Vincent Laswai wa Kibo Palace na Trust Bureau de changes yuko matatani?

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,987
22,515
Wanajamvi,
Vincent Laswai ni mfanyabiashara maarufu sana pale Moshi. Ndiye mwenye ile Kibo Palace Arusha, mwenye Bureau de changes Moshi na Arusha ambazo zilivamiwa na jeshi kipindi kile, na hadi sasa zimefungwa. Pia ana biashara za jumla kuagiza sukari na bidhaa nyingine kama batteries nk kutoka nje.

Kuna waliokuwa wakisema hiyo Kibo Palace wako na Uhuru Kenyatta. Hoteli hiyo ni maarufu sana. Viongozi wakubwa hufikia hapo. Kuanzia kina Kenyatta, Kikwete, na hata Bernard Membe, ambaye naye inasemekana ni rafiki mkubwa wa ndugu Laswai!

Sasa mida hii ninayozungumza, maafisa usalama pamoja na askari wamezunguka biashara zake na inasemekana anatafutwa. Nadhani tayari alikuwa amesha surrender passport yake, ila kama kachomoka, pengine alikuwa na zaidi ya moja.

Kuna wanaodai kuwa kuna mipango inayoendelea dhidi ya wafanyabiashara flani, wengine wanasema ni ukaribu wake na Bernard Membe ndiyo umemponza! Amekuwa monitored na hakuwa akiweza kuongea hata kwa simu bila kufuatiliwa.

Bado nasubiria kusikia nini hatma yake. Sijui kama ni issue ya utakatishaji fedha au ni kitu gani!

Pia wamebeba computers nk, kama kuna wenye info ya kinachoendelea watueleze. Hapo chini akiwa na JK
1551203173039.jpeg

Update:
Vyombo vya uchunguzi vimevamia biashara za mfanyabiashara tajiri wa Moshi, Vicent Laswai vikimchunguza kwa tuhuma za ukwepaji kodi.

Moshi. Vyombo vya uchunguzi ikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) vimevamia biashara za mfanyabiashara tajiri wa Moshi, Vicent Laswai vikimchunguza kwa tuhuma za ukwepaji kodi.

Biashara zake yakiwamo maghala matatu ya kuhifadhi bidhaa mbalimbali kutoka nchini Kenya yaliyopo maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na duka la jumla vimewekwa chini ya uchunguzi wa vyombo hivyo

Laswai mwenyewe jana na juzi hakupatikana kueleza juu ya uchunguzi huo kutokana na simu yake kutokuwa hewani na marafiki wa karibu wanadai yuko nchini India kwa matibabu.

Uchunguzi huu mpya unakuja ikiwa ni mwezi mmoja tu umepita, tangu Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuamuru kufungwa kwa duka lake kubwa la kubadilisha fedha la Trast lililopo mjini Moshi

Kufungwa kwa duka hilo nako kulikuja miezi mitatu baada ya BoT kufunga maduka 30 ya kubadilisha fedha jijini Arusha likiwamo la Central Forex ambalo lilikuwa ni tawi la duka lake la Trast la Moshi.

Operesheni hiyo iliyohusisha pia polisi lakini Kamanda wa Polisi mkoa Kilimanjaro, Hamis Issah hakupatikana ofisini na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi hakupokea ingawa juzi alionekana akiwa na kikosi kazi hicho majengo ya TRA.

Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo alithibitisha kuwapo kwa uchunguzi huo, lakini akakataa kueleza chochote akisema itakuwa ni kuingilia uchunguzi.
Source: Mwananchi.

Update: 1/3/2019

Kwa mujibu wa taarifa nilizonazo, Leo hii wamevamia nyumbani kwa ndugu Laswai kule Shanty town! Pia inasemekana kuwa mtoto wake anashikiliwa na polisi kule Arusha! Pengine ni kwenye jitihada za kutaka arudi kutoka huko aliko? Maana taarifa rasmi zina sema kuwa yuko India kwa matibabu!
 
Wanajamvi,
Vincent Laswai ni mfanyabiashara maarufu sana pale Moshi. Ndiye mwenye ile Kibo Palace Arusha, mwenye Bureau de changes Moshi na Arusha ambazo zilivamiwa na jeshi kipindi kile, na hadi sasa zimefungwa. Pia ana biashara za jumla kuagiza sukari na bidhaa nyingine kama batteries nk kutoka nje.

Kuna waliokuwa wakisema hiyo Kibo Palace wako na Uhuru Kenyatta. Hoteli hiyo ni maarufu sana. Viongozi wakubwa hufikia hapo. Kuanzia kina Kenyatta, Kikwete, na hata Bernard Membe, ambaye naye inasemekana ni rafiki mkubwa wa ndugu Laswai!

Sasa mida hii ninayozungumza, maafisa usalama pamoja na askari wamezunguka biashara zake na inasemekana anatafutwa. Nadhani tayari alikuwa amesha surrender passport yake, ila kama kachomoka, pengine alikuwa na zaidi ya moja.

Kuna wanaodai kuwa kuna mipango inayoendelea dhidi ya wafanyabiashara flani, wengine wanasema ni ukaribu wake na Bernard Membe ndiyo umemponza! Amekuwa monitored na hakuwa akiweza kuongea hata kwa simu bila kufitiliwa.

Bado nasubiria kusikia nini hatma yake. Sijui kama ni issue ya utakatishaji fedha au ni kitu gani!

Pia wamebeba computers nk, kama kuna wenye info ya kinachoendelea atueleze.
Nchi hii ya hovyo sana,
Kwenye korosho,wameburunda,tumetoka kapa,na mbwembwe zote za jeshi,sifa za kisiasa,hakuna kitu,Tsh,inazidi kuporomoka.
Badala ya kukamata mifisadi,Ana Tibaijuka,Chenge,Ngereja,na majizi yote yalioyoingia mikataba ya gesi,wanasumbua wafanyabiashara Wazalendo,wanaotoa ajira kibao kwa wa TZ.
Wao watuambie wanatoa ajira kwa nani,zaidi ya kuficha pesa yote nje ya nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kwa mfanyabiashara kuushindwa kuusoma upepo na kushikamana na mpinzani wa jiwe kwa zama hizi nikutaka kurudi kwny umaskini aisee.
Sidhani kama kabila linaingia hapo
Kwamba akichukuliwa hatua mtu wa kabila flani inakua vita ya kabila husika.
Lakini sishangai mko jirani sana na nchi zenye mwelekeo ambao mwizi analindwa na kabila lake na akiguswa na sheria ni kabila limeguswa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama kabila linaingia hapo
Kwamba akichukuliwa hatua mtu wa kabila flani inakua vita ya kabila husika.
Lakini sishangai mko jirani sana na nchi zenye mwelekeo ambao mwizi analindwa na kabila lake na akiguswa na sheria ni kabila limeguswa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu nionyeshe kwny comment yangu nimetaja neno kabila wapi?

Hujaona wanasema Laswai ni rafikiye Membe.

Na Membe si ndiye anatajwa kama mpinzani wa Magu?

Then huo ukabila unaosema umetoka wapi?
 
Back
Top Bottom