Vingozi wa Dini chukueni mfano wa wenzenu wa S. Africa

M_kara

JF-Expert Member
Jan 9, 2016
385
293
Katika jitihada ya kupinga wizi wa mali ya umma wazi wazi, viongozi wa kidini Afrika ya kusini wiki juzi walikuwa wakikutana na kuhamasisha umma kutoa shinikizo la kujiuzulu kwa Rais Jacob Zuma, baada ya kukutwa na mahakama ya katiba ya nchi hiyo kwa utumiaji vibaya wa madaraka na kutumia pesa za serikali katika ujenzi wa nyumba yake ya binafsi. Tanzania ya leo hali hii siyo siri tena. Kumekuwa na msululu wa matukio ya wizi wa mali ya umma katika kiwango kinacho sikitisha, na wahusika kutowajibishwa kwa maovu yao. Sasa hivi wizi wa mabilioni katika mashirika ya umma, taasisi na asasi za kiserekali ikiwemo polisi siyo kitu kigeni tena au cha kushangaza. Ni leo tu vyombo vya habari vimeripoti wizi wa trilioni (Escrow Part II) na list inaendelea on and on. Nina imani viongozi wengi wa kidini wamekuwa na mwelekeo wa kupendezwa na hatua zinazo chukuliwa na serikali ya Mh.J.P. Magufuri kuhusu kupiga vita na kuwashughulukia waharifu wa kiuchumi, lakini kwa nafasi zenu kubwa katika jamii mimi ninadhani ni vizuri kwenda an extra mile kumsaidia Rais kwa kuanzisha na kuhamasisha mijadala ya pamoja (ikiwa ni pamoja na kuandaa maandamano) kupinga ufedhuli na wizi wa mali ya umma ulio kithiri katika nchi hii. Hii nchi ni yetu wote.
 
Back
Top Bottom