Viongozi 32 wa ngazi ya juu wa CDM warudisha kadi zao za uanachama!

Liverpool,
Hii taarifa unayopitoa hapa ni imekwisha tokea Sengerema, tarafa au kata ya Nyanza na hao wanaozugmizwa ni idadi ya viongozi pamoja na wanachama.. Kwa hiyo kubali kusahihishwa haina noma kaka!... Tunajua habari hii sio ya uongo isipokuwa umekosea wilaya ilipotokea...

Thankx Best! Humu ndani kuna watumwa wa chichiem tena sana tu! Nami nimeshatoa source ya thread inatokea wapi.
Lakini hawataki kunielewa.
Lakini nimewaambia ukweli na asietaka kuielewa somo lilivyo nakwambia ni juu yake na aliyenielewa ni dhahiri ndio wetu huyo Best.
Cjaenda tofauti na mrusha hili radio free africa.!
Sasa Mi nimeshangaa kuona comment ikiwa kedekede Best!

Ila Mi ujumbe nimeufikisha kama nilivyoipokea!
 
Wapo baadhi yao wanaona kuhama hama ni ajira. Watakula hivyo vihela na keshokutwa utasikia wamekimbilia NCCR au CUF. Hivi kweli CCM ndiyo chama cha kukimbilia? Ngeleja anajiosha tu ili hasijepigwa panga kwa sababu ya ufisadi wake Madini.
 
Viongozi tajwa hapo juu wa CDM Mkoani Mwanza wilaya ya Nyanza wameripotiwa kurudisha kadi zao ya uanachama.

Wamerudisha kadi zao baada ya chichiem kufanya mkutano wa hadhara ktk wilaya ya Nyanza na ndipo mafisadi wakawarubuni wanaCDM hao na kurudisha kadi ya chama na kupewa ya chichiem.

Mgeni rasmi ktk mkutano hiyo ni waziri wa nishati na madini William Ngeleja.

Nini itatokea hapo? Kama siyo wamegawiwa kodi zetu na huyu fisadi wa mafisadi?

Source: RFA!

Mkoa wa Mwanza hauna Wilaya ya Nyanza. Nafikiri huijui vizuri Nchi yako.
 
Ngoja ataona moto utakao washwa jimboni mwake,anjidanganya na viongozi njaa 32,wala hao co makamanda wa maana sisi hatuangalii, 2015 ni lazima kieleweke.
 
Wananchi ndio wanaochagua pia ndio wanao teseka na maisha ya ssa na ndio wataipiga chini Ccm na sio hao viongozi njaa/matumbo.Kwanza tujiulize Ngeleja ukiondoka hapo Nishati na Madini atakumbukwa kwa lipi? Matamko ya kuropoka?10% ya mikataba ya madini?Au kuchangisha posho ya kuhonga wabunge?Au waziri mwenye rekodi ya kukataa kujiuzuru kwa madudu yanayofanyika chini yake?Kweli eti Tanzania tuendelee kwa viongozi dizaini ya Ngeleja!
 
hilo si jambo la kuliweka akilini,ni kawaida yao ccm kununua baadhi ya viongozi njaa wa upinzani ili kuuza taarifa,huku kwetu kiongozi alikuwa ananunuliwa kwa elfu 20,na mwanachama wa kawaida elfu 5.na mpaka sasa wote wamerudi ktk vyama vyao.kamanda wa kweli mwenye akili timamu hawezi kwenda ccm,hao waganga njaa tu.sukari elfu 3,
mafuta ya taa 2500
mbole ya ruzuku toka elfu 21 hadi elfu 52 kwa mfuko!mtu anakwenda ccm kwa kuvutiwa na nini kama sio njaa?hila zao haziwezi kuzima moto wa mabadiliko japo wasaliti hawakosekani.
 
