Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
Chadema. Kama kuna fumbo Mungu ameweka juu yenu ni juu ya familia ya Nyerere. Haya ni maoni yangu binafsi. Yanaweza kupuuzwa ama kuungwa mkono. Sitajali. Ila nitasimama katika maono yangu.
Ndoto ya Baba wa Taifa ilikuwa ni kuona Tanzania inaendelea kuwa nchi ya amani na utulivu(dhana ambazo zinahubiriwa kinafiki na CCM ya leo). Nyerere hatunaye. Ametangulia kwenye haki.
Watoto wake warithi nini?
Nyerere hakuwa mwizi. Kwa hiyo watoto wake hawawezi kuwa wezi.
Nyerere hakuwa mtu wa viduku. Kwa hiyo watoto wake hawawezi kuwa watu wa kuandikwa kwenye magazeti ya udaku na kupigwa picha za kuweka kwenye blog za michuzi anayepigwa picha akibeba kinyago cha uume.
Nyerere alikuwa mtu wa watu. Watoto wake wanajaribu kukimbilia kwenye kundi (japo dogo) la watu wanaohubiri mageuzi na usawa katika jamii. Alianza Makongoro na NCCR. Mrema akamuangusha. Mrema akawa mnafiki asiye na msimamo anayefarakana na kila chama anachokuwa yupo. Lyatonga kafulia. Huyo tumuache.
Chadema.
Mungu amegeuza macho kwenu. Amewapa Vincent.
Jiulizeni.
Mwaka 2005, Chadema haikuwa na diwani jimbo la Musoma mjini. Leo ina madiwani 8 (usisahau uchakachuaji wa CCM). Damu ya Nyerere. Halmashauri ya Mji wa Musoma iko chini ya Chadema. Chini ya Nyerere.
Chadema musione kitu hiki kuwa kidogo. Na wala musione kuwa cha kawaida. Ni baraka za Mungu Chadema kuhusishwa na familia ya Nyerere, na popote pale walipo, CCM inawauma sana.
Mtembeleeni Maria (Mrs. Nyerere). Hebu muulizeni mzee alikuwa akisema nini kuhusu Tanzania ya leo walipokuwa wamelala kitandani. Atawaambia mengi yatakayosaidia kuturudisha Watanzania kwenye njia sahihi.
Nina amini kama Maria angeona tatizo, asingekubali Vincent na Leticia kugombea uongozi kupitia Chadema.
Kuna kitu Maria anacho. Mfuateni.
Namaliza kwa kusema: Ahsante Mungu kwa familia ya muasisi wa Taifa hili.
Chadema mumepewa Fumbo.
Epukeni ushetani uliokisambaratisha NCCR cha Mrema na kumuacha Makongoro akionekana mtu wa kawaida katika jamii, wakati damu yake ni lulu....damu ya Julius Kambarage Nyerere.