Vinara wa Soka Waliopotea Kabla ya Wakati Wao!

Ni kweli Companero naona huyo namba 4 ni kaka yako etie....Comrade Companero...... kapotelea wapi?
 
Nkwingwa....Umenikumbusha mbali sana babu.....Huyu jamaa mzee wa 'Scorpion kick' alikuwa na mbwembwe na vituko golini dizaini ya Juma Pondamali 'Mensah'....Kwa mujibu wa wikipedia jamaa kastaafu soka mwezi January mwaka huu akiwa anadakia Deportivo Pereira ya kwao Colombia

René Higuita - Wikipedia, the free encyclopedia

Kuna wakati Colombia ilicheza mechi ya kirafiki (nadhani) na England pale Wembley stadium...jamaa aliokoa goli kwa sarakasi flani hivi....mpaka sasa sijawahi kuona tena kipa akiokoa goli kwa njia ile. Unaikumbuka hiyo Nkwingwa?
 
Kuna wakati Colombia ilicheza mechi ya kirafiki (nadhani) na England pale Wembley stadium...jamaa aliokoa goli kwa sarakasi flani hivi....mpaka sasa sijawahi kuona tena kipa akiokoa goli kwa njia ile. Unaikumbuka hiyo Nkwingwa?

Yeah....Naikumbuka vizuri sana,ilikuwa ni mwaka 1995 jamaa aliokoa mpira uliopigwa na mtaalam Jammie Redknapp uliokuwa ukielekea nyavuni aliaruka kama mtu anavyoruka kuingia kwenye maji akitokea nje halafu anainua miguu miwili ya nyuma kuupiga mpira unaoelekea golini(kama nge anavoinua mkia wake),nakumbuka kwa Bongo miaka ya 95 mwishoni na 96 ITV walikuwa wakiionesha sana clip ya tukio lile.......Hii iliitwa 'Scorpion kick'
 
hah hah haaaaah nilikuwa napita tu but nilipoona mkongwe mwandamizi Barantanda nikadumbukia humu coz nilijuwa pameiva...
Ok labda nimtaje Santiago Solari
 
Wako wapi kina Hassan Sas, Ilhan Mansiz, wale jamaa wa uturuki waliofika semifinal world cup 2002?
Hao wote wamestaafu soka,kuna mwingine anaitwa Yildray Basturk ni mfupi anaonekana kama mjapan yupo blackburn rovers,alicheza na kina Ballack,Lucio,Placente,Neuville na Berbatov pale Bayer Leverkusen 2002 inacheza final champions league baada ya kuwatoa Man Utd ,vs Real Madrid Zidane anafunga bao maridadi la ushindi.
 
Mosesk: Uko sahihi kwa kiasi fulani ila hapa suala ni wachezaji hao kuisha kabla ya wakati - Aimar alitakiwa awe anatesa pamoja na Messi kwenye timu ya taifa; yaani kuna siku walicheza pamoja timu ya taifa na Messi akafurahi sana kuungana na mtaalamu mwenzake waliyetesa pamoja kwenye timu ya taifa ya yosso; Ronaldinho wachambuzi wote wa soka wanakubali kuwa bado umri unamruhusu kutesa katika kiwango chake cha zamani ila amepoteza hamu yake ya kufanya mambo mazito kutoka na msongo wa matatizo ya nje ya uwanja - akitatua hilo basi atarudisha tu kasi yake; Okocha si wa kustaafu bila kuwa mchezaji bora wa dunia katika viwango vya Maradona na Messi; Signori alikuwa mkali kuliko hata Baggio ila Azzuri haimkumbuki; Asprilla alipaswa kuifikisha Colombia mbali; na Companero angezaliwa kwingine angetesa!

Kweli: ni kweli Van Basten alipotea kutokana na kuumia, alikuwa anapiga mabao Van Nilsteroy cha mtoto!
Wachezaji wengi wanaokuwa moto kwenye age 17-23,huwezi kuwakuta ktk age 30 wakifanya mambo makubwa. Huwa wanakuwa wametumika vya kutosha kuweza kuhimili kashkash na wengine hupotea sababu ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu na wanapokuwa wamepona wanapata wakati mgumu kurudi kwenye kiwango chao,hivyo makocha wengine huwaacha bench au kuwatoa kwa mkopo kwenye timu ambazo wengi huwa hatuna mazoea ya kuzifuatilia kwa hiyo huwa wanapotea katika fikra zetu japo huko waliko kiwango huwa juu.

