VINCENT Nyerere: Waziri Nchimbi afukuzwe kazi mara moja

unaonesha ni jinsi gani unavyofurahi wanainch wanavyouwawa na hao polisi ambao wanafanya kazi za sifa kufurahisha wakubwa wao, ok mkuu nimekusoma mbuyu twite ritz

Polisi aliyemuuwa Mwangosi (R.I.P) tayari kaishafikishwa mahakamani.
 
ni aibu kwa viongozi wa nchi hii kudhani kuwa cheo ni mali binafsi. ni aibu kwa rais na serikali yake kushindwa kuwawajibisha wale wanaokwenda kinyume na utu na kusababisha athari kubwa kwa nchi. ni aibu kwa nchi hii kushindwa kuwachukulia hatua viongozi wote watendao mambo ya hovyo. hivi majuzi tu kule DRC kuna waziri aliachishwa kazi na kufunguliwa mashtaka kwa sababu ya mambomu yaliyolipuka na kuua watu kadhaa na kuharibu maliza watu.

lakini cha kushangaza, nchi hii, viongozi wetu (kwa sababu ya uroho wa madaraka na mali) hawako tayarti kuwajibika kwa uzembe wao ama wa wasaidizi wao! na serikali ipo kimya! wananchi nao wamelala usingizi wa pono! mataifa ya nje yanatushangaa. yanatuona tu mazuzu!
 
Kauzu zaidi ya dagaa kwa kweli unaweza kuniambia viongozi wako walienda Ikulu kuongea nini cha maana zaidi ya kunywa juice na kashata...unacheza na JK wewe.

Lakini dhaifu alikubaliana na hoja za Chadema isipokuwa kwa udhaifu wake akasema wenzake hawatamuelewa.
 
Lakini dhaifu alikubaliana na hoja za Chadema isipokuwa kwa udhaifu wake akasema wenzake hawatamuelewa.

Kesho yake Mnyika akaanza kulia lia kwa waandishi wa habari eti hawakukubaliana hivyo...JK kawachuuza viongozi wako yote waliyosema kayapuuza, kaenda kuwapa kazi kina Jaji Warioba...hatimaye Mtei, analalamika ovyo na udini.
 
Naomba Wanasheria wa hapa JF mnisaidie, leo jioni nilikuwa nasikiliza BBC Swahili kuna wana harakati wa Mazingira wa Nigeria wamefunguwa kesi The Hugue Uholanzi kutaka walipwe fidia kutokana na uchafuzi wa mazingira uliofanywa na kampuni ya Shellys kule Niger Delta.

Sasa swali langu kwani Serikali hii haiwezi kufunguliwa mashtaka kwenye Mahakama za kimataifa? haya matamko kwangu sasa hivi naona ni useless tu.

Nimeona Mtikila akizitumia Mahakama kama ya Afrika sasa sisi tunashindwa vipi kuistaki hii Serikali moja kwa moja The Hugue?

Wale wanaharakati wenye kupewa hela na wafadhili huu ndo wakati wao wa kuzitumia hizo hela kuwatetea wanachi wanyonge badala ya kugawana posho na kuishia kutoa matamko kila siku. ujumbe huu umfikie Mama Bisimba na wanaharakati wenzie
 
Mh. Vincent Nyerere asante kwa mada nzuri hii but I assure you Mh. Nchimbi ni mtu wa karibu sana na JK. Hata aharibu kiasi gani hawezi kumwondoa!!! Atakuwa Waziri hadi 2015!!! Kazi aliyoifanya kumwandalia jamaa njia 2005 kupitia UVCCM lazima fadhila yake iendelee kulipwa. Take my words!!
Hii ni kesi ya ngedere iliyopelekwa kwa nyani wakubwa! Ametumwa, katekeleza maagizo ya mkubwa, sasa kwa nini asilindwe?. Huyu atakuwa mmoja wa wagombea urais 2o15!
 
Anyongwe mara moja
Katimiza maagizo ya chama chake ili kibaki madarakani, nani ataamuru anyongwe shujaa wao? kuua mtu hadharani namna ile na kutoa ripoti inayotetea wauaji "kwa maslahi ya chama kunampa nguvu ya kuwa shujaa wa chama kama mafisadi wengine wakubwa!"
 
Nchimbi kwa muonekano wa muendelezo wa wachangiaji,na kwa kuwa upo humu unasoma haya,basi jiondoe tu kaka katika nafasi ili kutunza ka Heshma ka Wangoni wote,najua inauma ila jikaze baba
 
Ni kwel mh. mb,huyu nchimbi inabidi afukuzwe kazi haiwezekani aunde tume ya uchunguzi kwa ajili ya kudanganya umma kwa malengo ya kulisafisha jesh la polisi,umma unaelewa wazi kabisa yale mauaji yaliratibiwa na yalikuwa ni ya kisiasa zaidi.kama mambo yako mahakamani kwa nini tume iliundwa?.kwa hiyo nasema serikali isitake kutufanya wananchi kama watu wapumbavu wasio elewa kitu,na inabidi iwe makin sana na inachokifanya.lakin sitashangaa kuona mh rahis kuto muwajibisha waziri nchimbi,hii inatokana na kuwa analipa fadhila kwa kile alichofanyiwa kipindi cha kampen 2005,usitegemee chochote kutokea.ni hayo tu yangu!
 
Chama lege kinaongozwa na mwenyekiti bwabwa.na serikali lege inaongozwa na rais lege anaeteuwa viongozi lege
 
Inachekesha sana kwa hiyo mtaendelea kuomba kwa JK mpaka lini?

Kwanza tambua kitu kimoja...................... Jk haombwi na chadema kutekeleza majukumu yake, bali kutokana na udhaifu wake wa kutokutunza kumbukumbu, chadema wanachofanya ni kumkumbusha kufanya majukumu yake!

Tutaacha kumkumbusha atakapotukabidhi Nchi yetu!
 
Kikwete hawezi kumfukuza Nchimbi, nia anayo sababu anayo na uwezo anao. Namchukia Rais, naichukia CCM, Nachukia uozo uliopo, na kura yangu haitapotea, nitakuja nyumbani kuitetea haki yangu KWA GHARAMA ZOZOTE.
 
Nyie mnasema kila siku humu JF ni JK ni dhaifu sasa mnamuomba tena amfukuze Nchimbi.

Kuwa dhaifu akumaanishi kuwa aachwe afanye atakavyo..lazima aendeshe nchi kama sisi wenye nchi tunavyotaka.
 
ED....DHAIFU hajawahi kumfukuza yoyote kazi tangu aingie madarakani miaka 7 iliyopita na kwa UDHAIFU wake hakuna dalili za kumfukuza kazi Nchimbi. Kama siyo Wabunge kumshinikiza kuhusu akina Mkullo, Ngeleja etc hadi hii leo wangekuwa wanapeta kama Mawaziri....Dr Slaa hakukosea pale aliposema, "Kumchagua Kikwete katika uchaguzi wa 2010 ni janga la Taifa."

Nani atamfukuza? aliyeshindwa hata kutoa kauli juu ya mauaji ya Mwangosi?
 
Atolewe mara moja maana hio kazi hakuiomba aliwekwa tu, ingekuwa ameiomba angekuwa anaiweza vizuri
 
Back
Top Bottom