Vinara wa Soka Waliopotea Kabla ya Wakati Wao!

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
1. Pablo Aimar - Kabla Messi hajatokea huyu ndiye aliyekabidhiwa mikoba ya Maradona!
2. Austin Okocha - Pele alikiri kuwa huyu kiungo madoido ni balaa na atafanya makubwa!
3. Faustino Asprilla - Alitegemewa kutumia mapande ya Valderamma kutesa muda mrefu!
4. Comrade Companero - Bahati mbaya timu ya taifa lake ni kichwa cha mwendawazimu!
5. Giuseppe Signori - Serie A ilishuhudia magoli yake murua ila Azzuri haikumtumia vizuri!
6. Ronaldinho Gaucho - Umri bado unamruhusu ila ameshapoteza kasi, nguvu na ari zaidi!
 
Habari hii imenishitusha kidogo kwa sababu mimi ninavyojua miongoni mwao wamecheza kwa umri ambao mchezaji anakuwa kwenye hali ya uchezaji na baada ya hapo mwili hauwezi tena kuendana na kasi ya mpira. Lakini inategemea pia unafuatilia ligi zipi, maana kwa wale wanaofuatilia ligi ya uingereza tu hapo ni sawa. Lakini kwa wanofuatilia ligi nyingine nyingi basi utafahamu kuwa wachezaji wametumika kama ilivyostahili ispokuwa Van Basten ambaye sababu ya majeraha yalifupisha muda wake wa kucheza hata hivyo katika umri wa miaka 30. Kichekesho ni Mchezaji ULIMBOKA MWAKINGWE yeye amestaafu akiwa na umri wa miaka 25, kama ni kweli umri uonaonekana ni sahihi.

Lakini Pablo César Aimar bado anacheza kwa kiwango cha juu kabisa kwenye Club ya benifica akishirikiana na Javier Saviola, kama ilivyo kwa Gaucho ambaye pia ni mchezaji wa kudumu AC Milan. Kama unafuatilia kwa kina mambo ambayo yalimuweka kwenye wakati mbaya kocha wa Brazil -Dunga ni kumuacha Gaucho.

Ninaambatanisha vielelezo vya wachezaji husika kwa msaada wa wikipedia
 
Attachments

  • players profile.xls
    16.5 KB · Views: 69
Mosesk: Uko sahihi kwa kiasi fulani ila hapa suala ni wachezaji hao kuisha kabla ya wakati - Aimar alitakiwa awe anatesa pamoja na Messi kwenye timu ya taifa; yaani kuna siku walicheza pamoja timu ya taifa na Messi akafurahi sana kuungana na mtaalamu mwenzake waliyetesa pamoja kwenye timu ya taifa ya yosso; Ronaldinho wachambuzi wote wa soka wanakubali kuwa bado umri unamruhusu kutesa katika kiwango chake cha zamani ila amepoteza hamu yake ya kufanya mambo mazito kutoka na msongo wa matatizo ya nje ya uwanja - akitatua hilo basi atarudisha tu kasi yake; Okocha si wa kustaafu bila kuwa mchezaji bora wa dunia katika viwango vya Maradona na Messi; Signori alikuwa mkali kuliko hata Baggio ila Azzuri haimkumbuki; Asprilla alipaswa kuifikisha Colombia mbali; na Companero angezaliwa kwingine angetesa!

Kweli: ni kweli Van Basten alipotea kutokana na kuumia, alikuwa anapiga mabao Van Nilsteroy cha mtoto!
 
7. Sebastian Deissler - kupotea kwake kunasikitisha sana hata nashindwa kuelezea!
8. Said Mwamba - tatizo alilolipata ni kama la Compa na vinara wengine Tanzania!
9. Ronaldo Lima -akipunguza uzito anaweza kucheza kwa kiwango cha juu siku zote!
10. Ricardo Kaka -dogo ndio kashapotea kwa uzembe wake labda muujiza umtokee!
 
11. Emanuel Adebayor
12. Robin Van Persie
13. Andriy Schevchenko
14. Zlatan Ibramovich
15. Edibily Lunyamila-ambaye aliingiwa na ushamba akaanza kula hovyo, kunywa pombe
ovyo na kulazimika kustaafu mapema. Shule aliacha, sasa hivi
hakuna elimu hakuna soka. Kwishney.
 