Van Basten...! Blatter,aliumia sana kiasi cha kupiga kampeni kuwa tackle from behind iwe red card, akasisitiza kuwa hiyo ndiyo iliyokatiza maisha ya soka ya gwiji huyo wa kupachika magoli.
 
Yu wapi Rene Higuita yule kipa wa Colombia?
Nilibahatika kuona mechi moja,nadhani mwaka juzi,jamaa alikokota mpira mpaka katikati ya uwanja na kwa mshangao wa wengi, akatoa pasi kwa adui na halafu akageuka haraka kurudi golini kabla hajafika akakuta gozi linadundadunda ndani ya kimia!!!
 
Allan Smith,Alexandra Helb,Jose Antonio Reyes, nA wengine wengi bana nikitaja wote page itajaaa coz bongo ndio nahisi hata mia wamefika.......
 
Paul Gasgoine 'Gazza' - Mabangi nibangue yalifanya kipaji chake kipotee kabla ya wakati!
Diego Armando Maradona - Madawa ya kulevya yalifanya tukose uhondo wake WC 1994!
No! Kipaji cha mtu huyu hakikupotea sababu ya bangi. Alivunjika mguu ktk mechi ya FA Cup final na wakati huo akitakiwa kwenda ku join Lazio Rome ya Italy,so alikwenda Italy akiwa majeruhi na akakosa namba katika kikosi cha kwanza. Waingereza wakanzisha mkakati wa kumrudisha nyumbani,hivyo Headlines za magazeti ya Uingereza zikamchanganya mno na ndipo alipohamia Rangers ya Uskoch ambako alikuwa moto.

Kama utakumbuka vizuri huyu jamaa aling'ara san kwenye uro 96,basi tu kwa vile bahati haikuwa yao.
 
1998...
Tafarer, cafu, carlos, baiano aldair...

2002...
Marcos, cafu, carlos, roque Jr, edmilson, lucio...

kati ya hao yupo huyo uliyemsahau?
Huyo aliyemsahau alikuwepo 1994, alitolewa kwa red card ktk mechi na USA baada ya kumpiga kwa kiwiko Tab Ramos (hapa nadhani gutierez anakumbuka vizuri,nshazeeka sasa!!!)
 
Nasisitiza: Huyo ni kivuli cha Dinho tunayemjua!
Narudia: Kwa umri wake Dinho hastahili kuisha!
Nakumbusha: Bado Dinho anapaswa kukimbiza!
Dinho alimalizwa na penzi la mtoto wa Rijkaardt!! Jamaa akaanza kumweka ubaoni,akakasirika sana na kuanza kukacha mazoezi, kisaikolojia, benchi lilimmaliza.
 
Hapa tunazungumzia tu wachezaji waliopotea kabla ya wakati wao japo walikuwa na kiwango cha juu sana, yaani, ama walistaafu au walikwisha kabla ya muda wao - watu kama Dahlin wa Sweden na Viola wa Brazil!
Martin Dahlin naye alishafika tamati maana wakati anasumbua wc 98 alikuwa aged,ila Thomas Brolin....aliishia mapema
 
Huyo aliyemsahau alikuwepo 1994, alitolewa kwa red card ktk mechi na USA baada ya kumpiga kwa kiwiko Tab Ramos (hapa nadhani gutierez anakumbuka vizuri,nshazeeka sasa!!!)

kama ni 94 basi huyo ni Leonardo ambaye alikuwa kocha mkuu msimu uliopita wa klabu yenye mafanikio zaidi hapa ulimwenguni hapa naizungumzia AC Milan.
 
Dinho alimalizwa na penzi la mtoto wa Rijkaardt!! Jamaa akaanza kumweka ubaoni,akakasirika sana na kuanza kukacha mazoezi, kisaikolojia, benchi lilimmaliza.

Dinho huyuhuyu ambaye Jana kawapiga goli Auxere dk ya 91 na kisha kuifanya Milan kufuzu au kuna Dinho mwingine wa Mbagala maji matitu
 
Dinho huyuhuyu ambaye Jana kawapiga goli Auxere dk ya 91 na kisha kuifanya Milan kufuzu au kuna Dinho mwingine wa Mbagala maji matitu
Huyohuyo Gang Chomba, ni boy friend wa binti wa Frank Rijkaardt na walikuwa wakijirusha sana, binti baada ya kuombwa na baba yake amwache Dinho,akatishia kujiua,
 
Back
Top Bottom