VINCENT Nyerere: Waziri Nchimbi afukuzwe kazi mara moja

Huwa napata kichefuchefu pale ninaposikia ama kusoma ya kuwa hata Mh. Nchimbi ni mmoja wapo wa wanaowania uraisi wa nchi hii. Hivi kweli kwa kufanya madudu yasiyovumilika na kutetea udhalimu kupitia dhamana (waziri) aliyonayo sasa, Je akipata uraisi si ndiyo itakuwa hali mbaya zaidi? Nawaza kwa kelele huku nikiogopa sana.
 
Kuna Agenda ya siri inaendelea humu JF, but war against crusaders will never succeed.

Baba nilimjibu Ritz nikala Ban ile ID nyingine ! Serikalini hakuna mwenye akili! Huwa siamini mtu Kama nchimbi AMA Yule Vuani nahodha ni mawaziri! Joel Bendera
mkuu wa mkoa na Ihema ni jaji lol! Mkwe re rais
 
hivi hawa CHADEMA siwalitoka nje wakasema hawamtambui jk sasa leo wanamuomba amuwajibishe nchimbi, siasa bhana! wajinga ndio waliwao
 
Kwa wayahudi Yesu alisema, "Baba uwasamehe kwa kuwa hawajui watendalo." Ingekuwa ni kina Nchimbi ndio wanamtesa angeweza kulia, "Baba uwaangamize watu hawa kwa kuwa wanajua walitendalo.",
 
Nani atamfukuza? aliyeshindwa hata kutoa kauli juu ya mauaji ya Mwangosi?
Ni kweli unachosema. Kwa jinsi Kamati ya Nchimbi ilivyotoa taarifa ile ambayo sisiti kuita ni rubbish! kwa kweli sasa wa-TZ. tutaanza kuunga mkono kauli aliyotoa mbunge wa Ubungo, John Mnyika, kuwa Rais wetu ni Dhaifu mno, na sasa tunabidi pia tutangaze pia kuwa JK kwa sasa ni janga la Kitaifa. Kwa kuwa kwa vyovyote vile, hii taarifa ya Jaji Ihema upo uwezekano mkubwa kuwa wakati inaandikwa, Jaji Ihema alikuwa akisaidiana kuandika na Salva Rweyemamu, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu. Kwa kuwa tumeona tofauti kubwa ya umbali wa Duniani na Mbinguni, kati ya taarifa takataka ya Jaji,Ihema, ambaye Tundu Lissu alishawahi kutamka hadharani kuwa ni Jaji feki, na ripoti iliyoenda shule, ambayo mara kadhaa imequate Ibara na vifungu vya sheria kama ambavyo wanavyotakiwa wanasheria wa ukweli, kama alivyofanya Jaji wetu shujaa, Amir Manento, wa Tume za haki za binadamu, ambaye hakutaka kuleta unafiki, na akaeleza bayana kabisa kuwa waloisababisha mauaji yale kwa kiasi kikubwa, ukimwacha yule koplo waliomtoa kafara, ni RPC Kamuhanda na kibaraka mkubwa wa CCM, Msajili wa vyama John Tendwa!!
 
hivi hawa CHADEMA siwalitoka nje wakasema hawamtambui jk sasa leo wanamuomba amuwajibishe nchimbi, siasa bhana! wajinga ndio waliwao
Wewe lazima utamke hayo maneno, maana hata avatar yako inajieleza bila shaka yoyote kuwa wewe ni 'propagandist' kama wewe haumo kwenye payroll ya Nape, basi utakuwa unashare ofisi na yule jamaa anayeitwa Zoka wa UWT!!!
 
Wakati nyie mnalalama kila kukicha, jamaa saa hizi yuko pale magogoni anapanga ziara zake za nje ya nchi.

Kusema Nchimbi afukuzwe kazi na jk ni sawa na kesi ya nyani kupelekwa kwa ngedere.
 
hivi kipindi kile CUF walivyokua chama kikuu cha upinzani, walikua wanasema haya?
 
Mh. Vincent Nyerere asante kwa mada nzuri hii but I assure you Mh. Nchimbi ni mtu wa karibu sana na JK. Hata aharibu kiasi gani hawezi kumwondoa!!! Atakuwa Waziri hadi 2015!!! Kazi aliyoifanya kumwandalia jamaa njia 2005 kupitia UVCCM lazima fadhila yake iendelee kulipwa. Take my words!!

