Vioja vya watoto wadogo (0-5years), tuambie vioja vya mwanao

Jembe langu lina miaka3,akimuona mtu flani akiongea kwenye tv,anakimbilia remote na kubadili chanel.Simply ana aleji naye.
Mi la kwangu lina miaka 30. Juzi limeniletea binti wa 6 mwenye ujauzito wake. Mzee mzima nakaribia kupata mjukuu wa sita toka kwa mabinti sita tofauti.
 
Dah!! Poleni kwa visa vya watoto wenu.
Ila naamini na nyinyi mliwafanyia visa wazee wenu kwa hiyo tulieni.
 
Wa kwangu Mwaka 1.7 hampendi Kunguru akimuona tu lazima amponde kwa mawe, Akilala usiku alafu Mvua akiwa inanyesha anaanza kulia "Mama Kunguru anakuja, Baba Kunguru anakuja" basi atalia weee mpaka Mvua iishe ndio analala! Najiuliza Hivi Kunguru alimfanya nini?mpaka leo sijapata jibu!

Alikuwa hafahamu kutamka vizuri neno Kikombe alikuwa anatamka "Kitombe"

Hapendi Ugali, Ukipika Ugali unaula mwenyewe. Yeye mpe wali hata kama ni kidogo kwake ni sawa tu!
Jf kiboko. Kikombe anasemaa ???
 
wale tusio na watoto hebu tubane kwa pembeni hapa kuona wenzetu wanavyo-enjoy maisha kufurahi na watoto
 
Watoto wana mambo mengi sana ya hatari na ya kuchekesha pia.

Penda sana jembe langu, alinikuta naangalia concert ya Peter Tosh akatulia tulii akawa makini kweli kuangalia sasa kazi ikaja siku nataka kumnyoa nywele asee dogo akaanza kukataa kunyolewa nywele eti ananiambia 'babaa kulee' ase nlipogundua anamuongelea Peter Tosh nlimcheka sana nikaona nimuache nazo adi siku zimkere ndio nimnyoe. Leo zina kama miaka 2 hiv hana mpango wa kuzichukia kabisa.

Ni ka dreadboy sijui shule itakuwaje mwakani. Hadi namsikitikia anavyopenda nywele zake. Utafikiri ni kamtu kazima vle.
 
Wa kwangu akiniona tu hata kama alikuwa anacheza basi ataangua kilio sijui kumchongea dada wa kazi kampiga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom