VINCENT Nyerere: Waziri Nchimbi afukuzwe kazi mara moja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VINCENT Nyerere: Waziri Nchimbi afukuzwe kazi mara moja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Oct 11, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180

  [FONT=&amp]KAULI YA AWALI YA VINCENT NYERERE (MB) WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI KUHUSU RIPOTI YA UCHUNGUZI WA MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN, DAUDI MWANGOSI[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]SERIKALI kupitia Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt Emmanuel Nchimbi, na kutoa taarifa yake tarehe 9, Oktoba 2012, imetoa hadharani kwa umma kile ilichoita kuwa ni Ripoti ya Uchunguzi wa kifo cha Mwandishi wa Habari wa Channel Ten, Bw. Daudi Mwangosi ambayo imelenga kulisafisha Jeshi la Polisi.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Licha ya Ripoti hiyo kuacha maswali mengi yasiyokuwa na majibu hasa juu ya uwezo na umakini wa serikali hii ya CCM kupitia Waziri Nchimbi, ni kwamba waziri pia ameshindwa kuthamini na kusimamia haki ya kuishi kwa mujibu wa katiba ya nchi na ni ushahidi wa matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.
  [/FONT] [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Moja ya sababu kubwa inayonifanya nifikie hitimisho hilo ni kitendo cha Waziri Nchimbi kupokea ripoti hiyo mbovu, kuikubali, na kuitetea huku akijua kuwa polisi walihusika na mauaji hayo na hivyo ameamua kuwalinda kwa udhalimu waliofanya kwa kisingizio cha suala kuwa mahakamani. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Wizara ya Mambo ya Ndani ingeweza kabisa kutoa ripoti yote hadharani bila kuingilia kesi iliyoko mahakamani kwa kuwa taarifa hiyo haielekezi mahakama itoe hukumu gani bali ilipaswa kueleza matokeo ya uchunguzi wa chanzo cha mauaji ya kinyama na masuala mengine ya ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria uliofanyika.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani nilitarajia ripoti hiyo ianike namna Jeshi la Polisi lilivyoingiliwa na viongozi waandamizi wa serikali na kutumiwa kisiasa kufanya operesheni zenye kuvunja sheria ya vyama vya siasa na kuweka bayana chanzo cha polisi kuamua kufanya mauaji ya kinyama ya mwanahabari Daud Mwagosi.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Aidha, ripoti hiyo imeshindwa kueleza ukweli kuhusu matendo ya uvunjaji wa sheria yaliyofanywa na Kamanda wa Polisi Mkoa Iringa Michael Kamuhanda kutoa agizo kinyume cha sheria kusitisha shughuli halali za CHADEMA bila kuzingatia matakwa ya sheria ya vyama vya siasa. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Kwa upande mwingine ripoti imekwepa kueleza ukweli kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa kukiuka masharti ya sheria ya sensa, masuala ambayo ndiyo yaliyosababisha polisi kupewa amri ya kufanya operesheni iliyopelekea mauaji ya Mwanahabari Daud Mwangosi, kujeruhi raia wengine wasio na hatia na kusababisha uharibifu wa mali.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani nilitarajia kwamba pamoja na kueleza kwa ukweli chanzo cha mauaji, ripoti hiyo ingetoa mapendekezo ya wazi ya hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wote waliovunja sheria na kusababisha mauaji na kuwajibishwa kwa mtandao mzima uliohusika na operesheni hizo zilizovunja haki za binadamu za kuishi na kujumuika pamoja na kukiuka misingi ya utawala bora bila kujali vyeo vyao katika Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na Jeshi la Polisi.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Kutokana na Waziri kuonekana wazi kuwalinda na kuwatetea waliohusika na mauaji nalazimika kuamini kwamba Serikali haina nia ya dhati ya kupiga vita vitendo viovu vinavyofanywa na Jeshi la polisi dhidi ya raia hali ambayo inatoa picha kwamba vitendo hivyo vimesababishwa na maagizo kutoka kwa viongozi wengine waandamizi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Itakumbukwa kwamba wakati nikiwasilisha Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Mambo ya Ndani katika mkutano wa nane wa Bunge mwaka huu, katika bunge la bajeti mwaka huu nilizuiliwa kusoma kipengele cha MAUAJI YA RAIA YENYE SURA YA KISIASA kwa kisingizio cha masuala kuwa mahakamani, hivyo bunge lilikoseshwa fursa ya kuisimamia serikali kuepusha hali hiyo kuendelea.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Matokeo yake ni Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kutokuwajibika na hatimaye kusababisha mauaji mengine yenye sura ya kisiasa katika Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Iringa mara baada ya mkutano huo wa Bunge. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Katika muktadha huo, kutokana na kukithiri kwa matukio haya ya kigaidi ya kuteka, kutesa, na kuua raia wasio na hatia hapa nchini, na kutokana na kuundwa kwa kamati mbalimbali za uchunguzi na Wizara ya Mambo ya Ndani au na Jeshi la Polisi ambazo matokeo yake hayafanyiwi kazi au kamati hizo kutoa ripoti zenye kuficha ukweli; kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani;[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Mosi; natoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Ndani Dr Emmauel Nchimbi kwa matumizi mabaya ya madaraka kwa kuruhusu ufujaji wa fedha za umma kufanya uchunguzi usiokidhi mahitaji na wenye kuficha ukweli na kulisafisha jeshi la polisi dhidi ya tuhuma za mauaji pamoja na kukwepa kueleza uvunjaji wa Sheria uliofanywa na Kamanda wa Polisi Michael Kamuhanda, Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa na wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kuvunja sheria, kusababisha mauaji na kukiuka haki za msingi za kikatiba. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Aidha, Rais Kikwete aagize hatua za kisheria kuchukuliwa kwa mtandao mzima ulioshiriki katika kumpiga na hatimaye kusababisha mauaji ya Daudi Mwangosi.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT] [FONT=&amp]Pili; kutokana tatizo hili la mauaji yenye sura ya kisiasa kuendelezwa bila Serikali kuonesha kukerwa nalo na kuchukua hatua madhubuti za kukomesa ugaidi huu; nitapeleka ripoti zote tatu za uchunguzi wa kifo cha Mwangosi, yaani Kamati ya iliyoundwa na Waziri Nchimbi, Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Tume ya Haki za Binadamu kwa Baraza Kivuli la Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuzijadili na kufanya maamuzi kwa ajili ya hatua za ziada za kibunge kuchukuliwa. [/FONT]

  [FONT=&amp]Imetolewa tarehe 11 Oktoba 2012 na:[/FONT]

  [FONT=&amp]Vicent Nyerere (Mb)[/FONT]
  [FONT=&amp]Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani[/FONT]   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kwako mhe. mbunge,
  umefika mahala sasa matamko pekee hayatoshi tunazo sababu za msingi ikiwemo matumizi mabaya ya pesa za wananchi. kwahiyo kwa kuwa aliombwa kuvunja kamati na wananchi kwa sababu za msingi na yeye kukataa na kusababisha upotevu mkubwa wa kodi za wananchi kufikia conclusion ambayo watanzania asilimia kubwa walishaiona bila hata kuundwa kwa kamati ile basi tuna kila sababu za kuandamana kumwambia ajiuzuru mara moja kwa matumizi mabaya ya kodi za wananchi kwani hii ni sawasawa na hujuma dhidi ya nchi.

  Panga siku ya maandamano tuingie uwanjani ningependekeza jumamosi hii inayokuja tunafanya hili kupeleka ujumbe kwa viongozi wengine kama yeye kuwa wananchi sasa hatutokubali kuburuzwa na viongozi uchwara wanaojiona wana akili kuliko wananchi wa kawaida
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nadhani si kufukuzwa tu, huyu jamaa anapaswa kuadibishwa.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  na kama asipofukuzwa kazi itakuwaje?
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nchimbi auwawe very simple!
   
 6. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Chadema nimewakubali Hawakurupuki,Ripoti ya Nchimbi kwa kweli nimeipokea kwa masikitiko sana,kwa kweli angalau sasa narudisha matumaini kuwa nilikuwa nawaza mawazo sahihi
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  kama kawaida yao watasema ni dua la kuku hilo. Hata hivyo hiyo kamati haikuwa na baraka zozote toka popote, na ndio maana wakaona waje na lolote. Ngoja tusubiri Tume sasa.
   
 8. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145

  Naunga mkono hoja
   
 9. p

  politiki JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wanasheria wake wizarani walimkatalia kuunda kamati walimwambia hakuna haja ya kuunda tume kwani swala liko mahakamani atakuwa anaingilia uhuru wa mahakama lakini yeye kwa jeuri yake akaamua kuunda kamati kushindana na chadema waliomwambia hana nguvu ya kisheria ya kuunda tume. leo hii amefikia conclusion ileile aliyoambiwa atafikia kuwa ataingilia uhuru wa mahakama ni lazima ajiuzuru kwa matumizi mabaya ya kodi za wananchi.
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mchungaji keshakula Ban! Nchi hii aibu
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mh. Vincent Nyerere asante kwa mada nzuri hii but I assure you Mh. Nchimbi ni mtu wa karibu sana na JK. Hata aharibu kiasi gani hawezi kumwondoa!!! Atakuwa Waziri hadi 2015!!! Kazi aliyoifanya kumwandalia jamaa njia 2005 kupitia UVCCM lazima fadhila yake iendelee kulipwa. Take my words!!
   
 12. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145

  Sio aibu peke ake Wozoza ......yaani ukiifikiria sana hii nchi unaweza kupata wazimu asee......mambo magumu viongozi wanayafanya kuwa marahisi......kama hili la Daudi (RIP).....yaani hawana hata aibu jamani..........hivi wanafikiri watatutaala milele?

  Mchungaji kafanyaje tena jamani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Nani atamfukuza? aliyeshindwa hata kutoa kauli juu ya mauaji ya Mwangosi?
   
 14. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni upepo tu na hasira za kisiasa yatapita! Tusonge mbele...!
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  Naomba Wanasheria wa hapa JF mnisaidie, leo jioni nilikuwa nasikiliza BBC Swahili kuna wana harakati wa Mazingira wa Nigeria wamefunguwa kesi The Hugue Uholanzi kutaka walipwe fidia kutokana na uchafuzi wa mazingira uliofanywa na kampuni ya Shellys kule Niger Delta.

  Sasa swali langu kwani Serikali hii haiwezi kufunguliwa mashtaka kwenye Mahakama za kimataifa? haya matamko kwangu sasa hivi naona ni useless tu.

  Nimeona Mtikila akizitumia Mahakama kama ya Afrika sasa sisi tunashindwa vipi kuistaki hii Serikali moja kwa moja The Hugue?
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Anyongwe mara moja
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  Kuna Agenda ya siri inaendelea humu JF, but war against crusaders will never succeed.
   
 18. Mentee

  Mentee Senior Member

  #18
  Oct 11, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
   
 19. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchimbi ni Muuaji na gaidi, anabariki ugaidi wa polisi
   
 20. Fyong'oxi

  Fyong'oxi JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sauti ya wengi ni sauti ya mungu, ipo siku zitawarudia damu za raia wema walizojipaka kwa kutumia mamlaka yao!
   
Loading...