chama na kupewa ya chichiem.

Mgeni rasmi ktk mkutano hiyo ni waziri wa nishati na madini William Ngeleja.

Nini itatokea hapo? Kama siyo wamegawiwa kodi zetu na huyu fisadi wa mafisadi?

Source: RFA!

Propaganda zenu pelekeni huko huko,hao ni wanachama wa CCM sio CDM.
 
Of all the people Ngeleja bado anathubutu kutoka kifua mbele na kupokea wanachama nkikumbuka alivyotutenda kwa mgao na mikataba ya kizushi.
 
Kwanza wana Jamii lazima mjue kuwa CCM imepoteza umaarufu sana Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla. Hivyo Ngeleja anachokifanya ni kujipendekeza kwa mgombea Urais wa CCM 2015 pamoja na halmashauri nzima ya NEC ili aonekane ana nguvu kule kanda ya ziwa, ili kwa lolote litakalo tokea huko mbele ya safari aonekane ni potential person pale Mwanza. Hii ni pamoja na kujifahamu/kuelewa kuwa ktk utendaji ndani ya wizara hana lolote au hajiamini, kapoteza kabisa umaarufu.[/QUhiyo ni kweli kabisa mkuu.mr megawatt anatafuta nafasi kwa mgombea urais wa 2015 kwani anajua kabisa kwamba kiutendaji wa kazi za kiserikali hakuwezi kumfanya awe karibu na mgombea wa 2015 kwani ataonekana kuwa na ushawishi mkubwa kisiasa au kichichiem huko mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla.
 
Gazeti Moja leo limesema Ngeleja alikuwa hapokei simu ili athibitishe vigogo gani wa Chadema Sengerema amewasambaratisha ha ha ha hana jeuri jamaa jizi limekubuhu anadhani anaweza kuwajairo wana Sengerema

Yeye mwenyewe yuko njiani kuwafuata masha na diallo 2015
 
Watarudi wamechukua fedha siku ya pili ni CDM,kuwa na kadi sio kuwa muumini wa chama hicho,fainali ni 2015
 
Wakiwapa pesa rudisha kadi kwani hali ni mbaya ila baadae kata kadi nyingine faida kula. hiyo ndiyo dawa ya chichiemu! mbona hizo fedha wengine hazitifikii?
 
Back
Top Bottom