bartenderznz
JF-Expert Member
- Jul 18, 2016
- 398
- 195
Klabu ya Villarreal imechukua Ubingwa wa Ligi ya Europa baada ya kuifunga Klabu ya Manchester United kwa penati 11-10
Timu hizo zilifungana goli 1-1 katika dakika 120 hatua iliyofanya mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati.
Villarreal ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya 29 kupitia kwa Gerard Moreno, lakini Manchester iliweza kusawazisha kupitia kwa Edinson Cavani katika dakika ya 55.
Katika upogaji Matuta, Kipa wa Villarreal, Geronimo Rulli aliweza kuokoa penati na kipa mwenzake David De Gea na kuipa timu yake Ubingwa huo.
Kocha wa Villarreal Unai Emery ameweka rekodi ya kuwa Kocha wa kwanza kushinda mataji ya UEFA Cup/Europa League kwa mara nne (2013-14, 2014-15, 2015-16 & 2020-21).