Elections 2010 Vinara watano wa uchakachuaji kura Afrika wapo Dar kumpongeza mwenzao...J\k\y\ Kikwete

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,612
728,446
Unapoona maraisi wa tano tu kutoka Afrika wamekuja kushiriki katika hafla ya kumpongeza JK na ushindi wa mezani basi ujue mabadiliko Afrika bado yana safari ndefu................

Maraisi hao ni Mwai Kibaki wa Kenya, Mugabe wa Zimbabwe, Rupiah Banda wa Zambia, Kabila wa Kongo na Zuma wa Afrika ya Kusini...............

Kibaki, Mugabe, Kabila na Banda hawahitaji utambulisho hata chembe kwenye ulingo wa kuchakachua kura..........

Zuma atakumbukwa kwa jinsi alivyompindua bosi wake Bw. Thabo Mbeki isivyo halali na kinyume cha sheria....................Matarajio ya wasauzi kuwa Zuma angeleta mabadiliko ya kiuchumi sasa yamefifia kabisa na wanafikiria namna ya kumtupia virago vyake............

Kutokana na viongozi Afrika kuingia madarakani bila ya ridhaa ya wapigakura ndiyo maana huchukia utawala bora na hufanya jitihada za khali na mali kuuchelewesha kwa sababu utawala bora ni tishio lao kuendelea madarakani....................

Hii yatushibisha kwa nini AU ipo tayari kubeza maelekezo ya mahakama za kimataifa ili kuwalinda akina Al-Bashir wa Sudan na kukwepa kuwakamata ili wajibu tuhuma za mauaji kule Darfur................Bila ya misingi ya kiutu ya utawala bora Afrika itaendelea tu kuwa shamba la bibi na kutafunwa na wajanja wachache...............Kibaki alikwisha mwalika Al-Bashir Kenya na kudharau maelekezo ya mahakama ya kimataifa kuwa akamatwe.........Huu ni mfano mzuri wa viongozi wa Afrika wasivyopenda kuwajibishwa ila ni magwiji wa kuwaajibisha mahasimu wao kisiasa............ kama kule Rwanda kugombea uraisi dhidi ya Kagame ni kosa la jinai na waweza kuhukumia kifungo cha maisha.................Kweli Afrika bado tunayo safari ndefu ya kujikomboa.................
 
Susuviri

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
3,713
885
Sawa sawa mkuu, Banda ameshinda 27% ya kura, Kabila ni dikteta, Kibaki naomba nisiendelee kupoteza muda, Mugabe ndo kabisaaaa. Hata wale marais wababe lkn wenye akili kidogo kama Museveni na Kagame walituma wawakilishi... hawataki kuji-associate. Alafu pia sijaona mabalozi wengi huko, kama vile wathungu nao wamesusa... :smile-big:
Mi ninaamini kuwa hao hao wazungu anaowategemea JK kwa misaada sasa hivi wako makini nae na hawako tayari kujihusisha na kiongozi asiyekubalika. Na kila wakiuliza maoni ya watu nje ya serikali kama vile waangalizi wa ndani, ripoti inayotoka si nzuri... hata wasimamizi wa ndani wamesema kulikuwa na uchakachuaji, kwa hiyo wameshaona kuwa ni rais wa uchakachuaji. Na jinsi ambavyo Dr Slaa alivyoamua kuachana na unafiki wa kijinga eti ya kwenda kumshika mkono na kumpongeza, ndivyo hata mataifa wa nje wanavyozidi kujiuliza kulikoni.
JK atarajie kipindi kigumu sana baada ya kuwa kipenzi cha watanzania 2005 na cha nchi za nje, sasa amekuwa most hated president, na amegawa nchi. This is his legacy. It could have been different!
 
Omuregi Wasu

JF-Expert Member
May 21, 2009
749
141
Unapoona maraisi wa tano tu kutoka Afrika wamekuja kushiriki katika hafla ya kumpongeza JK na ushindi wa mezani basi ujue mabadiliko Afrika bado yana safari ndefu................

Maraisi hao ni Mwai Kibaki wa Kenya, Mugabe wa Zimbabwe, Rupiah Banda wa Zambia, Kabila wa Kongo na Zuma wa Afrika ya Kusini...............

Kibaki, Mugabe, Kabila na Banda hawahitaji utambulisho hata chembe kwenye ulingo wa kuchakachua kura..........

Zuma atakumbukwa kwa jinsi alivyompindua bosi wake Bw. Thabo Mbeki isivyo halali na kinyume cha sheria....................Matarajio ya wasauzi kuwa Zuma angeleta mabadiliko ya kiuchumi sasa yamefifia kabisa na wanafikiria namna ya kumtupia virago vyake............

Kutokana na viongozi Afrika kuingia madarakani bila ya ridhaa ya wapigakura ndiyo maana huchukia utawala bora na hufanya jitihada za khali na mali kuuchelewesha kwa sababu utawala bora ni tishio lao kuendelea madarakani....................

Hii yatushibisha kwa nini AU ipo tayari kubeza maelekezo ya mahakama za kimataifa ili kuwalinda akina Al-Bashir wa Sudan na kukwepa kuwakamata ili wajibu tuhuma za mauaji kule Darfur................Bila ya misingi ya kiutu ya utawala bora Afrika itaendelea tu kuwa shamba la bibi na kutafunwa na wajanja wachache...............Kibaki alikwisha mwalika Al-Bashir Kenya na kudharau maelekezo ya mahakama ya kimataifa kuwa akamatwe.........Huu ni mfano mzuri wa viongozi wa Afrika wasivyopenda kuwajibishwa ila ni magwiji wa kuwaajibisha mahasimu wao kisiasa............ kama kule Rwanda kugombea uraisi dhidi ya Kagame ni kosa la jinai na waweza kuhukumia kifungo cha maisha.................Kweli Afrika bado tunayo safari ndefu ya kujikomboa.................
:A S angry:Duhh! Ina maana JK baada ya utawala wake asubiri kwenda Keko au Ukonga? !!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom