Vimifuko vidogo vya plastiki vinavyotumika na wauza matunda, vitafunwa na mabucha ni janga kwa mazingira

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,346
45,702
Ikiwa ni miaka miwili imepita tangu marufuku ya kutengeneza na kutumia mifuko ya plastiki kupitishwa nchini bado kuna vimifuko vya plastiki ambavyo hutumika zaidi kwenye mabucha ya nyama na biashara ya matunda.

Kama serikali ilikataza matumizi ya mifuko ya plastiki kwa sababu ya athari zake nyingi na za muda mrefu katika mazingira ni sababu gani imeendelea kuruhusu hii mifuko ya plastiki nyepesi kuendelea kutumika baadaye katika baadhi ya biashara? Umefika wakati sasa wa kuharamisha kabisa mifuko yoyote ya plastiki ambayo bado inaendelea kutumika.

Tuyalinde mazingira yetu kwa nguvu zote.Ni wajibu wetu kwa kizazi chetu na kijacho kuuacha ulimwengu ukiwa mzuri zaidi.
 
SerikaLi yenyewe imeshindwa kutuLindia haki yetu acha na ss tufanye tunachojiskia tuuh
 
Back
Top Bottom