Vioja vya TAKUKURU

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,041
Pamoja na Watanzania wengi kutaka TAKUKURU iwashughulike mafisadi wakubwa wakubwa kama akina Mkapa, Chenge, Rostam, Mgonja, Mramba, Karamagi, Mkono, Mzindakaya na wengine Waliohusika na wizi wa mabilioni ya EPA, kujimilikisha Kiwira katika mazingira ya kifisadi kulipwa mabilioni ya shilingi na BoT lakini bado inawafuatilia watu ambao hata kama wana makosa lakini kamwe hayawezi kulinganishwa na ufisadi dhidi ya hao niliowataja hapo juu.

TAKUKURU tumechoka na vioja vyenu acheni unafiki kama mmeshindwa kupambana na mafisadi ni bora mtutangazie hadharani.


TAKUKURU yavamia TANROADS

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
July 11, 2008

MAOFISA wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wamevamia kwa siri ofisi za Wakala wa Barabara (TANROADS) na kuanzisha uchunguzi mkali dhidi ya tuhuma zinazoelekezwa kwa mtendaji mkuu wa taasisi hiyo, Ephraem Mrema.

Habari zilizopatikana kutoka ndani ya ofisi hiyo jana, zilisema TAKUKURU imeanza kazi ya kuhoji wahusika mbalimbali katika vikao vya siri katika ofisi hiyo.

Kwa mujibu wa habari hizo, kikubwa kilichokuwa kinachunguzwa ni endapo Mrema alikuwa analipa kodi kama ilivyoelezwa na jinsi alivyoingia katika ajira hiyo.

Habari hizo zinasema kwamba TAKUKURU ilifuatilia masuala mbalimbali kuhusu rushwa, hadi ofisi ya Kamishna wa Kodi za Ndani, na ajira yake katika Wizara ya Miondombinu na jinsi alivyoingia katika ajira hiyo wakati kukiwa na wasiwasi kwamba hakuwa na sifa.

Mbali ya TAKUKURU kuanza kufuatilia malalamiko hayo, kumeanza kusikika kwa taarifa zinazoeleza kuwa Mrema aliwahi kufutwa kazi na baadaye kuajiriwa tena kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Kwa mujibu wa habari hizo, Mrema alikuwa mmoja wa wahandisi wasimamizi wa ujenzi wa Barabara ya Dodoma-Manyoni mkoani, Singida kabla ya Julai 4, mwaka 2004.

Kwa mujibu wa barua kutoka katika Wizara ya Miundombinu, wakati huo ikiitwa Wizara ya Ujenzi, Mrema, aliondolewa kazini katika mradi huo na ndipo akaenda Zanzibar.

Habari hizo zinasema kuwa, barua kutoka Wizara ya Ujenzi (Miundombinu), ya Julai 4, mwaka 2003 iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wakati huo, F.C.T Kilowoko, ilionyesha kuwa, Mrema alitimuliwa kazi wakati huo.

Barua hiyo yenye kumbukumbu Na. Ref. No. AB.1337/148/02/60 kwenda Meneja Mradi wa Kampuni ya Konoike Construction, ikitakiwa aione Y. Miyazawa, ilieleza kuvunja mkataba na Mrema kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi katika ujenzi wa barabara hiyo.

Ilikuwa inafahamisha kuvunjwa kwa mkataba wa Mrema kulikuja baada ya kikao na utawala na ufundi kilichofanyika Juni 9, mwaka huo wa 2003.

Barua hiyo ambayo Tanzania Daima imeiona inaeleza kuwa, Mrema, alikuwa na mtazamo tofauti wakati wa utendaji kwani kwa nafasi yake, aliwahi kuzuia mafuta kwa ajili ya safari ya msimamizi wa mshauri wa ujenzi huo, John Leonard aliyekuwa asafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.

Barua hiyo imesema suala la utoaji wa mafuta kwa Leonard au kwa waajiriwa wengine, hususani wahandisi, limewekwa wazi katika kifungu cha 1,407 kwamba wafanyakazi wanaruhusiwa kutumia amana ya kampuni bila kipingamizi chochote. Leonard aliyekuwa anatumia gari la mradi, alisafiri Mei 29, 2003.

