Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa mara na pia mbunge wa jimbo la musoma mjini Vincent Nyerere amemaliza kazi ya kuwanadi wagombea wa ukawa mkoani mara,siku ya leo amefanya mikutano sita katika wilaya tofauti za musoma vijijini na kumalizia kuwanadi wagombea wa kijiji cha mugango ambapo wazee 10 wa vitongoji na wanachama 60 wa CCM wameamua kurudisha kadi za ccm na kujiunga na wanaharakati kudai haki zao.Upepo wa CCM mkoani mara umebadilika na kuwa wa hovyo kuliko ilivyowahi kutokea.Siku ya kesho atahitimisha kampeni katika jimbo lake la musoma mjini ambapo mkutano utafanyika viwanja vya shule ya sekondari mara