Vimini Vya Wanawake Vyasababisha Kweli Tetemeko la Ardhi-TAIWANI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vimini Vya Wanawake Vyasababisha Kweli Tetemeko la Ardhi-TAIWANI

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Apr 28, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,375
  Likes Received: 5,662
  Trophy Points: 280
  Tuesday, April 27, 2010 5:05 PM
  Tetemeko la ardhi limetokea kweli katika siku ambayo wanawake toka sehemu mbali mbali duniani walivaa vimini na wengine kuonyesha sehemu za matiti yao ili kupinga kauli za kiongozi wa kidini wa Iran aliyesema kuwa vimini vya wanawake ndivyo vinavyosababisha mabalaa duniani.Kampeni ya wanawake zaidi ya laki moja na nusu toka sehemu mbalimbali duniani kupinga kauli ya kiongozi wa kidini wa Iran kuwa wanawake wanaovaa vimini na nguo zisizo za heshima wanasababisha matetemeko ya ardhi imeula wa chuya baada ya tetemeko la ardhi kutokea kweli walipoamua kuvaa vimini na kuonyesha matiti yao.

  Tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa 6.9 lilitokea nchini Taiwan na kusababisha majengo kuyumba na kutokea kwa mmonyoko wa ardhi uliopelekea kuzikwa kwa magari matatu.

  Hakuna taarifa ya vifo katika tetemeko hilo la ardhi lakini tetemeko hilo limewakatisha tamaa viongozi wa kampeni ya BoobQuaqe iliyoanzishwa kwenye mtandao wa FaceBook.

  Akiongea katika sala ya ijumaa mjini Tehran nchini Iran aprili 16 mwaka huu,
  mmoja wa viongozi wa juu wa kidini wa Iran, Ayatollah Kazem Sedighi alisema "Wanawake wengi siku hizi hawavai nguo za heshima na matokeo yake wanawachanganya wanaume na kupelekea kuongezeka kwa matendo ya zinaa ambayo ndiyo yanayosababisha matetemeko ya ardhi na mabalaa duniani".

  "Majanga yanayotokea duniani yanatokana na madhambi ya watu", aliongeza Ayatollah Sedighi.

  Kauli hiyo ilipelekea mwanafunzi Jennifer McCreight, 22 wa Indiana Marekani, aanzishe kundi kwenye facebook kupinga kauli za kiongozi huyo wa kidini wa Iran.

  Jennifer alianzisha kundi linaloitwa "BoobQuaqe" kwenye Facebook ambalo liliwahimiza wanawake kuyaonyesha matiti yao hadharani majira ya mchana jana tarehe 26 aprili.

  Akiliongelea tetemeko la ardhi lililotokea nchini Taiwan, Jennifer alisema kuwa matetemeko ya ardhi yenye ukubwa kati ya 6 na 6.9 hutokea mara moja kwa mwaka, kama likitokea tetemeko jingine ndani ya masaa 24 basi tutaanza kusali na kuvaa nguo za heshima.


  [​IMG]
  NIFAHAMISHE.COM
   
 2. K

  Kachero JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hee hii ni balaa na sijawahi kuisikia tena,Duuh!
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,375
  Likes Received: 5,662
  Trophy Points: 280
  Wapendwa mambo mengine yanatisha
  majuzi tulileta mada ya ayatollah mmoja wa iran kulaan vimini na kusema ndivyo vinajaza matetemeko ya ardhi iran
  ndugu zetu hao wakiongozwa na bint moja wa marekan akatangaza SIKU YA KUVUA SIDIRIA DUNIAN KUONYESHA MA-NESTLE
  kulaani maneno ya ayatollah ..jamaa wakaitikia wito moto ukawafwata....bado dar siju tutapunguzaje hili tatizo
   
 4. M

  Makanyagio Senior Member

  #4
  Apr 28, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hawakuvaa vimini wala utemebea matiti wazi. Picha ziko wapi?
   
Loading...