Hiyo ya Ibracadabra si Gang Chomba pekee atakayeibishia!

Kuhusu Van Persie nakubaliana na wewe, muumiaji sana!

Sheva alifanya kosa kama la Kaka - la kuondoka AC Milan!

Adebayor bado ana nafasi ila inabidi ahame na atulie!

Lunyamila alipaswa kupewa lishe maalum kama Messi!
 
malota soma...john makelele...itutu kigi...issa athuman.....damian mrisho...pondamali
 
Andriy Mykolayovich Shevchenko a.k.a SHEVA
Adrian MUTU a.k.a adimutu

hawa wawili wamepotea machoni na masikiano mwangu still wakiwa bado katika form

with out 4gettin my all time fev. katika avatar yangu "wit his magic left leg" nafkiri mnamfahamu..

_38080950_rivaldo_ok_allsport.jpg

1. Pablo Aimar - Kabla Messi hajatokea huyu ndiye aliyekabidhiwa mikoba ya Maradona!
2. Austin Okocha - Pele alikiri kuwa huyu kiungo madoido ni balaa na atafanya makubwa!
3. Faustino Asprilla - Alitegemewa kutumia mapande ya Valderamma kutesa muda mrefu!
4. Comrade Companero - Bahati mbaya timu ya taifa lake ni kichwa cha mwendawazimu!
5. Giuseppe Signori - Serie A ilishuhudia magoli yake murua ila Azzuri haikumtumia vizuri!
6. Ronaldinho Gaucho - Umri bado unamruhusu ila ameshapoteza kasi, nguvu na ari zaidi!

Pablo Aimar El Mago alikuwa habari nyingine katika ulimwengu huu wa soka na tulitegemea mengi kutoka kwake ila ghafla akazimika kabla ya wakati wake naungana na wewe kumuweka katika kundi hili japo taarifa nilizo nazo yeye na Saviola hapo Benfica timu pinzani zinalala na viatu kwani kashikashi zao lakini bado atabaki katika kundi la waliopotea....Tanzania katika kundi hili ntamuweka Gula Joshua aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga ambaye aliwika sana mchangani mpaka Palson kama sijakosea, ya Arusha lakini nae ghafla hata kabla hajatumikia taifa naye kwishney....Jose Antonio Reyes nae takwimu zinamuhusu
 
1. Pablo Aimar - Kabla Messi hajatokea huyu ndiye aliyekabidhiwa mikoba ya Maradona!
2. Austin Okocha - Pele alikiri kuwa huyu kiungo madoido ni balaa na atafanya makubwa!
3. Faustino Asprilla - Alitegemewa kutumia mapande ya Valderamma kutesa muda mrefu!
4. Comrade Companero - Bahati mbaya timu ya taifa lake ni kichwa cha mwendawazimu!
5. Giuseppe Signori - Serie A ilishuhudia magoli yake murua ila Azzuri haikumtumia vizuri!
6. Ronaldinho Gaucho - Umri bado unamruhusu ila ameshapoteza kasi, nguvu na ari zaidi!

Haya bwana, nimekuelewa.
 
Hristo hakupotea kabla ya wakati wake - alicheza katika kiwango cha juu mpaka akawa mkongwe!
 
11. Emanuel Adebayor
12. Robin Van Persie
13. Andriy Schevchenko
14. Zlatan Ibramovich
15. Edibily Lunyamila-ambaye aliingiwa na ushamba akaanza kula hovyo, kunywa pombe
ovyo na kulazimika kustaafu mapema. Shule aliacha, sasa hivi
hakuna elimu hakuna soka. Kwishney.
16.Fernando Redondo,jamaa alitoka Real Madrid akaenda AC Milan.Na kama kawaida yao Milan wakaua kipaji adimu ambacho dunia imewahi kukiona.The guy was very skilled and stylish,a real playmaker!!
 
3. Faustino Asprilla

Huyu alifunga magoli mengi sana akiwa Parma, Italy. Alikuwa akifunga basi yeye ni kujibinua tu....

Faustino Asprilla - Wikipedia, the free encyclopedia

Hawa vijana wangu walidumu kwa mud amfupi sana kwenye timu za Simba na kufariki mapema pia:

1. Salehe Sonda 1. Method Mogella (Mafundi Mchundo wa kutoka TC Arusha).
 
Back
Top Bottom