Ukaribu wa jk na watu wake unawafanya watanzania wateseke sana kwakuwa urafiki wao unatumika vibaya. Mfano wafanyakazi wa UDOM tulivuonyang'anywa, na kuporokrwa haki zetu ikiwemo arreas inayotokana na promotions na annual increment zetu
 
Hivi hakuna wa kumtandika risasi huyu Nchimbi? Hizi dharau sasa!
Mimi nadhani jambo pekee lililobaki nchi hii ni kuendesha maandamano ya nchi nzima, ili kushinikiza hawa watu design ya Nchimbi, Mwema, Kamuhanda,Chagonja,Shilogile na huyu kibaraka mkubwa wa CCM anayejiita msajili wa vyama,Tendwa walazimishwe kujiuzuru!! Bila hivyo hakuna litakalofanyika, na huyo kiongozi dhaifu anaeleweka strategy yake kubwa hivi sasa, ni kutegemea vyombo vya dola vikiwezeshe chama chake cha magamba kiendelee kukaa madarakani, kwa gharama yoyote, hata kama ni kwa raia wasio na hatia kupoteza maisha. Kwa kweli inatia hasira sana kwa Serikali hii kuamua kuwakingia kifua wahalifu wote wakubwa, ili mradi tu, uhalifu huo wataufanya kwa ajili ya kuwalinda watawala. Hivi sasa ndiyo tutaanza kuelewa, Kamuhanda alikuwa anamaanisha nini siku ile alipouawa Mwangosi, alipotamka kuwa anaogopa kopoteza kazi na angependa astaafu vizuri!!!
 
Ule mtandao woote uliompa kichapo Mwangosi unatakiwa kukamatwa sambamba na Nchimbi na kufungwa Maisha
 

KAULI YA AWALI YA VINCENT NYERERE (MB) WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI KUHUSU RIPOTI YA UCHUNGUZI WA MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN, DAUDI MWANGOSI



SERIKALI kupitia Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Emmanuel Nchimbi, na kutoa taarifa yake tarehe 9, Oktoba 2012, imetoa hadharani kwa umma kile ilichoita kuwa ni Ripoti ya Uchunguzi wa kifo cha Mwandishi wa Habari wa Channel Ten, Bw. Daudi Mwangosi ambayo imelenga kulisafisha Jeshi la Polisi.

Licha ya Ripoti hiyo kuacha maswali mengi yasiyokuwa na majibu hasa juu ya uwezo na umakini wa serikali hii ya CCM kupitia Waziri Nchimbi, ni kwamba waziri pia ameshindwa kuthamini na kusimamia haki ya kuishi kwa mujibu wa katiba ya nchi na ni ushahidi wa matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.

Moja ya sababu kubwa inayonifanya nifikie hitimisho hilo ni kitendo cha Waziri Nchimbi kupokea ripoti hiyo mbovu, kuikubali, na kuitetea huku akijua kuwa polisi walihusika na mauaji hayo na hivyo ameamua kuwalinda kwa udhalimu waliofanya kwa kisingizio cha suala kuwa mahakamani.

Wizara ya Mambo ya Ndani ingeweza kabisa kutoa ripoti yote hadharani bila kuingilia kesi iliyoko mahakamani kwa kuwa taarifa hiyo haielekezi mahakama itoe hukumu gani bali ilipaswa kueleza matokeo ya uchunguzi wa chanzo cha mauaji ya kinyama na masuala mengine ya ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria uliofanyika.

Kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani nilitarajia ripoti hiyo ianike namna Jeshi la Polisi lilivyoingiliwa na viongozi waandamizi wa serikali na kutumiwa kisiasa kufanya operesheni zenye kuvunja sheria ya vyama vya siasa na kuweka bayana chanzo cha polisi kuamua kufanya mauaji ya kinyama ya mwanahabari Daud Mwagosi.

Aidha, ripoti hiyo imeshindwa kueleza ukweli kuhusu matendo ya uvunjaji wa sheria yaliyofanywa na Kamanda wa Polisi Mkoa Iringa Michael Kamuhanda kutoa agizo kinyume cha sheria kusitisha shughuli halali za CHADEMA bila kuzingatia matakwa ya sheria ya vyama vya siasa.

Kwa upande mwingine ripoti imekwepa kueleza ukweli kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa kukiuka masharti ya sheria ya sensa, masuala ambayo ndiyo yaliyosababisha polisi kupewa amri ya kufanya operesheni iliyopelekea mauaji ya Mwanahabari Daud Mwangosi, kujeruhi raia wengine wasio na hatia na kusababisha uharibifu wa mali.

Kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani nilitarajia kwamba pamoja na kueleza kwa ukweli chanzo cha mauaji, ripoti hiyo ingetoa mapendekezo ya wazi ya hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wote waliovunja sheria na kusababisha mauaji na kuwajibishwa kwa mtandao mzima uliohusika na operesheni hizo zilizovunja haki za binadamu za kuishi na kujumuika pamoja na kukiuka misingi ya utawala bora bila kujali vyeo vyao katika Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na Jeshi la Polisi.

Kutokana na Waziri kuonekana wazi kuwalinda na kuwatetea waliohusika na mauaji nalazimika kuamini kwamba Serikali haina nia ya dhati ya kupiga vita vitendo viovu vinavyofanywa na Jeshi la polisi dhidi ya raia hali ambayo inatoa picha kwamba vitendo hivyo vimesababishwa na maagizo kutoka kwa viongozi wengine waandamizi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.

Itakumbukwa kwamba wakati nikiwasilisha Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Mambo ya Ndani katika mkutano wa nane wa Bunge mwaka huu, katika bunge la bajeti mwaka huu nilizuiliwa kusoma kipengele cha MAUAJI YA RAIA YENYE SURA YA KISIASA kwa kisingizio cha masuala kuwa mahakamani, hivyo bunge lilikoseshwa fursa ya kuisimamia serikali kuepusha hali hiyo kuendelea.

Matokeo yake ni Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kutokuwajibika na hatimaye kusababisha mauaji mengine yenye sura ya kisiasa katika Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Iringa mara baada ya mkutano huo wa Bunge.

Katika muktadha huo, kutokana na kukithiri kwa matukio haya ya kigaidi ya kuteka, kutesa, na kuua raia wasio na hatia hapa nchini, na kutokana na kuundwa kwa kamati mbalimbali za uchunguzi na Wizara ya Mambo ya Ndani au na Jeshi la Polisi ambazo matokeo yake hayafanyiwi kazi au kamati hizo kutoa ripoti zenye kuficha ukweli; kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani;

Mosi; natoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani Dr Emmauel Nchimbi kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuruhusu ufujaji wa fedha za umma kufanya uchunguzi usiokidhi mahitaji na wenye kuficha ukweli na kulisafisha jeshi la polisi dhidi ya tuhuma za mauaji pamoja na kukwepa kueleza uvunjaji wa Sheria uliofanywa na Kamanda wa Polisi Michael Kamuhanda, Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa na wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kuvunja sheria, kusababisha mauaji na kukiuka haki za msingi za kikatiba.

Aidha, Rais Kikwete aagize hatua za kisheria kuchukuliwa kwa mtandao mzima ulioshiriki katika kumpiga na hatimaye kusababisha mauaji ya Daudi Mwangosi.

Pili; kutokana tatizo hili la mauaji yenye sura ya kisiasa kuendelezwa bila Serikali kuonesha kukerwa nalo na kuchukua hatua madhubuti za kukomesa ugaidi huu; nitapeleka ripoti zote tatu za uchunguzi wa kifo cha Mwangosi, yaani Kamati ya iliyoundwa na Waziri Nchimbi, Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Tume ya Haki za Binadamu kwa Baraza Kivuli la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuzijadili na kufanya maamuzi kwa ajili ya hatua za ziada za kibunge kuchukuliwa.

Imetolewa tarehe 11 Oktoba 2012 na:

Vicent Nyerere (Mb)
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani




Mh. Vicent,
Nimefika mahali pa kuona haya matamko yanayotolewa kila siku kama ni mchezo ule ule wa serikali yetu kuunda kamati na kuja na ripoti za kijinga. Matamko haya nina hakika hayataheshimiwa na rahisi (rais) wa nchi hii na wala hakuna hata mtu mmoja atakayewajibishwa akijua wazi hakuna litakalotokea.
Nina hasira sana na viongozi wa nchi hii kwa kuua watu bila kujali na hakuna hatua inayochukuliwa. Kesho yaweza kuwa wewe au mie au wanangu au ndugu zangu, na watabaki wakitabasamu mbele za luninga huku wakiwa na matamko kama yako.
Naomba siku nyingine mkija na matamko mseme kabisa hatua ambazo mnadhani zitatumika au kuwalazimisha wachukue hatua wasipochukua au namna tunavyoweza kuwaadhibu sie wenyewe wananchi wote wanaohusika na mauaji maana uwezo upo (Msije na hoja za sanduku la kura).
Lakini haya matamko useless hatuyataki tena. Hayana maana si kwetu bali hata kwa familia za wanaouliwa.
Nakumbuka CUF walikuwa na kamtindo aka ka matamko mpaka walipojikuta wameolewa na bwana wao. Sie hatutaki kuyasikia maana yametosha. Tunahitaji hatua zichukuliwe hata kama kiongozi atakuwa kastaafu ashughulikiwe na wananchi wapenda amani kwa namna watakavyoona inafaa. Inawezekana na yaweza kuwa fundisho.
Tumeona nchi zingine ikifanya kazi.
 
Back
Top Bottom