Ukiona kiongozi au mwanachama yeyote kutoka upinzani anahamia ccm katika kipindi hiki ambacho watu wengi wameichoka ccm mwogope sana kuliko simba mwenye njaa
 
Na hizo ndizo wilaya zilizopo kwa sasa ukiondoa Geita na Sengerema ambazo zimeungana kutengeneza mkoa!!
hiyo ni janja ya chichiem kupotosha watu! maana mtu akisikia pasipo kuweka umakini ataamini kuwa mwanza umebomolea. ni sawa na mfano wa ndege ilianguka mpakani na wakawapo majeruhi! je, hao majeruhi wazikwe wapi? mwengine atakurupuka na kesema wazikwe walikokuwa wanaelekea, mwingine atasema wazikwa walikokuwa wanatoka na mwingine aweza kusema wazikwe mpakani!! swali je, majeruhi wanazikwa? vivyo hivyo je, wilaya isiyokuwepo inawezaje kuwa na viongozi?

ZINGATIA KWENYE RED, hii wilaya ya Nyanza imekuwa ngeni kwangu labda kwavile nimekuwa sipo huko muda mrefu but nimegoogle sikuipata kabisa. Nilipotoka mimi niliacha Mwanza ilikuwa na wilaya kama ifuatavyo. ILEMELA, NYAMAGANA, SENGEREMA, GEITA, MAGU, KWIMBA, MISUNGWI NA UKEREWE. Hii wilaya ya Nyanza iko upande gani mkuu?
 
Na hizo ndizo wilaya zilizopo kwa sasa ukiondoa Geita na Sengerema ambazo zimeungana kutengeneza mkoa!!
hiyo ni janja ya chichiem kupotosha watu! maana mtu akisikia pasipo kuweka umakini ataamini kuwa mwanza umebomolea. ni sawa na mfano wa ndege ilianguka mpakani na wakawapo majeruhi! je, hao majeruhi wazikwe wapi? mwengine atakurupuka na kesema wazikwe walikokuwa wanaelekea, mwingine atasema wazikwa walikokuwa wanatoka na mwingine aweza kusema wazikwe mpakani!! swali je, majeruhi wanazikwa? vivyo hivyo je, wilaya isiyokuwepo inawezaje kuwa na viongozi?

Asee!!sie tusio wenyeji wa huko kanda ya ziwa tulishaanza kutilia maanani hii...kumbe ni propaganda.
 
Gazeti Moja leo limesema Ngeleja alikuwa hapokei simu ili athibitishe vigogo gani wa Chadema Sengerema amewasambaratisha ha ha ha hana jeuri jamaa jizi limekubuhu anadhani anaweza kuwajairo wana Sengerema
 
kweli nimejua heading ya JF haiendani na baadhi ya wana JF.....hao watu wote walikuwa tayari wametemwa na CDM kwa sababu za UFISADI wao sasa kwa sababu CCM hawajijui wafanyalo ndio maana wanachukua makapi...Think twice before posting
 
Viongozi tajwa hapo juu wa CDM Mkoani Mwanza wilaya ya Nyanza wameripotiwa kurudisha kadi zao ya uanachama.

Wamerudisha kadi zao baada ya chichiem kufanya mkutano wa hadhara ktk wilaya ya Nyanza na ndipo mafisadi wakawarubuni wanaCDM hao na kurudisha kadi ya chama na kupewa ya chichiem.

Mgeni rasmi ktk mkutano hiyo ni waziri wa nishati na madini William Ngeleja.

Nini itatokea hapo? Kama siyo wamegawiwa kodi zetu na huyu fisadi wa mafisadi?

Source: RFA!
Bora wamejipambanua mapema maana cdm kuelekea 2015 kinapaswa kuwa na wapenzi wa dhati na sio mamluki kama hao kwenye nafasi za uongozi wenye tabia za kimagamba, leo akipewa ofa hii yupo tayari kula matapishi yake
 
mbona thread nyingine inayo elezea kwamba huu ni uzushi?. halafu riverpool mnamuonea bule, yeye kaleta taarifa kama ilivyo tolewa na rfa. so wakulaumiwa ni rfa sio mzee wa river. Mia
 
Back
Top Bottom