Vilio vya wafanyakazi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
wachinaurafiki.jpg


Wafanyakazi wameanza kulalamika siku nyingi kuhusu mambo mbali mbali kuhusiana na ajira zao. Lakini siri kali imekaa kimya. Hatusikii tena ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya wala maisha bora kwa kila Mtanzania.
 
..hapo wazee kazi ipo na wanahitaji zaidi ya hayo maandamano ili kufanikiwa la sivyo nyimbo zitakuwa hizo miaka yote,naamini sana haki kama hizo zipo mahakamani na kama hakuna sheria ni bora kumobilize wafanyakazi kuweka muswada huo..ni kazi kweli kweli lakini vitu vizuri lazima jasho likutoke!
 
Wafanyakazi Urafiki wachachamaa

2007-10-30 16:36:59
Na Job Ndomba,Urafiki


Wafanyakazi zaidi ya 500 wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha Jijini Dar es Salaam, waliosimamishwa kazi kwa muda usiojulikana, kufutia menejimenti kuhofia kushindwa kuwalipa mishahara mipya iliyotangazwa na Serikali hivi karibuni kwa sekta binafsi, wameipa masaa matano menejimenti ya kiwanda hicho kutoa tamko kuhusu haki zao.

Wakiongea na gazeti hili leo asubuhi, wafanyakazi hao wameapa kushusha skadi za rushwa kwa TAKUKURU wanazodai zimekithiri ndani ya kiwanda hicho.

Aidha wamesema menejimenti kama haitasema lolote katika masaa hayo waliyotoa, hawataondoka katika lango kuu la kiwanda hicho hadi kitakapoeleweka.

``Tutawasha moto na kulala hapo kwenye lango kana kwamba kuna matanga,`` baadhi ya wafanyakazi waliodai wanawakilisha wenzao wamesema.

``Sisi tunawapa masaa matano kuanzia asubuhi hii na itakapofika saa nane ya leo watupe tamko kuhusu haki zetu za miaka mitano, la sivyo tumeaandaa mabango yetu ya kushinikiza malipo yetu, ambayo tutayashika mchana,`` wakaongeza.

Aidha wameiomba TAKUKURU kutupia macho kiwandani hapo kwa madai kuwa kuna mianya ya rushwa iliyojificha ndani yake.

``Sisi sasa tumechoshwa na vitendo vya unyanyasaji ndani ya kiwanda hiki tunaiomba TAKUKURU ije tuwape siri zilizojificha huku ndani kwani kuna kiwanda cha mbao ndani ya Urafiki... wanadai wanasafirisha pamba kumbe magogo,``akasema kiongozi huyo.

Wamesema wameshaandaa mabango yenye vilio mbalimbali na tuhuma za siri za kiwanda hicho ambayo wanatarajia kuyaonyesha leo endapo menejimenti haitatoa tamko.

Vyombo vya habari vimeripoti leo asubuhi kuwa Urafiki inaungana na viwanda vya nguo vya Kanda ya Ziwa, Musoma Textile (MUTEX) na Mwanza Textile (MWATEX) ambavyo vimeripotiwa vikijiandaa kupunguza wafanyakazi wake.


SOURCE: Alasiri
 
Back
Top Bottom