Vincent Nyerere... Leticia Nyerere... Fumbo kwa CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vincent Nyerere... Leticia Nyerere... Fumbo kwa CHADEMA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Nov 4, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Chadema. Kama kuna fumbo Mungu ameweka juu yenu ni juu ya familia ya Nyerere. Haya ni maoni yangu binafsi. Yanaweza kupuuzwa ama kuungwa mkono. Sitajali. Ila nitasimama katika maono yangu.

  Ndoto ya Baba wa Taifa ilikuwa ni kuona Tanzania inaendelea kuwa nchi ya amani na utulivu(dhana ambazo zinahubiriwa kinafiki na CCM ya leo). Nyerere hatunaye. Ametangulia kwenye haki.

  Watoto wake warithi nini?

  Nyerere hakuwa mwizi. Kwa hiyo watoto wake hawawezi kuwa wezi.

  Nyerere hakuwa mtu wa viduku. Kwa hiyo watoto wake hawawezi kuwa watu wa kuandikwa kwenye magazeti ya udaku na kupigwa picha za kuweka kwenye blog za michuzi anayepigwa picha akibeba kinyago cha uume.

  Nyerere alikuwa mtu wa watu. Watoto wake wanajaribu kukimbilia kwenye kundi (japo dogo) la watu wanaohubiri mageuzi na usawa katika jamii. Alianza Makongoro na NCCR. Mrema akamuangusha. Mrema akawa mnafiki asiye na msimamo anayefarakana na kila chama anachokuwa yupo. Lyatonga kafulia. Huyo tumuache.

  Chadema.

  Mungu amegeuza macho kwenu. Amewapa Vincent.

  Jiulizeni.

  Mwaka 2005, Chadema haikuwa na diwani jimbo la Musoma mjini. Leo ina madiwani 8 (usisahau uchakachuaji wa CCM). Damu ya Nyerere. Halmashauri ya Mji wa Musoma iko chini ya Chadema. Chini ya Nyerere.

  Chadema musione kitu hiki kuwa kidogo. Na wala musione kuwa cha kawaida. Ni baraka za Mungu Chadema kuhusishwa na familia ya Nyerere, na popote pale walipo, CCM inawauma sana.

  Mtembeleeni Maria (Mrs. Nyerere). Hebu muulizeni mzee alikuwa akisema nini kuhusu Tanzania ya leo walipokuwa wamelala kitandani. Atawaambia mengi yatakayosaidia kuturudisha Watanzania kwenye njia sahihi.

  Nina amini kama Maria angeona tatizo, asingekubali Vincent na Leticia kugombea uongozi kupitia Chadema.

  Kuna kitu Maria anacho. Mfuateni.

  Namaliza kwa kusema: Ahsante Mungu kwa familia ya muasisi wa Taifa hili.

  Chadema mumepewa Fumbo.

  Epukeni ushetani uliokisambaratisha NCCR cha Mrema na kumuacha Makongoro akionekana mtu wa kawaida katika jamii, wakati damu yake ni lulu....damu ya Julius Kambarage Nyerere.
   
 2. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Well said Ng'wanangwa
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Good wishes!
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Good advice
   
 5. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kweli huo na uchambuzi yakinifu,pongezi mkuu.Kupitia chadema tutazifikia ndoto za watanzania
   
 6. W

  We can JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  I agree
   
 7. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,683
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Waende wakampe kadi ya uanachama mama Maria na Makongoro maana wao bado ni Vijani:israel:
   
 8. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  naked truth!!
   
 9. Nkoboiboi

  Nkoboiboi JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama mtu aliwahi kunigusa ni Ng'wanagwa

  Ndani ya CHADEMA kuna mbegu ya "aradali" Mama Maria anajua; ila huyo ni mzazi (1st : !st Lady ever)

  CHADEMA tumwendee atuambie siri ya Malaika Gabriel kwa Tanzania

  Bravo Ng'wa.....
   
 10. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Naunga mkono hoja
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Safi imetulia
   
 12. doup

  doup JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  nimeipenda sana!
   
 13. h

  hebronipyana JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 261
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Imesimama.
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Napinga hoja kwa sabau siamini kama kuna kitu kama damu lulu. Kama hawa wamechaguliwa kutokana na jina lao na si uwezo wao basi nchi hii imekwisha. Ni huku kusujudia watu kwa sababu ya uzawa wao unachangia kwa kiasi kikubwa kutufikisha hapa ambapo wakina na January nao wanaona wana damu ya lulu! Mama Maria alikuwa mke wa Mwalimu na si zaidi ya hapo. Kumgeuza leo oracle ni kutotutendea haki watanzania. Tuwape heshima wanayostahili kama binadamu lakini tusivuke mpaka na kuanza kuwasujudia. Mbaya zaidi hao unaowadai wana damu ya Mwalimu mbona waliojiita wasemaji wa ukoo waliwatolea nje? Walisema (I stand to be corrected) kuwa Vincent si ndugu wa karibu ( ingawa ni mtoto wa mdogo wake Mwalimu) na Leticia ni mtaliki wa mtoto wa Nyerere kwa hiyo si damu yao ( Makongoro amfungia safari Leticia Nyerere! ) Sasa hayo ya baraka yalikuwa wapi? Tumshukuru Mungu kwa Mwalimu lakini si kwa familia yake. Hapa si Korea ya Kaskazini.

  Amandla......
   
 15. gillard

  gillard JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 227
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 60
  kweli mkuu nimeipenda!
   
 16. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kingine kilichobaki ni kutafita CONSPIRACY THEORY ya kujipa moyo!
   
 17. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Yombaga Yombaga Yombaga wa ng'wise Yombaga.

  Hamo CCM bhale na Shida sana

   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  very good advice ..tuko pamoja
   
 19. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280

  Laughed off
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Sauti ya hofu.

  Si munawadharau!! Hatujasahau. Tarehe 14 October 2010 hakuna kiongozi wa Serikali alikwenda huko. Gazeti la Mwananchi likawaumbua. Mukaja na vitisho vya kutaka kulifungia.

  Mungu si mwanadamu bwana.

  Jaribuni kuwachakachua kama munaweza.
   
Loading...