Villarreal yanyakua Kombe la Ligi ya EUROPA. Yaifunga Man. Utd kwa penati 11-10

bartenderznz

JF-Expert Member
Jul 18, 2016
398
250
CF8D84FB-BC80-4E8D-BB47-F84ED151B758.jpeg

Klabu ya Villarreal imechukua Ubingwa wa Ligi ya Europa baada ya kuifunga Klabu ya Manchester United kwa penati 11-10

Timu hizo zilifungana goli 1-1 katika dakika 120 hatua iliyofanya mchezo kuamuliwa kwa mikwaju ya penati.

Villarreal ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli katika dakika ya 29 kupitia kwa Gerard Moreno, lakini Manchester iliweza kusawazisha kupitia kwa Edinson Cavani katika dakika ya 55.

Katika upogaji Matuta, Kipa wa Villarreal, Geronimo Rulli aliweza kuokoa penati na kipa mwenzake David De Gea na kuipa timu yake Ubingwa huo.

Kocha wa Villarreal Unai Emery ameweka rekodi ya kuwa Kocha wa kwanza kushinda mataji ya UEFA Cup/Europa League kwa mara nne (2013-14, 2014-15, 2015-16 & 2020-21).
 

tc_edo

Senior Member
Apr 9, 2021
123
225
Ni fainali ya EUROPA, Manchester United ikichuana na Villareal kwenye kiwanja cha Stadion Energa Gnask, Gnask, nchini Poland mnano saa Nne kamili muda wa afrika mashariki.
Ni battle ya Unai Emery na Ole Gunnar Solskjaer​

IMG_20210526_185758.jpg
 

Kizibo

JF-Expert Member
Jul 3, 2018
2,749
2,000
Kwa wanaotumia antena za star times, inawezekana kulipia bundle la siku 1 (masaa 24?) ni sh ngap?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom