De Professor

JF-Expert Member
May 21, 2021
206
395
Habari wanajamvi, katika maisha kweli kuna safari ndefu leo nimekumbuka zamani sana kipindi natafuta maisha nilipoanza kupanga kwenye nyumba za watu vile vioja vya hapa na pale.

Mara mwenye nyumba yupo hivi mwingine nae yupo vile Mara sehemu uliyohamia unakuta wapangaji wanatabia hii wengine hivi basi ni mtafaluku.

Nimetamani kushare baadhi ya ioja nilivyokutana navyo nadhani tutapata kujua makasheshe ya huku na kule.

Nakumbuka
I. Nilianzia Yombo sehemu flani karibu na makaburi ya City huku mwenye nyumba alikua maza flani yeye mumewe alifariki sasa nyumba wakawa wamepangisha baadhi ya vyumba na wao wanaishi humu humo kulikua na dogo wa kiume wa kwanza nasikia yeye ndio alikua na sauti ya kuchukua kodi mle ndani na siku akichukia anatembeza makofi kwa dada zake mpaka mama, dogo alikua anapuliza majani hana kazi ni kwenda vijiweni kucheza kamali basi.

2. Buza kwa Lulenge huku nilikutana na wapemba wapangaji wenzangu wao usiku wanalala nje kwenye varanda kisa ndaji joto ila life style yao ya chai ndo ilinikosha sujari inanunuliwa robo baada ya chai inaisha kesho nyingine.

3.Kigamboni kuna nyumba tulikuabwapangaji 3 mwenye nyumba mzungu sana wala haishi pale dah kumbe yule jamaa mmoja ana familia watoto 2 kazi yake huwa anauza Gongo yeye mchana yupo usiku anatoka asubuhi mapemaa utaona vidumu vinatolewa ndani nilikaa na jamaa miezi zaidi ya 6 sijashtukia.

Kelo ilikua bachela nilikua pekeangu wengine wawili walikua wameoa tatizo wake zao wanatoka sehemu yao wanakuja kupigia stori mlangoni kwangu afu wameweka mkeka, hapo inaeza kuwa siku sijaenda job au wekend basi ukifungua mlango tu hata kwenye saa Nne asubuhi unakutana na migongo yao mlangoni dah nilikua nakereke hatari, sasa usiombe ukawa umevusha hahahaha wataganda pale mpaka utoke nae dah.

Hizo ni baadhi tu ya nyunba nilizokaa mpaka sasa namshukuru Mungu maisha hayo nilisha yapita.
 
Kuna Uzi kama huu nadhani

Kuna Uzi kama huu nadhani

Ooh...naona wakati na type haikuja headings za kulandana namna hiyo, shukrani Mshana De Legendary 😃
 
hqdefault-5.jpg
 
Mkuu ulikuwa uwahi sehemu nini.....
 
Cheku,cheku cheku..cheku chekuu/gutu gutu gutu sasa hpo upo chumba cha katikati kushoto wanashambulia kulia wanamilika chumba cha mbele yako kuna msukuma anaongea na simu kwa kilugha na watu wa usukumani. Hallow weeeeeee utatamani utulivu wa nyumba za tembe mbona
 
Changamoto namba moja ni hiyo ya kua na wadada au wamama wanaopenda kukaa maeneo ya milangoni mwa watu kupiga stori, hufanyi mishe zako kwa uhuru kabisa.

Nyingine ni ile mnakaa wapangaji wengi afu choo cha kuchangia na wapo wenye watoto. Unakuta sasa wale watoto nao wanatumia choo hicho halafu kwakua bado wadogo, kuzingatia usafi hawawezi mpaka wawaite wazazi wao.

Unakuta sasa ndo time zile umebanwa haja, unawai choonia unakuta dogo kasha haribu afu anamskilizia mama yake aje kusafisha, mama yake nae hata hajui yuko bize uko. Utachukia sana nyumba za kupanga za kuchangia vyoo
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom