Vilio na kusaga meno kwenye Ngome ya CHADEMA vyatawala pale mlimani

KIDUNDULIMA

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
966
537
Ngome ya chadema imeingiwa na vilio na kusaga meno baada ya vijana wengi wenye usongo wa kuibwaga CCM kutoona majina yao kwenye orodha ya majina yaliyobadikwa kwenye jengo la Nkruma pale mlimani. "kwa kweli inasikitisha sana kutoonekana jina langu wakati mwaka 2005 nilipiga kura hapa hapa" Alilalama dada mmoja.

Mwingine aliuliza "iwapo hajaona jina lake achukue hatua zipi ili kuhakikisha kuwa haki yake ya kupiga kura inapatikana" wenine walimshauri aende ofisi za NEC au awapigie simu. Cha kushangaza majina yamebandikwa lakini hakuna maelekezo kwa yule ambae hatakuta jina lake afanye nini.

Kwa kweli dalili za uchakachuaji zimeanza kuonekana mapema kabisa.
 
Mbona nami sijaliona jina langu huku kwetu na sijasaga meno? Wewe ni CCM? Kwa nini unaonekana kuchekelea demokrasia inapopindishwa na serikali ya CCM?
 
You are not serious!! Umenikitisha binafsi kama unaona ni poa tu kunyimwa haki ya kuchagua viongozi uwapendao watakaotuongoza taifa miaka 5 ijayo
 
ingia website ya nec, muangalie kwanza, mi mwenyewe niliangalia kwa kupanic sikuliona ila baadae nilifanikiwa kuliona
 
unajua mi nashangaa sana.Ukiona mtu hajaona jina lake msaidie kuingiza namba zake kwenye mtandao wa NEC itakupa majibu.Ila kituoni unaweza ukaruka jina lako kumbe lipo.Pia labda kwa mistake limtokea kituo cha karibu.
 
Afuatilie kujua yamebandikwa katika jengo gani. Hata mwaka 2005 tuliojiandiksha kwenye kituo cha Dispensary majina yetu yalibandikwa huku LRD. Sasa si ajabu kwamba wale walioandikishwa Nkurumah, mwaka huu watapigia kura Library. wasifanye haraka kukata tamaa. Naamini haki yao haiwezi kupotea bure, wapite vyumba vyote vitakavyotumika kupigia kura waangalie kama majina yao yapo huko.
 
Hizi ni dalili za kutaka kuchakachua tu matokeo kwanini majina hayaonekani
au yamebandikwa vituo vingine?
 
Nilikuwa na wasiwasi huo baada ya kutoliona jina langu na la wife kituoni lakini ndani ya mtandao lipo poa kabisa
 
nendeni mkapige kura, ccm wanavumisha sana kuhusu wizi wa kura ili kukatisha wapiga kura tamaa. kura muhimu , wizi siyo rahisi hivyo
 
Kama hana uhakika jina lake lipo pale alipojiandikishia aende siku ya kupiga kura au ani PM namba yake nimuahikikishie kama lipo au la!
Nina hakika kila mtu atapiga kura bila shida. Acha uoga
 
Kuna watu wamejiandikisha majina yao yamebandikwa yanaonesha wamekataliwa kupiga kura. Hivyo kucheki kwenye mtandao may mislead, nenda kituoni kuhakikisha
 
Angalia kwenye mtandao vile vile na kwenye karatasi wamebadilisha vituo kwa mfano kama ulikuwa A unaweza kuwa umewekewa upande wa B wafanye haraka kama hawaoni wameambia waende kwa msimamizi wa uchaguzi wapewe mawaidha wako wapi
 
ingia website ya nec, muangalie kwanza, mi mwenyewe niliangalia kwa kupanic sikuliona ila baadae nilifanikiwa kuliona

jamani mnafanya makosa website jina lipo ila ukienda ubaoni halipo.

chondechonde wana jf muende ubaoni ukaangalie jina lako sio online jamani watu wana lia huku mtaani, leo nimekutana na dereva tax kaniambia jina lake alipo na amelala mika kaambiwa aende kesho waka pekue upya labda lipo ndani kwemye makaratasi.

nilichukua id yake nika mchekia nikamuonyesha jina lako lipo hapohapo ila ccm wajanja watakuwa wamefuta jina ubaoni ili usiende kupiga kura na hii ndio sababu za hawa jamaa kunakili majina mtaani kutumia wajumbe wao.

Ngome ya chadema imeingiwa na vilio na kusaga meno baada ya vijana wengi wenye usongo wa kuibwaga CCM kutoona majina yao kwenye orodha ya majina yaliyobadikwa kwenye jengo la Nkruma pale mlimani. "kwa kweli inasikitisha sana kutoonekana jina langu wakati mwaka 2005 nilipiga kura hapa hapa" Alilalama dada mmoja.

Mwingine aliuliza "iwapo hajaona jina lake achukue hatua zipi ili kuhakikisha kuwa haki yake ya kupiga kura inapatikana" wenine walimshauri aende ofisi za NEC au awapigie simu. Cha kushangaza majina yamebandikwa lakini hakuna maelekezo kwa yule ambae hatakuta jina lake afanye nini.

Kwa kweli dalili za uchakachuaji zimeanza kuonekana mapema kabisa.
Ndo tabu yakupumuliwa kisogoni hii
 
pia kwa wale ambao hawjaona majina hadi sasa kuna madaftari ya kudumu ya wapiga kura yameletwa kila kata na hata kila ofisi za vijiji unaruhusiwa kwenda kuhakikisha jina lako katika daftari la kudumu,wahi sasa kabla ya jumapili
 
Hapo maanake wamepunguza kura za upinzani kwani wanajua chuo kikuu cha dsm wanafunzi wengi wangeweza kupigia upinzani na wachache ccm
 
Back
Top Bottom