Vinyago: Vivutio kwa watalii au vinatudhalilisha watu weusi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vinyago: Vivutio kwa watalii au vinatudhalilisha watu weusi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Apr 14, 2009.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Vinyago vya kuchonga vimekuwapo tangu zama za historia na vimechukuliwa kama utamaduni wa nchi nyingi za Bara hili la Afrika, ikiwemo Tanzania.

  Tanzania imejijengea sifa kubwa ya kuwa na utamaduni wa vinyango vinavyochongwa na Wamakonde kutokana na mti wa mpingo (blackwood), aina ya miti ambayo hapa duniani inapatikana katika sehemu za kusini mwa Tanzania pekee.

  Vinyago hivyo -- ambavyo vingi huwa ni sura au umbile la mtu mweusi – vimetokea kuwa vivutio vikubwa kwa watalii na hivyo kuwa biashara kubwa inayoingizia taifa fedha za kigeni.

  Lakini hapa inafaa kujiuliza kidogo: Vinyago hivi hunuuliwa na hao Wazungu na kuvipeleka kwao ambako hufanywa mapambo ktk sitting room zao.

  Kwa maoni yangu, matumizi haya ya mwisho ya vitu hivyo yamekuwa yanatudhalilisha sisi watu weusi. Kuna rafiki yangu mmoja aliyewahi kuishi Denmark alinieleza kuwa watoto wanaozaliwa na kukulia ktk nyumba hizo huambiwa na wazazi wao kuwa watu weusi wameumbwa kama vilivyo vinyago hivyo.

  Aidha wageni wao wanaotembelea nyumba hizo zenye mapambo ya vinyago nao huambiwa hivyo hivyo.

  Hali hii inawafanya watu weusi daima kuwa ktk kudhalilishwa mbele ya mataifa ya Wazungu yanayoendelea, kitu ambacho daima hutuendeleza kuwa wanyonge mbele yao. Matokeo ni kwamba daima wanatudharau.

  Kwa maoni yangu nadhani biashara hii ingeanza kupigwa vita, Tanzania hapa na kwingineko Barani Afrika, potelea mbali kama inatuingizia kipato.

  Naamini kabisa ingekuwa nia wao Wazungu wasingekubali kufanyiwa kitu cha namna hii.
   
 2. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hebu tuwahamasishe hawa jamaa zetu wanaochonga vinyago waanze kuchonga vinyago vya kizungu tuone kama vitanunuliwa.
  Kwa kuanzia hapo tutaangalia kinachotoka zaidi basi tutakiondoa sokoni.
  Siwatetei wazungu la hasha! Wachongaji ni sisi sisi, tunaouza vinyago ni sisi.
  Jamani hii ni art tu wala sio kama tunavyodhania. Angalao kuna wanaoelewa kuwa Waafrika hawana mkia kama wanavyodhani.
  Kama tunataka kupandisha thamani ya bei ya vinyago basi tuvipige marufuku,,, utaona bei itakavyopaa
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Hebu tuwahamasishe hawa jamaa zetu wanaochonga vinyago waanze kuchonga vinyago vya kizungu tuone kama vitanunuliwa.
  Kwa kuanzia hapo tutaangalia kinachotoka zaidi basi tutakiondoa sokoni.
  Siwatetei wazungu la hasha! Wachongaji ni sisi sisi, tunaouza vinyago ni sisi.
  Jamani hii ni art tu wala sio kama tunavyodhania. Angalao kuna wanaoelewa kuwa Waafrika hawana mkia kama wanavyodhani.
  Kama tunataka kupandisha thamani ya bei ya vinyago basi tuvipige marufuku,,, utaona bei itakavyopaa"

  **********************

  Eeka Mangi: Kidooooogo unayo hoja ndugu yangu. Pesa mbele, na tufumbie macho udhalilishwaji. Nafikiria katika sitting room zao hizo huwa kuna vicheko vikubwa wanapokuwa wanavijadili vinyago!

  Hata hivyo, ni vigumu kupiga marufuku biashara hii, maana kosa lilishatokea tangu zama za historia, kwa nini sisi wa sasa kituume zaidi kuliko wale waliotutangulia?

  Kama biashara ya utumwa iliyotudhalilisha na hatimaye kupigwa marufuku mbona hadi leo ipo? sasa hivi tunajipeleka wenyewe kwa Wazungu katika maboti duni ambayo wengi huzama na kufa maji wakiwa katikati ya bahari.

  Afadhali akina Kunta Kinte ambao walikuwa wanaona bora kujirusha kutoka kwenye meli na kufa maji kuliko kupelekwa utumwani.
   
 4. h

  herikujua Member

  #4
  Apr 14, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nakubaliana na wewe kuwa hivi vinyago vinavyouzwa kwa watalii katika "curio shops" vinatudhalilisha.Ila inabidi tujikumbushe imekuwaje ikafikia hapo. Wanunuzi wa hivyo vinyago wanapendelea vilivyoko sokoni na hiyo imekuwa ndio chanzo cha wachongaji kuchonga aina mbali mbali za vinyago ambazo zinaonekana kudhalilisha. Nimewahi kusoma kuwa hata huu uchongaji ambao mwishowe kinyago kinakuwa na "smooth and polished surface" sio wa asili ya kiafrika na umetokana na nguvu za soko la wanunuaji.
   
 5. M

  Mundu JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu ya mafundisho ya Biblia hasa kwa wakristu, wakati wa uumbaji, Mungu alisema 'na tufanye mtu kwa mfano wetu na sura yetu' na ndipo mwanadamu wa kwanza Adam aliumbwa.

  Sasa kama kuna watu ambao wanajiona ni daraja la kwanza kwa kuwa wao ni weupe nadhani hiyo ni arrogance tu, kwa Mungu wote ni sawa. Na pia kama mtu anatumia rangi yake kukudharau, nawe ukataabika na maneno yake, nadhani tatizo haliko kwake bali lipo kwako. Jivunie hivyo ulivyo na hakuna mtu atakayetumia nafasi yake kukudharau au kudharau vitu vyako.

  Sanaa ya vinyago Afrika ilikwepo tokea miaka mingi, tena kabla wazungu hawajafika Afrika na itaendelea kuwepo. Na hii ni mojawapo ya utamaduni wa mwafrika. Sidhani kama ilikuwa rahisi kwa wakati huo kwa ndugu zetu wamakonde kutengeneza vinyago vyeupe kwa kuwa hakukuwa na wazungu wakati huo. Hivyo kwa kujitambilisha walitengeneza sanamu na vitu vinavyofanana nao. Utakuta kuna wanyama, mitumbwi, sanamu za binadamu weusi n.k. Hata Ulaya wazungu pia walitengeneza sanamu zinazofanana na asili yao.

  Hivyo sioni tatizo lolote la kuendeea kutengeneza vinyago vya kimakonde, vyeusi kama mkaa, kisa tunaogopa watu weupe watatufananisha navyo. Kwani waafrika weusi tutabaki weusi tu hata tusipotengeneza vinyago. Tuache upumbavu wa kudharau asili yetu.
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  hapa Spain kuna waahamiaji wengi tu kutoka mataifa mbalimbali,wapo ndugu zetu kutoka Africa wanatafuta pesa kwa njia ya ajabu, utakuta baadhi yao wanavaa vinyago na mask kama kima vile wanapita wakichezacheza na kurukaruka kama,nyani huku wazungu wakiwarushia kwenzi. kwa kazi hiyo tu mtu anakwambia anatengeneza euro kadhaa kwa mwezi na nyengine anapeleka nyumbani, waliniacha hoi kweli.
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  There is such a thing as being oversensitive.
   
Loading...