Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,270
Kinywaji hiki kilitumiwa sana na wanajeshi wakati wa WWI, walifungiwa mabox ya Vimto na kuoekekewa huko mstari wa mbele.
Miaka ya 1900+ waarabu walipata leseni ya kutengeneza Vimto na waliendelea kuitengeneza kwa ubora ule ule. Leo hii Vimto ya Saudia imebaki kuwa bora kuliko ile inayotengenezwa Uingereza. Arabuni kinywaji hiki ni maarufu hasa wakati wa Ramadhani baada ya mfungo wa siku nzima.
Kwa ubora wake changanya 100mls za Vimto kwenye jug la maji lenye ujuzi wa 500mls. Maji ya baridi yanafaa zaidi.
Si kuwa ninawafanyia promotion lakini ningependa kizuri tukinywe wote. Mbele ya Vimto ya Saudia huwa beer 🍺 siipi nafasi.