"Hivyo kitendo cha Mrema kupinga matumizi ya gari hili, ni kinyume na utendaji," ilisema barua hiyo ambayo nakala yake ilitumwa kwa Rais wa Konoike ambaye ofisi yake iko Tokyo, Japan.

Pia nakala ilitumwa kwa Mhandishi wa Mkoa, Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Dodoma-Manyoni.

Katika barua hiyo, wizara ilimueleza wazi meneja mradi kwamba, Mrema anafutwa kazi mara moja katika orodha ya wafanyakazi wahandisi katika mradi huo, sambamba na kufanyia kazi mapendekezo ya kumfuta kazi mara moja, ikisisitiza utekelezwaji wa jambo hilo ungekamilika mara moja.

Wiki iliyopita, Mbunge wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi (CCM), alifichua vitendo vya ufisadi na utata wa ajira ya CEO huyo bungeni.

Mporogomyi alidai bungeni kwamba, mtendaji huyo analipwa malipo makubwa tofauti na vigezo vya kazi aliyopewa, kadhalika stahili ya kiwango tofauti na utaalamu alionao.

Alisema licha ya Mrema kuwa Mtanzania, ameajiriwa kwa mkataba unaoonyesha kuwa analipwa kama mgeni, na kuligharimu taifa kiasi cha dola za Marekani takribani 24,450 kwa mwezi, sawa na sh milioni 30, mbali ya malipo mengine ambayo yametengwa nje ya pato lake rasmi la kila mwezi.

Mbali na mshahara huo, pia analipwa posho ya nyumba ya dola 2,200, posho ya pensheni dola 850, posho ya matibabu dola 400 na posho ya usafiri dola 500.

Mrema analipwa pia dola 3,000 za likizo na mkataba wake unaonyesha kuwa, alipochukua madaraka, alilipwa dola 9,000 zikiwa ni malipo ya dola 150 kwa siku kwa muda wa siku 60 za awali alipoajiriwa.

Pia analipwa dola 102,000 kama bonasi ya utendaji kila mwisho wa mwaka na dola nyingine 10,000 mwishoni mwa mkataba wake.
 
TAKUKURU yavamia TANROADS

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
July 11, 2008

Kwa mujibu wa habari hizo, kikubwa kilichokuwa kinachunguzwa ni endapo Mrema alikuwa analipa kodi kama ilivyoelezwa na jinsi alivyoingia katika ajira hiyo.

Wiki iliyopita, Mbunge wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi (CCM), alifichua vitendo vya ufisadi na utata wa ajira ya CEO huyo bungeni.

Mporogomyi alidai bungeni kwamba, mtendaji huyo analipwa malipo makubwa tofauti na vigezo vya kazi aliyopewa, kadhalika stahili ya kiwango tofauti na utaalamu alionao...


Kodi gani?

Kama ilivyoelezwa na nani?

Hiyo kodi inahusiana vipi na utata wa ajira ambayo Mbunge kaizungumzia?

Ki-stori haki make sense!
 
jamaa walikatazwa kutumia mafuta "bila kipingamizi chochote"... Watanzania hatuhitaji viongozi kama Mrema, tunahitaji watendaji wanaoacha watu waliochini yao kufanya lolote watakalo.
 
Huko tunakoenda nahisi Mrema atakuja kuonekana ni kiongozi bora kabisa,mfano mh Mporogomi alisema hana sifa kwa kuwa yeye ata barabara hajawahi kuzifanyia kazi,leo tunaambiwa kumbe amepata kuwa hadi project manager wa konoike!!!!!!!!!!!!!huu ni mchanganyo..kosa la kumfukuza kazi ni kusimamia mtazamo wake kuwa watu wasitumie mafuta vibaya...kwangu mimi hii ni credit unless mtu anipe maelezo yake kuwa alikubaliana na uamuzi huo.ata tanroads ninahisi ni chuki za kuwaminya watu ugali wao.
 
Hawa jamaa wakiona dagaa iwa wanakuwa shap sana na wanakuwa wanoko sana ila wakifika kwenye mapapa wanalowa kabisa nakuishia ooh uchunguzi unaendelea subilini tukisahau kidogo basi ndo ishu basi tena.
 
Back
Top Bottom