Vilio, simanzi vyatawala kumuaga MJAZITO ALIEUWAWA NA MAJAMBAZI-Jackline

ni kweli walieuwawa sio wao kabisa serikali kupitia jeshi la po;lisi wanawadanganya watu wamewauwa majambazi husika kumbe sio
waliouwa wako huru wanakula kuku zao kwa starehe

walaaniwe nyari familly

Polisi wote wa ngazi za juu wanayajua mambo ya Nyari lakini hawathubutu kuchukua hatua yoyote. Hata alipokamatwa wakati ule nadhani 2004 hivi kwa ujambazi, kilichomfanya akamatwe si kuwa eti polisi waliamua kufanya kweli na kumaliza mzizi wa ujambazi. Ni hasira ya James Kombe (akiwa RPC wakati huo) kutokana na dharau Nyari aliyoonesha siku Minja aliporipoti tukio la ujambazi aliofanya. Nyari alikuwa anadai kuwa Kombe anastahili ampigie saluti kwa sababu hata bosi wake Mahita alikuwa anafanya hivyo kwa Nyari. Ndipo Kombe alipoamua liwalo na liwe, namweka ndani na kesi itashughulikiwa kama za wengine bila kujali urafiki wao na Mahita. Daniel ole Njoolay akiwa mkuu wa mkoa alitaka kumtoa kwa amri, Kombe akagoma na kuapa kuwa yuko tayari kuvua kombati arudi kwao kulima kuliko kumuachia kimizengwe. Yaani huyu Nyari ni hatari ana mtandao serikali yote, sasa hivi baada ya kutoka jela ana cheo kipya, ni kamanda wa vijana wa CCM na ni mmojawapo wa wafadhili wakuu. Mtu kama huyu utamwezaje ukiwa raia wa kawaida? Mama wa watu keshakufa hivyo, na hakuna kitakachoendelea zaidi ya kupigwa 'changa la macho' kuwa waliomuua nao wameshauawa, ni mafia style ya kuzima uchunguzi. Bahati mbaya tunaojua kinachoendelea hatuthubutu kujitokeza hadharani. Wale waliotoa ushahidi uliomfunga Nyari wakati ule wamekimbia na huko walikokimbilia nina uhakika wanaishi kwa mashaka makubwa sana. Alipofungwa kifungo cha miaka 30 walishangilia, lakini alipoachiwa na kurudi mjini kwa mbwembwe nyingi (ndege ya kukodi kutoka Dodoma alikokuwa amefungwa Isanga, msafara mrefu wa magari ya kifahari na party la kufa mtu), na kutangaza hadharani uswahiba na wakuu wa nchi, jamaa walinywea, wakatokomea kusikojulikana! Nchi hii ni ngumu sana ndugu zanguni.
 
What has this country come to!!!!!!!
Bandits killing innocent woman and the police killing the villians who could shed light on the reasons of such wanton killing!!!!
Now we will never know why did such thing happen
VERY SAD
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom